Kanda ya Ziwa yaongoza kwa Utoaji mimba

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
16,515
28,487
Utafiti uliofanywa kwa ubia na Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu(NIMR), Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi cha Muhimbili(Muhas) na Taasisi ya Kimarekani iitwayo Guttmacher, mwaka 2013 ulibaini Kanda ya Ziwa inaongoza kwa utoaji mimba zisizo salama nchini.

Takwimu za utafiti wa Guttmacher, zinafafanua kwamba Kanda ya Ziwa inaongoza kwa asilimia 51 ambayo ni sawa na matukio 120,857 ya mimba.

Sababu za kuwepo kiwango hicho kikubwa cha utoaji mimba, inalezwa kuwa kuna kiwango kidogo sana kitaifa katika matumizi ya uzazi wa mpango, huku kukiwapo mahitaji makubwa ya ngono katika jamii hiyo.

Nyanda za Juu Kusini, ndiyo inayofuata kwa kuwa na matukio ya mimba 68,910 zilizotolewa, ambazo ni sawa na asilimia 47 ya mimba zote.

Kanda ya Magharibi ina asilimia 44 ya matukio hayo yenye mimba 59,565; Kanda ya Kaskazini ina mimba 51,965 ambayo ni sawa na asilimia 31.

Pia, Kanda ya Kati kuna matukio ya mimba 23,465 ambazo ni sawa na asilimia 28; Kanda ya Kusini mimba 21,923 ambayo ni sawa na asilimia 27; Mashariki mimba 54,655 sawa na asilimia 24,
Zanzibar ndiko kwenye kiwango kidogo kitaifa kwa kuwa na asilimia 11 pekee, ikihusisha mimba 3,714.

Sababu inayotajwa na asasi ya Guttmacher ni kwamba wanawake wa Zanzibar wanaanza kushiriki ngono wakiwa na umri mkubwa na wameolewa.

Mtafiti Profesa Andrea Pembe, kutoka Muhas anasema utafiti huo imebaini kila mwaka kuna mimba zisizotarajiwa moja na kati yao, mimba 405,000 ambazo ni sawa na asilimia 39 hutolewa katika mazingira yasiyo salama na kwa usiri.

Anasema takriban theluthi mbili ya mimba hizo zinazotolewa huendana na madhara ya kiafya kwa kukosa matibabu sahihi, inayoendana na vifo vya wanawake 1,500.

Profesa Pembe anasema Chama cha Madaktari Bingwa wa Magonjwa ya Wanawake(Agota) wamekuwa wakikumbana na matukio mengi ya namna hiyo.

Anasema katika majukumu yao, ama mtu mmoja mmoja au Agota kama chama, wamekuwa wakikumbana na matukio mengi ya wanawake kutoa mimba katika mazingira hatarishi.

Source: http://www.ippmedia.com/sw/makala/u...ngwa-nusu-ya-mimba-zisizopangwa-kanda-ya-ziwa
 
Source: UTAFITI WA MADAKTARI BINGWA: Nusu ya mimba zisizopangwa Kanda ya Ziwa | Latest News, Sports, Business, Entertainment, Features, Columnist | IPPMEDIA
 
Mahitaji makubwa ya ngono maanake nini???
Au watu wa kanda ya ziwa wa hisia za ngono kuliko sehemu nyingine

Mtafiti angesema kanda ya ziwa ina idadi kubwa ya watu ningemwelewa.
 
ulaji,dona,maboga,sato,sangara na shugul nyingi,mwil unakua safi,huko ukerewe wanapgana mikia hatari
 
Kanda ya ziwa kuna mambo ya ajabu sana sio kutoa mimba tu, hata kuua albino na vikongwe wanaongoza, sasa wanakuja na lingine la vijana kulala na bibi zao sijui ndio vijana wameamua kupumzisha wadada na utoaji mimba? wanashangaza sana.
 
Kuna ule Mkoa unaitwa Mara, Kibiblia tafsiri ya Neno Mara ni " MACHUNGU " kule shetani Ametia Kambi kabisa.
 
mmmh ila wanaume wa huko wanapenda saana chini na huwa hawangalii risk, achana na mimba ukimwi pia muda wote kunawasha
 
Back
Top Bottom