Sudysoko
JF-Expert Member
- Aug 19, 2015
- 449
- 180
Kupitia jarida la uchumi na uwekezaji Investec la Africa Kusini limetaja kampuni ya Vodacom Tanzania kuwa kinara wa mauzo ya data kampuni hiyo imeongeza mapato ya mauzo ya data kwa kipindi cha miaka 5 kwa asilimia 22 ukilinganisha na asilimia 26 ya Safaricom ya Kenya.
Ongezeko hili limetokana na upanuzi wa miundombinu ya minara ya 3G na 4G huku ongezeko la watumiaji wa simu za smart ikifikia asilimia 41 huku kukiwepo na uboreshwaji wa huduma.
Kampuni ya Vodacom imeendelea kufanya uwekezaji mkubwa katika miundombinu ya minara ya 3G na 4G kwa kuongeza spidi mara mbili ya ilivyokuwa awali huku kampuni ya Tigo ikiendelea kuwa mshindani wa karibu katika kuongeza spidi ya Internet.
Katika kipindi hiki cha uuzaji wa hisa mapato yatokanayo na data yamechangia kuwa kiashiria kikubwa kwa kukuza na kutanuka kibiashara siku za usoni kwa kampuni hiyo ya mawasiliano.
Source
Investec Africa.