Kanali mstahafu wa jeshi anapoumwa jeshi laweza kusaidia matibabu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kanali mstahafu wa jeshi anapoumwa jeshi laweza kusaidia matibabu?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mnyella, Sep 19, 2012.

 1. M

  Mnyella Member

  #1
  Sep 19, 2012
  Joined: Aug 8, 2012
  Messages: 43
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Kuna kanali mstahafu wa jwtz,anaumwa sana,je jeshi laweza kutoa msaada wa matibabu?
   
 2. m

  muafaka Senior Member

  #2
  Sep 19, 2012
  Joined: Oct 30, 2009
  Messages: 102
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Nadhani ungemtaja kwa jina na mahali alipo ingefaa zaidi
   
 3. Nyenyere

  Nyenyere JF-Expert Member

  #3
  Sep 19, 2012
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 8,568
  Likes Received: 1,934
  Trophy Points: 280
  Mpeleke Lugalo au hospitali yoyote ya kijeshi apate tiba.
   
 4. Echolima

  Echolima JF-Expert Member

  #4
  Sep 19, 2012
  Joined: Oct 28, 2007
  Messages: 3,169
  Likes Received: 531
  Trophy Points: 280
  Kama ni mstaafu kwisha habari yake serikali ya CCM baada ya kuwatumia wanajeshi wake na wanapostaafu huwa kama TOILET-PAPER huwatupilia mbali na kuwasahau kabisa maana hawana faida,mfano wastaafu wote tuliopigana vita vya KAGERA serikali haina na wala haijui kama sisi tulipigana vita kwa ajili ya kulinda nchi yetu.
  Wengi wa wastaafu wa jeshi wanjifia majumbani mwao bila msaada wa serikali,Angalia hata Afande MAYUNGA serikali ilimwacha tu mpaka hali yake ilipokuwa mbaya sana ndipo eti ikakurupuka kumpeleka INDIA wakati ilijua kuwa huyu Kwisha kazi.Hata kama watampeleka Lugalo jeshi halina mpango naye tena hapa tatizo ni sera mbaya za nchi yetu hasa kuhusu wastaafu.
   
 5. Abunwasi

  Abunwasi JF-Expert Member

  #5
  Sep 20, 2012
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 3,166
  Likes Received: 1,064
  Trophy Points: 280
  Kwa uelewa wangu ni kuwa katika TZ hakuna institution ambayo inajali wadau [wanajeshi wakiwa kazini na hata kustaafu] kama JWTZ.
  cha kufanya ni kuwa nenda kwenye kambi yeyote iliyokaribu nawe muone CO mwaleze matatizo na kama una service namba na taarifa nyingine mpatie and you will be surprised kwa kushtukia landrover iko mlangoni kumchukua 'mtu wao'
  Pole sana bro
   
 6. masopakyindi

  masopakyindi JF-Expert Member

  #6
  Sep 20, 2012
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 13,918
  Likes Received: 2,348
  Trophy Points: 280
  Kweli mkuu, mimi nimepata experience hiyo kwa vile Baba yangu alikuwa Kanali mstaafu.
  Baba yangu aliugua na hatimaye kufariki, JWTZ walishughulika sana kwa hatua zote mpaka mazishi.
  Nimelipenda na kuliheshimu sana JWTZ kwa kujali sana wastaafu wao.

  JWTZ ni sehemu moja hawawasahau wastaafu wao kwa lolote lile, na mimi vile vile sitawasahau kwa uadilifu wao.
   
 7. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #7
  Sep 20, 2012
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,635
  Trophy Points: 280
  Mkuu masopakyindi inategemea Baba yako alikuwa na ushawishi gani,pengine kuna wakubwa wa JWTZ walikuwa wakimjua.Naishi na jirani yangu Lt Col mstaafu hali yake inatisha sitamani mwanangu au mtu yoyote ninayemfahamu ajiunge na JWTZ au jeshi la polisi maisha baada ya kustaafu ni magumu sana kwa askari wengi.

   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 8. Bilionea Asigwa

  Bilionea Asigwa JF-Expert Member

  #8
  Sep 20, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 12,629
  Likes Received: 9,846
  Trophy Points: 280
  siku hizi hata kutibiwa kwa wastaafu wa majeshi yetu inategemea na kamtandao gani ulikua nako pindi ulipokuwa kazini...
  kama ulikuwa kazini kwa manufaa ya umma bila kuangalia next side imekula kwako
  mifano iko mingi sana mitaani jinsi hawa wastaafu wanavyochapika na hali ngumu ya kimatibabu
   
 9. Abunwasi

  Abunwasi JF-Expert Member

  #9
  Sep 20, 2012
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 3,166
  Likes Received: 1,064
  Trophy Points: 280
  Naomba uwajaribu JWTZ halafu uone.
  Kama una ndugu ambaye ni mjeshi mstaafu [whatever the cheo] nenda katoe taarifa kwenye kambi yoyote ile iliyokaribu na mjeshi mgonjwa wape particulars za mgonjwa halafu uje kwenye baraza hili utusute.
  Acheni kuzungumza mambo kijumla jumla tuu
   
