Kampumi ya simu ya tigo wamekua wasanii sana na ukweli wameanza utapeli wa waziwazi,ni karibu mwezi wa pili sasa naamaishwa na hela yangu 175,000/= ambayo niliingiza mwenyewe kwenye akaunti yangu ya tigopesa kwa nia ya kuiifadhi,lakini baada ya siku mbili hela ile ikawa haipo tena,nimewafuatilia nenda rudi nenda rudi,majibu yao wanayonipa ni upuuzi ule ule kila siku kua line yangu ina matatizo nikae baada ya masaa 48 watanitumia msg,mpaka leo hizo masaa 48 zimepita zaidi ya ishirini!na lingine ni kua,laini yangu sasa imekua na matatizo kiasi kwamba kuna baadhi ya namba nikipiga haziendi na hata nikipigiwa baadhi ya namba pia haziingii,week iliyopita kuna rafiki yangu nae kapata tatizo ilo ilo,hela yake 81,000/= haionekani,nae wamemuambia hayo masaa yao ya kitapeli 48 mpaka leo hajapata hela yake na line yake nae imeanza kumsumbua!kuna mtu wa tigo ametutonya kua utapeli huo unafanywa na tigo/wafanyakazi wenyewe kwa nia ya kumsumbua mteja mpaka akate tamaha na hela uhamishia kwenye akaunti zao za simu ambazo ni fake na wametengeneza kwa ajili hiyo tu!na hizo kesi kwa sasa zimekua nyingi mno bila kupatiwa ufumbuzi wowote,naombeni msaada wenu wadau je nifanyaje juu ya wizi huu wa wazi wazi wa tigo?