Kampuni za Simu Kuhodhi namba

bnhai

JF-Expert Member
Jul 12, 2009
2,824
2,381
Watu wasiporidhishwa na huduma za kampuni moja ya simu wanshindwa kuhamia kampuni nyingine kutokana na gharama za kuhama, "switching costs".

Gharama za kuhama si shs 1000 ya line bali ni gharama ya kutafutwa na kutopatikana ndio inayofanya watu waendelee kuabudia kampuni zao hata kama kuna kero au unafuu sehem nyingine.

Hii pia inafanya kampuni mpya kutaabika kuingia sokoni kwa sababu watu hawawezi kupoteza namba kisa kuhamia kampuni nyingine.

Pendekezo; TCRA ingeondoa ukiritimba wa kwamba 075/071/078....... kuwa ni wa kampuni.

Ni vyema tukaiga nchi nyingine ambapo unaweza kuhama kampuni ya simu moja kwenda nyingine kwa namba yako. Hii itaongeza ushindani na kuondoa ubabaishaji.

Suala la kutambua hii ni voda au tigo ili mtu apate huduma za bei rahisi zitabaki kwenye watumiaji au makampuni kutengeneza query service itakayoonyesha hii ni namba ya kampuni gani.
 
Last edited by a moderator:
Wazo zuri aisee.Hii itasaidia kuondoa huu ukiritimba wa kuhodhi namba za wateja.
 
  • Thanks
Reactions: PNC
Amiin ! yaani mleta hoja ungejua hii ndio dua yangu ya siku zote !hapa nilipo nina line za mitandao yote kasoro ile iliyojikita Darisalama tu kama tapeli vile! namba iwe mali yangu naamua kuingia contract na kamuni yeyote ile baasi!ukileta ukhanithi mwezi huu mwezi ujao niko voda,halotel,tigo,etc ni mwendo wa mduara tu mpaka akili ziwakae sawa! atayejiona anahamwa hamwa atajijua wapi mbovu!
 
Watu wasiporidhishwa na huduma za kampuni moja ya simu wanshindwa kuhamia kampuni nyingine kutokana na gharama za kuhama, "switching costs".

Gharama za kuhama si shs 1000 ya line bali ni gharama ya kutafutwa na kutopatikana ndio inayofanya watu waendelee kuabudia kampuni zao hata kama kuna kero au unafuu sehem nyingine.

Hii pia inafanya kampuni mpya kutaabika kuingia sokoni kwa sababu watu hawawezi kupoteza namba kisa kuhamia kampuni nyingine.

Pendekezo; TCRA ingeondoa ukiritimba wa kwamba 075/071/078....... kuwa ni wa kampuni.

Ni vyema tukaiga nchi nyingine ambapo unaweza kuhama kampuni ya simu moja kwenda nyingine kwa namba yako. Hii itaongeza ushindani na kuondoa ubabaishaji.

Suala la kutambua hii ni voda au tigo ili mtu apate huduma za bei rahisi zitabaki kwenye watumiaji au makampuni kutengeneza query service itakayoonyesha hii ni namba ya kampuni gani.
Uko sahihi mkuu sijui kama wahusika watakuwa wasikivu.
 
Ukifanikiwa utusaidie na kuwaambia TCRA tuwe tunaweza kulipia vifurushi vya azam kwa kutumia decoder na namba ya akaunti ya DSTV.
 
Voda ningewahama siku hiyo hiyo.... Wananikera sana.

Navumilia tu kwakuwa ni laini Inayojulikana na watu wangu.
 
Hoja nzuri sana , naomba ifanyiwe kazi tu maana hakuna namna sasa.
 
Yaani wewe mleta Mada kwa maono yako unafaa kuongoza ka inji fulani, ambako ni..............!"

.
.
 
Hiyo issue mbona ishahadiliwa humu kitambo? Inaitwa Number Management Portability(NMP) ipo mbioni kuanza wewe ndio utakuwa na umiliki wa Hiyo line ,line yako ya tigo unaweza ukaipeleka halotel kwa ridhaa yako mwenyewe....Nimeongea na mshikaji wa TCRA amesema itaanza mwezi wa pili kwa kampuni nne kwanza Airtel,Voda,smile na tigo kampuni nyingine ndio zinaendelea na installation.
 
Hii ni kweli... hakuta kuwa na maana kiwa na line mbili..
 
Watu wasiporidhishwa na huduma za kampuni moja ya simu wanshindwa kuhamia kampuni nyingine kutokana na gharama za kuhama, "switching costs".

Gharama za kuhama si shs 1000 ya line bali ni gharama ya kutafutwa na kutopatikana ndio inayofanya watu waendelee kuabudia kampuni zao hata kama kuna kero au unafuu sehem nyingine.

Hii pia inafanya kampuni mpya kutaabika kuingia sokoni kwa sababu watu hawawezi kupoteza namba kisa kuhamia kampuni nyingine.

Pendekezo; TCRA ingeondoa ukiritimba wa kwamba 075/071/078....... kuwa ni wa kampuni.

Ni vyema tukaiga nchi nyingine ambapo unaweza kuhama kampuni ya simu moja kwenda nyingine kwa namba yako. Hii itaongeza ushindani na kuondoa ubabaishaji.

Suala la kutambua hii ni voda au tigo ili mtu apate huduma za bei rahisi zitabaki kwenye watumiaji au makampuni kutengeneza query service itakayoonyesha hii ni namba ya kampuni gani.
Hakika wewe ni muona mbali, hayo ni maoni yalioenda shule
 
Mtandao gani huu? ndio naanza kuusikia leo

Hiyo issue mbona ishahadiliwa humu kitambo? Inaitwa Number Management Portability(NMP) ipo mbioni kuanza wewe ndio utakuwa na umiliki wa Hiyo line ,line yako ya tigo unaweza ukaipeleka halotel kwa ridhaa yako mwenyewe....Nimeongea na mshikaji wa TCRA amesema itaanza mwezi wa pili kwa kampuni nne kwanza Airtel,Voda,smile na tigo kampuni nyingine ndio zinaendelea na installation.
 
Huo mpango upo na mimi ni moja ya expert tutakaodeploy project hiyo katka kampuni yangu.. mwezi ujao project inategemewa kuanza hiyo itasaidia watu kupoteza watu wao kuhangaika kuwajulisha watu kuhusiana na namba mpya pind unabadili namba
 
Back
Top Bottom