 10. Abunwasi

  Abunwasi JF-Expert Member

  #10
  Sep 20, 2012
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 3,166
  Likes Received: 1,064
  Trophy Points: 280
  Humu ndani kuna wanajamvi ambao kwao kila issue ni negativeism na wanapenda kuambikiza wenzao.
  jamani tujifunze kuita spade a spade lakini tukiona ni spoon tuseme
   
 11. Fugwe

  Fugwe JF-Expert Member

  #11
  Sep 20, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 1,680
  Likes Received: 230
  Trophy Points: 160
  I beg to differ with you. Sema hao wazee walichanga vibaya karata zao, labda walikalia kunywa bia za motisha. Leo nenda ukaone jeshini vifaa vya ujenzi ni bei nafuu (free tax),bidhaa ni nyingi kwa bei za kutupwa hata sisi raia siku hizi tunaponea huko. Usije ukamkatalia mwanao au ndugu yako kwa ku-cite mifano isiyolingana na hali halisi
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 12. K

  Kindimbajuu JF-Expert Member

  #12
  Sep 20, 2012
  Joined: Jul 8, 2009
  Messages: 711
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  maelezo yako ni tofauti na madai ya ngongo. kuchanga karata vibaya isiwe sababu ya wastaafu kupuuzwa. ndo maaana tuna mifuko ya hifadhi za jamii , moja ya wajibu wa hiyo mifuko ni kuhakikisha wastaafu wanalindwa kwa wakati wa uzee wao. kuchanga karata unakosema siyo njia sahihi ya kutatua tatizo hili, aidha isitumiwe kama sababu ya majeshi kushindwa kuandaa schemes ya kufaa ya maisha uzeeni kwa wafanya kazi wake.

  nakushauri usitafute njia fupi kutatua tatizo la kudumu, kuchanga karata hakuta maliza tatizo kwakuwa ukumbuke wakati unaumwa waweza hata kukosa wa kuhakikisha pesa hiyo yako mwenyewe inakutibu. wapo wanakufa na pesa zao bank. uzee ni kama utoto , mzee akiumwa anaihtaji mwongozo wa wapi kupata tiba na hatimaye kutibiwa.ktk hali ya uzee na kuumwa, pesa ina mipaka yake, hata ukiwa na pesa, pasipo namna ya kusaidiwa kufikishwa kwenye huduma na hata kumanage hiyo pesa ni sawa na kuwa masikini tu
   
 13. M

  Malipo kwamungu JF-Expert Member

  #13
  Sep 20, 2012
  Joined: Mar 12, 2012
  Messages: 574
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Jamani hizo lawama mnazotoa si kweli fahamu kuwa wapo mnaowaita WASTAAFU lkn waliacha au kijiuzulu utumishi wajeshi kwa makosa ya kinidhamu! wako wengi hata wenyewe hawapendi kujulikana kuwa walikuwa huku!! Kwa huyu anaeugua tafadhali toa maelezo hata kwa mshauri wa mgambo wilayani utaona vijana watakuja mchua haraka, Jeshi haliwaachi waliokuwa ktk utumishi maana waliopo pia watu
   
 14. Echolima

  Echolima JF-Expert Member

  #14
  Sep 20, 2012
  Joined: Oct 28, 2007
  Messages: 3,169
  Likes Received: 531
  Trophy Points: 280
  Mimi ni askari mstaafu mpaka sasa hivi ninapoandika hakuna chochote ambacho jeshi linaweza kusaidia mtu aliyestaafu labda usaidiwe na wanjeshi wanaokujua na uliofanya kazi nao wao wachange pesa yao mfukoni wakusaidie.
  Hapa kinachogomba serikari haina sera ya kusaidia wastaafu wewe ukishatoka kafe rwako,tatizo hili si mimi tu waulize wastaafu waliopigana vita vya kagera hakuna hata mmoja ambaye alifaidika na mafao ya aina yoyote pamoja na kwamba tulijitoa kwa ajili ya nchi yetu,Waangalie wastaafu wote wa JWTZ wengi wao siku hizi ni walinzi kwenye maduka ya wahindi ni aibu sana kwa nchi yetu njinsi inavyowazalilisha wastaafu wa jeshi.
   
 15. Mwitongo

  Mwitongo JF-Expert Member

  #15
  Sep 20, 2012
  Joined: Jan 30, 2009
  Messages: 311
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Tatizo ni kwamba JWTZ, POlisi, Magereza,Usalama wa Taifa (wa viongozi?) wanapokuwa madarakani wanajisahau sana. Kazi yao kubwa ni amri na kupata upendeleo kwa kila jambo. Wanapostaafu wengi wanakuja uraiani wakiwa ma-Lena wa mnaisha. Hiyo inatosha kabisa kuwafanya maisha yao yawe mafupi maana hakuna wa kumkomandi wala wa kumpa kitu cha bure. Wakiishi vema, watastaafu na kuaga dunia kiungwana.Unadhani Kamuhanda ataishi maisha gani baada ya kustaafu?
   
Loading...