Tanzanite One yafilisika, Watanzania wainunua
Mwandishi Wetu, Manyara
KAMPUNI ya Tanzanite One iliyokuwa ikichimba madini ya vito aina ya Tanzanite,katika mji mdogo wa Mererani, Simanjiro Mkoani Manyara imefilisika na kulazimika kuuza hisa zake zote kwa kampuni ya Sky Associates Group inayomilikiwa na watanzania.
Kampuni hiyo iliyokuwa miongoni mwa kampuni tanzu zinazomilikiwa na kampuni ya Richland Resource ya nchini Uingereza chini ya utendaji wa Bernard Oliver imeamua kuuza hisa zake ambazo ni asilimia 50 kwa kampuni hiyo ya Kitanzania kutokana na kampuni ya Tanzanite One kudaiwa kukumbwa na madeni yanayofikia bilioni 23 na kushindwa kujiendesha.
Wakurugenzi wakuu wenye hisa nyingi katika kampuni ya Sky Associates Group ni Hussein Gonga na Faisal Shahbhati ambao kwa pamoja wamethibitisha kununua hisa zote za Tanzanite One baada ya kampuni hiyo kujitangaza katika mitandao yake ya kibiashara kuwa imeshindwa kujiendesha. Hisa zingine zimenunuliwa na raia wa India Rizwan Ullah.
Mbali ya madeni hayo kampuni hiyo inadai kushindwa kujiendesha kutokana na migogoro kati ya kampuni hiyo na wachimbaji wadogo ambao wamekuwa wakivamia migodi hiyo mara kwa mara na kukosa ulinzi madhubuti.
Kwa mujibu wa uchunguzi uliofanywa na gazeti hili ikiwemo kushuhudia baadhi ya nyaraka za Sky Associates Group, imethibitika kampuni hiyo ya wazawa imenunua hisa za tanzanite One na mali za kampuni hiyo kwa thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 32 fedha za kitanzania.
Hata hivyo kwa mujibu wa nyaraka hizo na kuthibitishwa na wakurugenzi hao, Sky Associates Group imechalipa bilioni 27 ikiwa ni pamoja na madeni na kumiliki mali za kampuni ya Tanzanite One na kubakiwa na deni la dola za Marekani Milioni 5.1 sawa na fedha za kitanzania shilingi bilioni 8.9
Habari kutoka ndani ya kampuni ya Tanzanite One zinasema kuwa madeni makubwa yanayoikabili kampuni hiyo ni pamoja na taasisi za Serikali na wabia wengine wa kampuni hiyo jambo lililofanya kukua na kufikia kiwango hicho cha shilingi bilioni 23.
Pia uchunguzi wa gazeti hili umebaini kuwa kampuni ya Sky Associates Group mbali ya kumilikiwa na wazawa kwa asilimia mia moja lakini imesajiliwa nchini Hong kong na wakurugenzi wa kampuni hiyo wamekuwa wakifanya biashara ya madini katika nchi mbalimbali duniani.
Mmoja wa wakurugenzi wa Sky Associates, Hussein Gonga alipotakiwa kuzungumzia ununuzi wa kampuni hiyo, alikiri yeye na mwenzake Faisal kununua hisa za Tanzanite One na hivyo kufanya wao kuwa wamiliki wabia na Serikali.
Ni kweli sisi wazawa kupitia kampuni ya Skye Associates Group tumeinunua Tanzanite One kwa kununua hisa zake baada ya kukabiliwa na mzigo mkubwa wa madeni na kushindwa kujiendesha kibiashara, hata hivyo taratibu zingine za ununuzi zikikamilika tutatoa taarifa rasmi, alisema Gonga
Kampuni ya Sky Associates Group mbali ya kufanya biashara ya madini pia imekuwa ikifanya utafiti, kutangaza madini yasiyotambulika na yamekuwa na soko zuri katika nchi mbalimbali za mabara ya Ulaya na Asia ambayo yanachimbwa sambamba na Tanzanite .
Miongoni mwa madini hayo ambayo yamekuwa yakitangazwa na kampuni hiyo ni pamoja na Pink tanzanite, Yellow tanzanite, Axinite, Grossular Garnet, Kyenite na Diopsite.
mwisho