HKigwangalla
JF-Expert Member
- Feb 6, 2008
- 717
- 971
Ili kuweka rekodi sawa niseme tu hapa kwamba Mimi kwa sasa (tokea May 2010 nilipoenda kugombea Ubunge Nzega) sijihusishi na uendeshaji wa kila siku wa Kampuni ya MSK Solutions Ltd na hivyo sijui baadhi ya mambo yanavyoendelea.
Nimesoma upya hiyo article ya The Guardian na nimeuliza kwenye Menejimenti ya Kampuni ya MSK Solutions Ltd (ambayo mimi nina hisa) wamenihakikishia kampuni yetu haiko kwenye Orodha ya Makampuni ya Tanzania yaliyo kwenye 'Blacklist'; ila kilichopo karibu na makala hii ya The Guardian ni kama ifuatavyo: MS inadaiwa marobota ya pamba ambayo ilifanya 'short supply' na kwa kufanya hivyo walijikuta wamekiuka makubaliano ya kimkataba, na Mteja anapenda asaini Mkataba mwingine na MSK mwaka huu ili kiasi ambacho hakikuweza kuwa supplied mwaka Juzi akipate mwaka huu, na hilo halina tatizo, ni kitu cha kawaida na kina utaratibu wa kufuata kabla ya kufikia makubaliano. Mazungumzo yanaendelea. Hata hivyo mteja hakuwa amelipa fedha zozote na huwezi kusema alidhulumiwa ama vipi.
Labda nielezee kwa ufupi tu hapa mchakato unavyokuwaga. Ni kwamba kama kulikuwa na marobota 2000 kwenye mkataba na wewe uka-supply 1700 (kama ilivyokuwa kwa MSK Solutions), utalipwa pesa ya hayo 1700 uliyo-supply tu (kwa mtindo wa Letter of Credit ama hata ule wa Cash against Documents, yaani CAD). Hata hivyo mnunuzi atakudai lazima umalizie hayo 300 yaliyobaki kwa kuwa utakuta na yeye (kama akiwa ni international merchant) alipofunga mkataba na wewe alienda akafunga mkataba na mwingine (mill users) ambao nao wanajipanga kuuza bidhaa yao kwa kuwa wana uhakika wa marobota 3000 kutoka kwake. sasa uki-supply nusu unakuta umesababisha hii chain yote ipate matatizo, na kwa kuwa mikataba ya kimataifa inalindwa na mikataba na kanuni mbalimbali za biashara ya kimataifa kama vile ICA, ICC, Inco-terms unakuta unatakiwa ulipe fidia kwa mteja wako. Sasa huwa kuna arbitral bodies ku-determine haki ya pande mbili na hii hutoa award, ambayo kisheria huja kusajiliwa hapa high court nchini. Pande mbili zina nafasi ya kujadili nini kifanyike (nje ama ndani ya utaratibu wa mahakama) na hivi sasa ndicho kinachofanyika! Hii hutokea mara nyingi tu.
Blacklist ni orodha ya makampuni ambayo hayaruhusiwi kuuza pamba yao nje, na kampuni (muuza pamba kama MSK SOlutions) huingia humo baada ya award na baada ya determination ya high court ya nchi husika, imeendelea kugoma kulipa fidia hiyo ama kufanya makubaliano na kampuni ile nyingine (mteja).
ANGALIZO: Kuna watu wamekuwa kazini usiku na mchana kunitafutia kashfa ili kunimaliza kisiasa na kibiashara. Naomba niwatake waache mara moja ama watayasababishia gharama kubwa magazeti haya kwa vile yatashitakiwa na kudaiwa fidia ama na kampuni ya MSK Solutions Ltd ama na Wanasheria wangu, kwa niaba yangu. Tayari mchakato unaendelea kulishtaki gazeti la Sauti Huru na nimeamua kushauriana na Mwanasheria wangu kuhusu nini kifanyike kuhusiana na hili. Ndg zangu wanabodi, na wanahabari, kuweni makini na 'fair' kwa watu, makampuni na personality zao ili kulinda uhuru na haki ya kila mtu. Tusipende sana kutendewa haki wakati sisi hatautoi haki kwa wengine na wala hatutekelezi wajibu wetu. Mchakato wa kawaida wa utoaji haki ni lazima uendane na utekelezaji wa wajibu na majukumu yetu ipasavyo bila kuathiri wengine.
I am slowly getting fade up na siasa za nchi yetu kwa sababu ya mambo kama haya.
Ahsanteni,
HK.