Kampuni za simu mjitathmini. Huduma za internet mbovu

Nini internet mkuu? Hata kupigia mtu tuu au kupokea simu network inasumbua vibaya mno,
Tena unajiuliza hapa nipo Dar je huko mikoani hali ikoje
 
Kichwa cha habari hapo juu chahusika.

Sina mengi, tunashindwa kuenjoy simu zetu bwana very slow internet service.
Fiber, Fiber, Fiber! Bila kuwekeza kwenye fiber matatizo yataendelea kuwepo. Wireless connection haijawahi kushindana na fiber hata siku moja. Hata ukienda kwenye zile nchi zenye 4G ya uhakika utakutana na changamoto za wireless.
 
Kweli kabisa leo nikadhani sehemu niliopo ndo tatizo kumbe limewakuta na wengine pia.
 
Maisha bwana...!? We ukisema cha nini, wenzako wanasema watakipata lini.

Bora nyiny huko mtandao mnao ila upo slow! Kuna sehemu nlienda vijijini (Kisarawe) kuna mnara ila unatumia nishati ya solar. Kama kuna mawingu hakuna mawasiliano hapo. Hata jua likiwepo, mawasiliano kwanzia saa tatu asubuh had tano usiku.

Sijui walitumia teknolojia gan hapo. Hovyooo...!
 
Back
Top Bottom