Kampuni ya kigeni ya Security Group inavyokwepa kodi Tanzania

Kampuni ya kigeni ya Security Group inavyokwepa kodi Tanzania

Warofo

Member
Joined
Mar 15, 2011
Posts
81
Reaction score
80


Kampuni ya kigeni ya Security Group inavyokwepa kodi Tanzania

Kampuni ya ulinzi ya kimataifa ya Security Group, ambayo inatoa huduma ya ulinzi kwa Umoja wa Mataifa (U.N.), mabalozi, mabenki na ofisi nyingine kubwa nchini Tanzania, inahusika na kashfa kubwa ya kukwepa kodi, utapeli, kuwakosesha ajira Watanzania na kuvunja sheria za nchi.

Kampuni hiyo inafanya utapeli mkubwa kwa kuajiri wafanyakazi wachache wake wenyewe na badala yake kuwavalisha sare (uniform za Security Group) wafanyakazi wa kampuni za ulinzi za Kitanzania ili kukwepa kodi na gharama za uendeshaji.

Security Group Tanzania ina wafanyakazi wa kwake wenyewe takriban 300 tu, lakini inatumia zaidi ya wafanyakazi 1,000 wa kampuni za ulinzi za Kitanzania kwa kuwavalisha sare zake na kuwaweka walinde ofisi za Umoja wa Mataifa na nyinginezo.

Kampuni hiyo ya Security Group inalipwa mabilioni ya shilingi kwa kutoa huduma kwa kuwachaji wateja wake kama kampuni ya kimataifa kumbe inatumia walinzi wa kampuni za Kitanzania wanaolipwa mishahara midogo wafanye kazi hizo.

Kuna mtandao wa raia wa Kenya ambao unatumika kufanikisha wizi huu mkubwa na unyonyaji wa wafanyakazi wa Tanzania.

Security Group Tanzania inaongozwa na Mkenya ambaye anashirikiana na kampuni ya ulinzi iliyosajiliwa Tanzania, Iron Side, lakini inayoongozwa na Mkenya ili kuhakikisha ukwepaji kodi huu.

Kampuni ya Iron Side ina wafanyakazi zaidi ya 700 ambao wanalipwa mshahara mdogo kama wafanyakazi wa kampuni ya kiTanzania. Hata hivyo, Security Group inawavalisha sare zake wafanyakazi hawa na kuwafanyikisha kazi kama wafanyakazi wa kampuni ya kimataifa ya ulinzi lakini inawapunja mshahara.

Kampuni hii ya Security Group pia inaitumia kampuni nyingine ya ulinzi ya Kitanzania, Insight Security, kufanya ukwepaji huu mkubwa wa kodi.

Kwa mujibu wa sheria za nchi, makampuni ya ulinzi ya kimataifa yanatakiwa yawalipe wafanyakazi wao mshahara wa juu kuliko makampuni ya ulinzi ya Kitanzania.

Wadau wa sekta ya ulinzi wanasema kuwa makampuni ya kimataifa ya ulinzi yanatakiwa yawalipe wafanyakazi wake kima cha chini cha mshara (net salary) cha shilingi 154,000.

Makampuni ya Kitanzania yanatakiwa kuwalipa wafanyakazi wake mshahara usiopungua 117,440.

Kampuni hii ya Security Group inawatapeli wateja wake wakubwa Tanzania, ikiwemo ofisi za Umoja wa Mataifa na mabenki, kuwa inawawekea walinzi waliopata mafunzo ya kimataifa kumbe inatumia wafanyakazi wa kampuni ndogo ambao hawajapata mafunzo ya kutosha na kuwavalisha sare zake ili kukwepa kodi.

Pia kampuni hii inawanyima haki ya ajira na mishahara Watanzania na kukwepa kodi za serikali.

Taarifa hizi zimetolewa na wafanyakazi wa kampuni hiyo ya Ulinzi (anonymous) ambao wamechoshwa na kunyonywa na kampuni hii ya kigeni ya Security Group inayowatumia kwa kuwavalisha sare za kampuni hiyo ili ipate tenda kubwa za ulinzi, lakini inawapunja mishahara na kukwepa kodi za serikali.
 
Tanzania kweli ni shamba la bibi. Wageni wanakuja na kujichumia mali hata kwa njia za wizi halafu serikali iko kimya. Tunaomba mawaziri wafuatao watoe majibu ya kashfa hii kubwa:

1. Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk. Emmanuel Nchimbi (Wizara yake ndiyo inasimamia usajili wa kampuni za ulinzi)
2. Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka (Wizara yake inasimamia masuala ya ajira)
3. Waziri wa Sheria, Mathias Chikawe (Wizara yake inasimamia sheria za Tanzania zisivunjwe)
 
Hii kampuni ya Security Group imekuwa ikipewa tenda kubwa kulinda mabenki ya kimataifa, kumbe ni wezi watupu. Serikali ichukue hatua haraka kuifuta isiendelee kuwanyonya Watanzania kwa kuwavalisha uniform za kampuni hiyo kumbe wala siyo wafanyakazi wa kampuni hiyo.
 
Hapo TRA inawabidi kufanya uchunguzi mara moja kabla ushahidi hauja potea,maana wakenya wanaosimamia maeneo mengi wana hujumu jitihada za serikali katika kujikusanyia mapato.
Watanzania kuweni wazalendo kwa kuisaidia serikali kufichua jitihada zinazo ikwamisha serkali kujipatia mapato halali.
 
