Kuna kanali mstahafu wa jwtz,anaumwa sana,je jeshi laweza kutoa msaada wa matibabu?
Kweli mkuu, mimi nimepata experience hiyo kwa vile Baba yangu alikuwa Kanali mstaafu.Kwa uelewa wangu ni kuwa katika TZ hakuna institution ambayo inajali wadau [wanajeshi wakiwa kazini na hata kustaafu] kama JWTZ.
cha kufanya ni kuwa nenda kwenye kambi yeyote iliyokaribu nawe muone CO mwaleze matatizo na kama una service namba na taarifa nyingine mpatie and you will be surprised kwa kushtukia landrover iko mlangoni kumchukua 'mtu wao'
Pole sana bro
Kweli mkuu, mimi nimepata experience hiyo kwa vile Baba yangu alikuwa Kanali mstaafu.
Baba yangu aliugua na hatimaye kufariki, JWTZ walishughulika sana kwa hatua zote mpaka mazishi.
Nimelipenda na kuliheshimu sana JWTZ kwa kujali sana wastaafu wao.
JWTZ ni sehemu moja hawawasahau wastaafu wao kwa lolote lile, na mimi vile vile sitawasahau kwa uadilifu wao.
Humu ndani kuna wanajamvi ambao kwao kila issue ni negativeism na wanapenda kuambikiza wenzao.Kama ni mstaafu kwisha habari yake serikali ya CCM baada ya kuwatumia wanajeshi wake na wanapostaafu huwa kama TOILET-PAPER huwatupilia mbali na kuwasahau kabisa maana hawana faida,mfano wastaafu wote tuliopigana vita vya KAGERA serikali haina na wala haijui kama sisi tulipigana vita kwa ajili ya kulinda nchi yetu.
Wengi wa wastaafu wa jeshi wanjifia majumbani mwao bila msaada wa serikali,Angalia hata Afande MAYUNGA serikali ilimwacha tu mpaka hali yake ilipokuwa mbaya sana ndipo eti ikakurupuka kumpeleka INDIA wakati ilijua kuwa huyu Kwisha kazi.Hata kama watampeleka Lugalo jeshi halina mpango naye tena hapa tatizo ni sera mbaya za nchi yetu hasa kuhusu wastaafu.
Mkuu masopakyindi inategemea Baba yako alikuwa na ushawishi gani,pengine kuna wakubwa wa JWTZ walikuwa wakimjua.Naishi na jirani yangu Lt Col mstaafu hali yake inatisha sitamani mwanangu au mtu yoyote ninayemfahamu ajiunge na JWTZ au jeshi la polisi maisha baada ya kustaafu ni magumu sana kwa askari wengi.
I beg to differ with you. Sema hao wazee walichanga vibaya karata zao, labda walikalia kunywa bia za motisha. Leo nenda ukaone jeshini vifaa vya ujenzi ni bei nafuu (free tax),bidhaa ni nyingi kwa bei za kutupwa hata sisi raia siku hizi tunaponea huko. Usije ukamkatalia mwanao au ndugu yako kwa ku-cite mifano isiyolingana na hali halisi
Jamani hizo lawama mnazotoa si kweli fahamu kuwa wapo mnaowaita WASTAAFU lkn waliacha au kijiuzulu utumishi wajeshi kwa makosa ya kinidhamu! wako wengi hata wenyewe hawapendi kujulikana kuwa walikuwa huku!! Kwa huyu anaeugua tafadhali toa maelezo hata kwa mshauri wa mgambo wilayani utaona vijana watakuja mchua haraka, Jeshi haliwaachi waliokuwa ktk utumishi maana waliopo pia watu