Kanda ya Ziwa ni Lowassa

Kanda ya Ziwa ni Lowassa

Mtaka yote

Senior Member
Joined
Nov 30, 2014
Posts
136
Reaction score
103
Wakazi wa Kanda ya Ziwa tunakumbuka sana juhudi za Edward Lowassa alivyofanikisha kutuletea maji kutoka ziwa Victoria baada ya kilio cha muda mrefu, tutatoa shukrani zetu kwake tarehe 25 Oktoba.

Ziara yake ukanda huu yatakua mafuriko zaidi ya Dar,Karibu shujaa wetu.

Ndg wanabodi, salaam!

Baada ya jana kupitia uzi fulani wa maandalizi ya kumpokea ENL Jijini Mwanza - taarifa kuwa Magufuli hakubaliki katika kanda yake sikuiamini. Imenichukua muda wa masaa kadhaa kufanya utafiti mdogo ili kujiridhisha na nani kati ya Edward Lowassa na Dkt. John Magufuli anakubalika. Mwanza niliongea wa watu watano (5) kwa nyakati tofauti na haya ndiyo maswali ya msingi niliyouliza:


  • Mwanza Jiji ikitokea watu kumi (10) wakienda kuchagua rais wagombea wakiwa Magufuli na Lowassa hvi wangapi kati yao watachagua Magufuli na wangapi watampigia Lowassa?


Nilijibiwa: Mtu wa 1: Lowassa anaweza kupata sita au saba

Mtu wa 2: Lowassa anaweza kupata 5 au 6

Mtu wa 3: Lowassa anaweza kupata 6

Mtu wa 4: Lowassa anaweza kushinda (hakutaka kuweka takwimu)

Mtu wa 5: Lowassa atapata kura 5 na Magufuli 5.


  • Katoro nimeuliza watu wawili (2): ikitokea watu kumi (10) wakienda kuchagua rais wagombea wakiwa Magufuli na Lowassa hvi wangapi kati yao watachagua Magufuli na wangapi watampigia Lowassa?
Nilijibiwa: Mtu wa

1: Lowassa anaweza kupata 7
Mtu wa 2: Lowassa anaweza kupata 5


  • Ushirombo nimeuliza watu wanne (4): ikitokea watu kumi (10) wakienda kuchagua rais wagombea wakiwa Magufuli na Lowassa hvi wangapi kati yao watachagua Magufuli na wangapi watampigia Lowassa?


Nilijibiwa: Mtu wa 1: Lowassa anaweza kupata 6

Mtu wa 2: Lowassa anaweza kupata 5

Mtu wa 3: Lowassa anaweza kupata 4

Mtu wa 4: Lowassa anaweza kupata 5

Baada ya kuuliza maswali kwa njia ya simu na kupata majibu haya nimeona ni vizuri niwaletee ili kama kuna waccm wanahitaji ushindi kanda ya ziwa basi waweke mkakati wa kubaini kwa nini kundi la watu fulani halimpendi Dkt. Magufuli badala yake linampenda Edward Lowassa. Aidha, kwa wale wa kundi la Lowassa utafiti huu mdogo uwasukume kuongeza jitihada za kumnadi ili ajulikane zaidi. Mimi sina kinyongo na mgombea yeyote hivyo kwa msomaji mwenye mashaka na findings hizi basi afanye utafiti wake na atuletee humu.

VIVA TANZANIA, 2015 CHAGUA RAIS UMPENDAYE MWENYE UWEZO WA KUTUVUSHA WATANZANIA
 
CCM wametangulia Bagamoyo kwa babu kuwanga. Maji ya Lowasa marefu. Ni mafuriko!
 
Ce huku mwanza tunamngoja kwa hamu rais wetu lowasa wala hatuitaji makufuri coz nchi inaenda kuwa ya umaja sa nana amtamuibia mwenzake wakati kila mtu atakuwanacho chake?milango hatufungi ng'oo makufuri ayapeleke jamaica kwa balali ili amuongezee milango tucje kumchomoa tumlete kwa wananchi
 
kanda ya ziwa, pwani, kaskazini bado wapi tena
 
Wakaz wa kanda ya ziwa tunakumbuka sana juhud za Edward Lowassa alivyofanikisha kutuletea maji kutoka ziwa victoria baada ya kilio cha muda mrefu, tutatoa shukran zetu kwake tar 25 October...Ziara yake ukanda huu yatakua mafuriko zaidi ya Dar,Karibu shujaa wetu

Peopleeee's!
 
Magufuli kawabomolea nyumba watu huko kanda ya ziwa na kachoma sana nyavu za wavuvi kwa ubabe. Nani anamtaka.....yaani hawataki hata kukuona zaidi ya wale wenye jezi za kijani. Pia nao wanajilazimisha kutabasamu
 
Back
Top Bottom