Hapo TRA inawabidi kufanya uchunguzi mara moja kabla ushahidi hauja potea,maana wakenya wanaosimamia maeneo mengi wana hujumu jitihada za serikali katika kujikusanyia mapato.
Watanzania kuweni wazalendo kwa kuisaidia serikali kufichua jitihada zinazo ikwamisha serkali kujipatia mapato halali.

Ni kweli kabisa, kuna mtandao wa Wakenya hapa Tanzania wanashirikiana kuhujumu uchumi wa Tanzania, kupora hela na kunyanyasa wafanyakazi wa Tanzania.
 
Jaribuni kupima kama habari hii ni ya kweli au ni majungu kutoka kampuni pinzani ili kupunguza biashara/tenda za SECURITY GROUP kwa kuwa sasa majungu yameongezeka sana.
 
Dah! kama ni kweli basi Watanzania tumefeli.
Nalog off
 
Mkishafukuzwa kazi ndio hasira zenu mnazimalizia JF
 
Jaribuni kupima kama habari hii ni ya kweli au ni majungu kutoka kampuni pinzani ili kupunguza biashara/tenda za SECURITY GROUP kwa kuwa sasa majungu yameongezeka sana.

Hii habari ni ya kweli kabisa. Mimi nimewahi kufanya kampuni hiyo kwa miaka 12 na nimeacha mwaka juzi baada ya kuona utapeli mwingi kwenye kila idara. Nilikuwa idara ya ufundi(technical) na yapo mengi juu ya hiyo kampuni
 
Hii habari ni ya kweli kabisa. Mimi nimewahi kufanya kampuni hiyo kwa miaka 12 na nimeacha mwaka juzi baada ya kuona utapeli mwingi kwenye kila idara. Nilikuwa idara ya ufundi(technical) na yapo mengi juu ya hiyo kampuni
mkuu uliacha baada ya kuona huo utapeli au kwa kuwa ulipata kibarua kingine?
 
Huwa najiuliza haya makampuni ya nje ni nani huwa anawafundisha mbinu za kukwepa kodi zetu hapa nchini?maana hapo security group anatumia ujanja wa kutumia wafanyakazi walioajiriwa na kampuni ya kitanzania badala ya security group direct.i.e (kampuni ndani ya kampuni)
 
Jaribuni kupima kama habari hii ni ya kweli au ni majungu kutoka kampuni pinzani ili kupunguza biashara/tenda za SECURITY GROUP kwa kuwa sasa majungu yameongezeka sana.

Wewe ndio mvivu wa kushughulisha akili yako.Mwenzako kaja na haya wewe unasema majungu.Ya kwako ambayo si majungu yako wapi?
 
Kuna mwingine yuko g4s huyo mama anatumia mpaka k kwenye mambo haya
 
Nadhani ifike mahali kigezo cha Mkenya kufanya kazi Tanzania ni lazima awe na PhD. Hivi kwa nn CCM na taasisi zake wanawalea sana hawa Wakenya? Wana kipi cha ziada kuwashinda Watanzania?
 
Isije ikawa huyo mtoa taarifa kafukuzwa kazi kwa utovu wa nidhamu akaanza unafiki wake.

Lakini kama yanayosema ni kweli basi serikali yetu ni sikivu, kuanzia sasa Security Group waanze kukunja vilago vyao.
 
Mtoa mada naona umeingia kwa jazba sana.
Labda utusaidiw kuliko kubaki kulalamika kwamba wanakwepa kodi hapo ungefafanua tuelewe, pia ungefafanua kipengele cha sheria ambacho wamekivunja.

Kuna taarifa kwamba kampuni ya Security Group imekuwa tishio kwa makampuni makubwa, sasa hii mada yako isiwe sehemu ya kuanza majungu.

Tunaamini kampuni yoyote iliyosajiliwa kihalali lazima ilipe kodi.

Mtoa mada ungekuja na facts kwamba wanakwepaje kodi, utoe facts pia kuhusu basic pay and gross pay ya makampuni makubwa, then take home maana uliyotaja obviously ni ndogo kwa makampuni ya kimataifa.

Halafu uje na facts ya basic pay ya kampuni ndogo, gross pay then take home, ambayo pia hapo umedanganya
 
Hii habari ni ya kweli kabisa. Mimi nimewahi kufanya kampuni hiyo kwa miaka 12 na nimeacha mwaka juzi baada ya kuona utapeli mwingi kwenye kila idara. Nilikuwa idara ya ufundi(technical) na yapo mengi juu ya hiyo kampuni

Yamwage jamvini mkuu. Hapa ndo mahali pake
 
anacho sema mkuu ni sawa kabisa,wao wanatafuta tenda kisha kazi wanawapa kampuni ya iron sides ipo mikocheni,na uniform wanazotumia ni za security group,ila mishahara ndio yao inakuwa midogo ukilinganisha na wale walio ajiriwa moja kwa moja na security group.Na hata usaili wanafanyia makao makuu yao pale msasani ila mkataba ndio utakuonyesha kuwa haupo chini yao ila upo kwa bosi mwingine ambaye ni iron side.na hata mafunzo yao ni ya kama wiki mbili tu na mabosi wote ni wakenya.
'
 
Back
Top Bottom