Kampuni ya Wengert katika kashfa ya bangi

MzeePunch

JF-Expert Member
Jun 8, 2009
1,412
203
Wengert katika kashfa ya bangi:

Kampuni hii ya Kimarekani ambayo imekuwa ikikiuka order za serikali na kung'ang'ania vitalu vya uwindaji sasa inazua maswali mengi. Mwaka uliopita gari moja ya kampuni ya Wengert Windrose Safaris ilikamatwa huko Arusha ikiwa na shehena ya bangi.

Mtuhumiwa hadi hivi leo hajafikishwa mahakamani licha ya kukamatwa red-handed akiwa na bangi kama inavyoonekana pichani. Inadaiwa kuwa wahusika wakuu wa mzigo huo hawajakamatwa hadi leo.

Nani anawalinda wahalifu hawa? Je, hiyo ndio sababu ya kung'ang'ania vitalu, ili kuendeleza biashara ya bangi?
 

Attachments

  • IMG-20150325-WA0007.JPG
    IMG-20150325-WA0007.JPG
    145.5 KB · Views: 65
  • IMG-20150325-WA0002.JPG
    IMG-20150325-WA0002.JPG
    127.7 KB · Views: 57
  • Wengert Bangi5.jpg
    Wengert Bangi5.jpg
    142 KB · Views: 64
  • Mtuhumiwa.JPG
    Mtuhumiwa.JPG
    51.8 KB · Views: 53
Tatizo bangi tunazovuta siku hizi sio walizovuta akina bob marley na lucky dube
 
Tatizo bangi tunazovuta siku hizi sio walizovuta akina bob marley na lucky dube
Mkuu ukiachana na Bob Marley, unaweza kutupa citation yoyote inayoonyesha kwamba enzi za uhai wake Lucky Dube alikuwa anavuta bangi?
 
Hawa watu kinachoshangaza ni kwa namna gani wanaweza kufanya jambo lolote walitakalo huku wakijua kwamba si sahihi. Haiyumkiniki kwenda Marekani na kufanya mambo ya kihuni ambayo serikali ya nchi hiyo haikubaliani nayo kisheria, kanuni au taratibu. Kwa nini vyombo vyetu vya dola havichukui hatua stahiki dhidi ya genge hili? nani anawalinda? Ana nguvu gani dhidi ya serikali yote ya Tanzania?
 
hii bangi hii!! kiukweli inavutwa na watu wengi sn tena wakiamua kuweka wazi tutapigwa butwaa sn.hata huyu???
 
Nasikitika tu Tembo wetu ,miaka 20 ijayo itabidi nimwonyeshe mwanangu picha ya Tembo ,akiniuliza ulikua wapi kuzuia jambo hili lisitokee sijui nitamjibu nini ,bangi sina tatizo nayo hiyo kitu hata kwenye barafu inaota
 
Back
Top Bottom