Comred Mbwana Allyamtu
JF-Expert Member
- Jun 28, 2016
- 351
- 866
KANALI KASHMIR NA KANALI MAHFOUDH WALIVYOSAIDIA KUPATIKANA KWA UHURU WA MSUMBIJI
Na. Simon Noel
Jeshi letu la wananchi wa Tanzania JWTZ limetimiza miaka zaidi ya hamsini sasa huku likiwa na rekodi ya aina yake kama jeshi shupavu liliongoza mapambano dhidi ya udhalimu na uonevu uliokuwa ukifanywa na makaburu, Wareno na wazungu wachache huko kusini mwa Africa
Tanzania ndio ilikuwa kitovu cha mapambano na makao makuu ya wapigania uhuru kwa kipindi chote cha mapambano.
Katika mapambano haya Kuna baadhi ya watanzania ambao walijitoa kikamilifu kuhakikisha nchi za kusini mwa Africa zinakuwa huru kutoka kwenye makucha ya wakoloni wadhalimu.
Baadhi ya watanzania hao ni marehemu Brigadier Hashim Mbita, marehemu Kanali Ali Mahfoudh, kanali Ameen Kashmir na General Sarakikya.
Watanzania hawa walikuwa mstari wa mbele kabisa kuhakikisha waafrika wenzao wanakombolewa na kazi yote hii ilifanywa chini ya amir Jeshi mkuu wa Tanzania Mwalimu Julius Nyerere.
Ili kuyajua haya na mengineyo ninafunga safari mpaka Upanga na kukutana na aliyekuwa mnadhimu mkuu wa jeshi la wananchi wa Tanzania JWTZ 1964-1974 mzee kanali Kashmir ambaye namuomba anieleze hatua kwa hatua juu ya mchango wake na wa wenzake katika ukombozi wa kusini mwa Africa.
Mzee Kashmir ananipokea kwa bashasha na ucheshi na ananiambia kuwa angependa sana kunielezea juu ya mchango wake katika mapambano dhidi ya Wareno nchini Msumbiji kwani ndiko haswa alisimamia na kuongoza Mapambano halisi dhidi ya udhalimu na uonevu wa wakoloni wakatili Wareno.
Mzee Kashmir ananiambia kuwa kama kuna mtu ambaye angestahili kupewa heshima na waafrika wote kwa mchango wake na upendo wake kwa waafrika wenzake basi mtu huyo ni mwalimu Nyerere. Na mpaka Sasa anashangaa sana ni kwa nini Africa haijautambua mchango wa mwalimu Nyerere na wala hata haijaweka siku maalum ya kumkumbuka.
Mzee Kashmir anaendelea kunielezea kuwa mara tuu baada ya kuundwa kwa JWTZ mwalimu Nyerere aliandaa mazingira ya kuwasaidia wapigania uhuru wa nchi za kusini mwa Africa na kwa kusema ukweli kabisa yeye mwenyewe mwalimu ndie haswa aliyewashawishi wanaharakati wa kusini mwa Africa kuanzisha mapigano ya kuzikomboa nchi zao. Kwa hiyo ndio kusema kuwa kama isingelikuwa uthubutu wa mwalimu Nyerere huenda mpaka leo Msumbiji ingekuwa chini ya ukoloni wa Wareno au labda ingechelewa sana kupata uhuru.
Umoja wa nchi huru za Africa OAU nao haukuwa nyuma katika kuunga mkono harakati hizo na mara moja walianzisha kamati ya ukombozi wa Africa ambayo makao makuu yake yaliwekwa hapa Dar es Salaam Tanzania. Mzee Kashmir anasema kuwa hata FRELIMO yenyewe ilianzishwa kwa msaada wa mwalimu Nyerere.
Mzee Kashmir ananiambia kuwa anakumbuka mwishoni mwa mwaka 1964 ndio walipokea vijana wa mwanzo kabisa waliokuwa wakihitajika kupatiwa mafunzo ya kijeshi. Sikumbuki vizuri idadi yao lakini walikuwa wapo zaidi ya 20. Wengi Kati ya vijana hao walikuwa ni wanafunzi wa vyuo vikuu ambao waliacha vyuo huko ureno na Kuja kujiunga na harakati za ukombozi wa nchi yao. Baadhi ninaowakumbuka ni Philipe Magaia, Samora Machel, Joachim Chisano, Raimundo Pachinuapa, Alberto Chipande na Marcelino Dos Santos.
Hawa tulivyowapokea tuliwapatia kwanza mafunzo ya kijeshi na baadae mafunzo ya kisiasa maana Mwalimu alitushauri tufanye hivyo kwa kuwa nao pia ingawa wataenda kupigana vita lakini ni vita ya kupigania uhuru hivyo ni lazima waielewe siasa. Kipindi hicho FRELIMO ilikuwa chini ya uongozi wa Dr Mondlane.
Mara tuu baada ya kuwapatia mafunzo hapa nchini Tanzania tuliwasafirisha mpaka nchini Algeria ili kupatiwa mafunzo zaidi na haswa kujifunza kupigana na taifa kubwa huku mkiwa na jeshi ambalo sio imara sana. Ikumbukwe kuwa Algeria ilikuwa imetoka kupigana vita ya kuikomboa nchi yao dhidi ya wakoloni wafaransa hivyo ilikuwa ni sehemu sahihi kabisa ya kupata uzoefu na ujuzi wa kupambana dhidi ya wakoloni wadhalimu Wareno. Nakumbuka hiyo ilikuwa ni Kati Kati ya mwaka 1965.
CUBA YAINGILIA KATI KUTOA MSAADA.
habari hizo za Tanzania kuandaa mpango wa kivita wa kuzikomboa nchi za kusini mwa Africa zilienea Duniani kama ujuavyo Dunia yetu vita sio jambo la siri haswa ukizingatia Kila nchi ina mifumo yake ya ujasusi wa kupata habari za usalama wa ndani na nje ya nchi yake.
Habari hizo zikawafikia wanaharakati wa Cuba ambao walikuwa wameuondoa utawala wa dikteta Batista na kuanzisha serikali ya kimapinduzi nchini humo.
Kwa kuheshimu harakati zetu serikali ya Cuba ikatuletea mpiganaji wa msituni aliyeitwa Pablo Ribalta Kuja kuwa balozi wa Cuba nchini Tanzania. Nia haswa ikiwa ni kutusaidia kushinda vita hiyo ya ukombozi kusini mwa Africa.
PABLO RIBALTA ALIKUWA NI ZAIDI YA BALOZI.
kwa kweli kabisa Pablo Ribalta alikuwa ni zaidi ya balozi kwetu. Mara tuu baada ya kuwasili nchini kwetu alikuwa karibu sana na sisi hatua kwa hatua akitushauri nini haswa tufanye ili kuweza kushinda vita hiyo. Baada ya muda mchache tuu wa kukaa na sisi na kuona ari yetu tuliyokuwa nayo alifanya mpango wa kumleta mpiganaji maarufu wa msituni aliyekuwa amebobea katika vita vya ukombozi Ernesto Che Guevara.
Itaendelea..............
Simon Noel
A. K. A Bob Sai
Rais wa vijana Tanzania
Fuatilia mfululizo wa makala hizi ili upate kufahamu mengi juu ya mchango wa Tanzania katika ukombozi wa kusini mwa Africa