Kamwaga kamwaga ukweli hadharani! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kamwaga kamwaga ukweli hadharani!

Discussion in 'Sports' started by ZENITH, Aug 30, 2012.

 1. ZENITH

  ZENITH JF-Expert Member

  #1
  Aug 30, 2012
  Joined: Feb 5, 2012
  Messages: 732
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 60
  Ni kuhusu suala la kuwapa mgao vijana wao baada ya kutwaa ubingwa wa super 8.Kamwaga kasema kwamba ni hiari ya uongozi wa simba kuwapa madogo mgao au kutowapa na hawashurutishwi na mtu yoyote kuwapa madogo mgao huo. Akizidi kutiririka zaidi,kamwaga alisema vijana wao waliotwaa ubingwa wa super 8 ni waajiriwa wa SSC na wanalipwa mshahara kila mwisho wa mwezi hivyo siyo lazima wao kupewa huo mgawo.
   
 2. Anselm

  Anselm JF-Expert Member

  #2
  Aug 30, 2012
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 1,705
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Umeona enh....yaani hawa Rage,Kaburu na Kamwaga wameigeuza hii team kama bidhaa yao binafsi,wanafanya vile wanavyojisikia,wamedhurumu rambirambi ya watu,sasa wanadhurumu jasho la madogo,mxsyyzzsxsss!!!!
   
 3. J

  Joo Wane JF-Expert Member

  #3
  Aug 31, 2012
  Joined: Mar 14, 2007
  Messages: 348
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 45
  Hao viongozi wa simba sasa wanapitiliza kwa tamaa ya hela. Wachezaji 27 pamoja na benchi la ufundi hawatazidi 35 jumla yao, zawadi millioni 40. Wapeni millioni moja moja wote zinazobaki ndio viongozi wachukue. Mimi hao viongozi walinishangaza sana kwenye issue ya Mafisango. Walizungumza kwa huzuni sana wakati wa msiba na hela zikachangwa nyigi tu. Baada ya mazishi na kutafuna hela mara ooh hatukuwa na mkataba na mafisango, mara ooh zilipatikana millioni saba tu na ndio zilisafirisha mwili wa marehemu mpaka kongo na blah blah kibao. Wapeni madogo pesa zao mmeshatafuna za mafisango, za usajili feki, za uwanja wa bunju, n.k. zinatosha jamani.
   
 4. mpalu

  mpalu JF-Expert Member

  #4
  Aug 31, 2012
  Joined: Sep 15, 2010
  Messages: 2,491
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 145
  ni kweli mkuu mwisho timu inakaribisha laana tu unajua watu kunung'unika co vizuri..
   
 5. p

  pilau JF-Expert Member

  #5
  Aug 31, 2012
  Joined: Aug 16, 2012
  Messages: 1,523
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  Kwa swala hili la kudhulumu "madogo" limewakera watu wengi sana, Viongozi wa Simba mkiongozwa na Alhaji Rage (mzee wa bastola) mswalieni Mtume S. A. W jasho la mtu haliendi bure pengine mlikosea mngekubaliana na vijana kabla ya mambo ya yote, sio mlipoona PESA udenda unawatoka na kuamua kuwafanyia mtima nyongo watoto wa wenzenu
   
 6. J

  Joo Wane JF-Expert Member

  #6
  Aug 31, 2012
  Joined: Mar 14, 2007
  Messages: 348
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 45
  Aisee pesa tamu. Kwa taarifa za chini chini madogo wametrain na matola kwa shida sana hakuna kiongozi yeyote aliyekuwa anahangaika natimu zaidi ya Matola na bwana mmoja aliyekuwa anaisaida timu kifedha anayeitwa patrick rweyemamu (sina uhakika na jina nipo tayari kusahihishwa). Mwishoni madogo wamewin viongozi wanakuwa kimbele mbele kupiga picha na kujifanya wanajua sana kugawanya pesa za zawadi na kujitia ooh tutawapandisha daraja vijana wetu kwenye timu ya wakubwa. Hivi hawa wakina Rage kweli wangekuwa wanijua simba B vizuri (na wanajua mpira vizuri) wangeenda rwanda kuingizwa mkenge wa usd 30,000 na sijui huyu mchovu mzee twita sijui base (twitte) au kusajili mara musombo, mara kanumbiyavanga wakati vifaa vipo hapo hapo Msimbazi?. Haki ya mtu haipotei bure na mikosi itaendelea simba iwapo hamtapeleka rambi rambi za mafisango ambaye kwa mwaka mmoja tu amefanya mambo makubwa msimbazi. Na mkiwadhulumu tu hao madogo ndio mtaongeza laana msimbazi.
   
 7. r

  rodrick alexander JF-Expert Member

  #7
  Aug 31, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 4,109
  Likes Received: 1,499
  Trophy Points: 280
  Rage aliingia Simba si kwa ajili ya kuleta maendeleo ukiangalia kilio alichokuwa anatoa wakati wa msiba wa Mafisango lakini mpaka leo wameshindwa kupeleka rambirambi lakini wa kulaumiwa ni wanachama wa simba kwani wameshindwa kuchagua viongozi makini mpaka sasa ameiletea simba hasara zaidi heri ya Dalali pamoja na kutokuwa na elimu aliiongoza simba vizuri
   
Loading...