mluhilaseko2020
Member
- Feb 22, 2021
- 55
- 151
Waungwana, nina kibanda changu hapa Babati kipo nje ya Mji kidogo ambako umeme wa TANESCO/REA bado haujafika.
Nilipoona matangazo ya Kampuni ya Sola ya Mysol yenye Makao Makuu Arusha kwenye Television nikaona nifanye mchakato wa kupata Sola Moja ya Mkopo.
Nikapiga simu na kupewa maelekezo yote niliyohitaji, nikalipia malipo ya awali ya Tsh. 285,000 kwa Mtambo wa Watt 200, baada ya siku 4 mafundi wao wakaja kunifungia tena kwa kuwalipia gharama za usafiri.
Cha kushangaza tangu wanifungie leo ni wiki ya nne Sola yao haiwaki, kila nikiwapigia simu wanasema wanakuja kurekebisha hawaji, mara waniambie watu wa Arusha ndio wataiwasha lakini kimya.
Nawashauri Watanzania wenzangu iepukeni na kuiogopa Kampuni hii ya Mysol kama mnavyouogopa Ugonjwa wa UKIMWI.
Nawasubiri waanze kufuatilia malipo yao ya mwezi niwaonyeshe kwa nini watoto huita maji MMA.