Kamwe siwezi kulidharau dafu huku nikijua embe ni tunda la msimu

Mchimwachimego

JF-Expert Member
Jun 15, 2020
358
271
Taifa letu kwa sasa kuna uchaguzi lakini kuna jambo ambalo si tu kwamba lakijinga bali ni lakishetani sana, katika mitazamo ya kawaida unaweza ukadhani vijana wamevutishwa bhangi lakini uhalisia ni kwamba shetani ana nguvu sana, kwa tabia ambazo watu hasa vijana wanazionyesha katika mikutano ya lisu ni wazi kwamba haya ni matokeo ya kizazi cha wajinga ,wavivu na maskini wa kifikra.

Vijana na watu walio wengi bado wanaamini katika urais wa kila kitu ni ruksa ili hali hawajui madhara ya taifa la namna hiyo, ukiangalia ushabiki wa wale wafuasi wa lisu ni vitu ambavyo havitaliendeleza taifa ni ujinga tu mtu anawaambia maendeleo ya vitu hayaitajiki huku akilalamikia kunyimwa kivuko,akihaidi kujenga daraja kati ya kisiwa na kisiwa ,treni za mijini NK. Katika mambo yaliniudhi kabisa hawa vijana kushabikia ni vyeti feki, watumishi hewa ,vitambulisho vya machinga , uvuvi haramu , ushoga na mengine mengi ambayo hayawezi kulisaidia taifa kwa wakati huu labda lile la katiba mpya na mfumo wa elimu na japo yapo baadhi ni mazuri .

Watu wengi tunafahamu kwamba vijana walio wengi hawana elimu ya uchambuzi wa hoja wanadhani kwamba lisu atakuja kugawa pesa , hawafaamu kuwa namna atakavyooendesha nchi lisu italeta madhara makubwa kwa taifa hili kwa sababu yeye anataka watu wawe na pesa bila kujali wamepataje, anataka watu wawe huru wafanye watakacho hii nchi itarudi nyuma sana.

Mifano ipo mingi ila tujaribu kuangalia ngazi ya familia : katika familia kama mukiamua kuwa tuishi huru bila kufuatiliana kila mtu atafuraia maisha ila mwisho wa familia hiyo hauwezi kuwa mzuri lazima kuna mengi yataiangamiza.

Tunaitaji mabadiliko lakini si kila mabadiliko yana tija na sio sawa kubadili kiongozi kama nguo vijana badilikeni licha ya kwamba nafahamu kuwa neno ningejua huwa halitangulii.
 
Wamekwisha lewa sera hewa za ubelgiji. Hawatakuelewa mkuu.
Kiukweli ukimsikiliza lisu anaongea kupinga kila kilichofanywa na serikali as if hakusoma hapa nchini tena kwa kodi za watanzania.

Ni kama katokea ulaya na kutua na hataishi hapa baada ya uchaguzi.

Ametudharau watanzania hadi wazazi wake. Tanzania ni kama hatuhitaji miundombinu wala vitu. Tunahitaji pesa tu? Ametudharau sana.

Mungu ampe adhabu ya kutosha kujitambua na awaombe radhi watanzania.

Sent from my Infinix X680 using JamiiForums mobile app
 
Mkuu hii hoja ni ya kiwango cha juu, wanazi wa mlengo fulani hawatachelewa kukutusi.

October 28th kura zote za ndio ni kwa JPM

JPM ANATOSHA
CCM KWA MAENDELEO YA TANZANIA
 
Matapeli huwa wanazungumza sana.

Chadema wanachokifanya ndio hicho,

Kiuhalisia hawana uwezo wa kuunda serikali bila kutegemea watu toka CCM.

Hakuna haja ya kumpa mtu kura akafanye jambo ambalo hana uwezo nalo.

Kuichagua Chadema ni sawa na kuharibu kura tu.
 
We will go with Magufuli because he loves the development of his people because everywhere you go there's electricity and hospitals have been building everywhere Maguguli has done a lot
 
Back
Top Bottom