OMOYOGWANE
JF-Expert Member
- Dec 30, 2016
- 5,139
- 12,915
Habari wakuu,
Kwa wale waliowahi kufanya biashara nadhani mtanielewa haraka, Mala nyingi kabla ya kufungua biashara mpya huwa tunaangalia hiyo biashara kama ipo kwa wingi kwenye eneo husika ili usiende hapo kuepuka kutupwa nje ya game sababu ya ushindani na kugawana wateja,
Biashara za kawaida ni zile ambazo kila mtu akiwaza kuhusu biashara basi ataanza kuwaza hizo, mfano
Mikoa ya Mashariki namaanisha Dar, Pwani na MOROGORO.
Nilianza kutafuta eneo lililochangamka ili niwekeze biashara kati ya hizo hapo juu, ebwana ehhhh!!! Nilianza na nafaka, kila mtaa ninao kwenda nakuta pamefulika maduka ya nafaka kibao, hadi mitaa ya pembeni na mji kote kuna maduka za nafaka kibao, sokoni ndio usiseme mfano pale Morogoro soko kuu floor ya chini kila mtu anauza mchele [emoji2][emoji2], Morogoro ndio pametia fola.
Vibanda vya Mpesa, Tigo pesa wakala wa CRDB na NMB vimefurika unakuta vimepangana hata vitano kila mtu ni wakala,
Magenge ndio usiseme hatarii, graduates kazi tunayo.
Maduka ya dawa muhimu ni mengi sana kila kona wamekaba yaani yameshonana kama maduka ya mangi,
NDIPO NILIPOWAKUMBUKA NDUGU ZANGU WACHAGA KWANINI HUWA WANAPAKIMBIA MAKWAO NA KUAMUA KWENDA KUWEKEZA MIKOA MINGINE KWA MAFANIKIO MAKUBWA.
Kiufupi hiyo mikoa niliyoitaja sasa hivi kila mtu ni mfanya biashara.
Kanda ya Mashariki mmetisha.
Wakuu vipi huko mikoa mingine kama vile Tabora, Katavi, Singida, Shinyanga, Mwanza, Musoma, Geita n.k hali ikoje???

- Kuuza nafaka
- Kuwa wakala wa M PESA, AIRTEL, CRDB, NMB n.k
- Kuuza genge (mboga mboga +matunda)
- Library ya kukodisha CD, kurusha movies na series
- Kufungua duka la dawa muhimu
- Na zingine nyingi