Kampuni ya MYSOL ni matapeli, rudisheni pesa yangu

Kampuni ya MYSOL ni matapeli, rudisheni pesa yangu

nyapinyapileo

Member
Joined
Oct 19, 2022
Posts
92
Reaction score
215
Heri ya mwaka mpya wapendwa

Nilishawishika kukopa sola ya Watt 80 kutoka kampuni ya mysol ili wadogo zangu kijijini kwetu itilima wapate mwanga na kusoma vizuri. Cha ajabu hii kampuni ni majizi matupu, baada ya kulipia malipo ya awali Tsh.180,000, iliwachukuwa siku 17 kuja kunifungia sola hiyo nyumbani (walifunga tarehe 12 Disemba 2022).

Siku ya tarehe 13 Disemba sola yao ilizima na haijawaka mpaka leo tarehe 2 Januari 2023. Tangu ilipozima,nimekuwa nikiwapigia simu waje watengeneze ikiwa ni pamoja na kuwatumia Tsh 20,000 ya usafiri lakini hawajaja,huu si ni wizi na utapeli wa waziwazi.

Nyie majizi kampuni ya mysol mbwa kabisa nyie rudisheni pesa yangu ifikapo leo saa 6 mchana,zaidi ya hapo nitavunjavunja mavifaa yenu yote wezi na matapeli wakubwa nyinyi.
 
lipa deni mzee

uzi wako wa nyuma ni huu hapa ambao unakinzana na huu mpya


Na maswali ulikataa kujibu
 
Utavunjavunja nikajua utavunja chungu kumbe vifaa vyao hivyo sio vyao tena ni vyako wameshakuuzia.

Pole mkuu badala ya kuwatumia hio nauli ungewafuata ofisini kwa na kuwashtaki sio mitapeli imekuwa mingi. Usimuamini mtu kirahisi hivyo matangazo ya TV ni mbwembwe tu.
 
Jamaa wako vizuri, labda tu wanapatikana mbali na hapo itilima. Mimi nimemchukulia solar mzee wangu miaka mitano iliyopita na mama mkwe miaka mitatu iliyopita. Hawakuzingua, usiwe na hasira.
 
Kuna kampuni moja unakopa simu kisha unalipa kidogokidogo. Simu ya laki 280000 dukani unakuja kulipa 620000 kwa kidogo kidogo. Bado nakumbuka maneno ya mkenya "Tanzania ni shamba la bibi"
 
lipa deni mzee

uzi wako wa nyuma ni huu hapa ambao unakinzana na huu mpya


na maswali ulikataa kujibu
Baada ya malalamiko ya awali tulikaa tukafanya marekebisho upya ya Mkataba,cha kushangaza mambo ni yaleyale na UHUNI na UTAPELI ni mkubwa sana,leo wasirudishia Pesa yangu navunjavunja vifaa vyao hawa ni MATAPELI
 
lipa deni mzee

uzi wako wa nyuma ni huu hapa ambao unakinzana na huu mpya


na maswali ulikataa kujibu
Mega bight zangu kusoma andiko la huyu bwana mdogo kumbe ni muongo
 
Baada ya malalamiko ya awali tulikaa tukafanya marekebisho upya ya Mkataba,cha kushangaza mambo ni yaleyale na UHUNI na UTAPELI ni mkubwa sana,leo wasirudishia Pesa yangu navunjavunja vifaa vyao hawa ni MATAPELI
Ukivunja tuwekee picha hapa tuamini.
 
Mimi ni mteja wa Mysol na ninapata huduma kwa wakati kabisa, tena wana namba yao kupiga ni bure kabisa. Phone: 0800 75 5000

Je, ni kweli umefanya mawasiliano nao kwa namna yeyote ile? Nafahamu MYSOL wanatoa huduma kwa mteja bure kabisa kwa miaka minne. Huitajiki kulipia chochote. Hebu wasiliana na hii namba yako makao makuu na kumbuka kuwa na namba yako ya mtambo utasaidiwa.

Kama utaweza unaweza kuweka namba yako ya mtambo/malipo DM, na watawasiliana na wewe. Au namba yako ya simu.
 
Back
Top Bottom