Kampuni ya kigeni ya Security Group inavyokwepa kodi Tanzania

Kampuni ya kigeni ya Security Group inavyokwepa kodi Tanzania

Jaribuni kupima kama habari hii ni ya kweli au ni majungu kutoka kampuni pinzani ili kupunguza biashara/tenda za SECURITY GROUP kwa kuwa sasa majungu yameongezeka sana.
mkuu arushaone habari hii ni kweli kwa asilimia mia moja.jamaa zangu waliofanya kazi kwenye kampuni hii kwa muda mrefu.wamelazimishwa kysaini mkataba mpya au wakae nyumbani kwa kigezo cha kusubiria malindo.Na wakienda nyumbani ndio imetoka hiyo.Zile ni sare tu ila kiukweli sio wafanyakazi sahihi wa sgroup.huu ni wizi.
 
Haya makampuni ya ulinzi ya kimataifa yanafanya utapeli mkubwa sana nchini na kuwapunja wafanyakazi wa Tanzania. Nimeambiwa hata kampuni ya KK wanafanya mchezo huu. Wao wanaajiri wafanyakazi wachache sana, halafu wakipata tenda kubwa wanatumia wafanyakazi wa kampuni ndogo za ulinzi za Tanzania kama manamba kwa kuwavalisha sare zao.
 
tanzania kweli ni shamba la bibi. Wageni wanakuja na kujichumia mali hata kwa njia za wizi halafu serikali iko kimya. Tunaomba mawaziri wafuatao watoe majibu ya kashfa hii kubwa:

1. Waziri wa mambo ya ndani, dk. Emmanuel nchimbi (wizara yake ndiyo inasimamia usajili wa kampuni za ulinzi)
2. Waziri wa kazi na ajira, gaudensia kabaka (wizara yake inasimamia masuala ya ajira)
3. Waziri wa sheria, mathias chikawe (wizara yake inasimamia sheria za tanzania zisivunjwe)

shida iliyopo na hao "old dogs" uliowataja hapo juu. Hakuna lolote litakalofanyika wala hakuna atakaetoa ufafanuzi wa hili.
Kama unabisha utaona.
Kuhusu tra ndo kabisa uctegemee kwan sasa hv wanaangaika na deal yao ya vmashine vya rict.
Mungu tuhurumie na huu uongoz wa ccm
 
Huu uzi ni ukweli mtupu, hii kampuni ya Security Group inaitumia kampuni ya Ironsides Limited iliyopo Mikocheni kufanya wizi huu mkubwa. Ni Wakenya wawili wanaoshirikiana kufanya umafia huu.
 
Serikali itoe msimamo haraka kuhusu jambo hili, haiwezekani Tanzania ikaendelea kuwa shamba la bibi na wageni wakawa wanaiba tu kila kukicha.
 
mkuu arushaone habari hii ni kweli kwa asilimia mia moja.jamaa zangu waliofanya kazi kwenye kampuni hii kwa muda mrefu.wamelazimishwa kysaini mkataba mpya au wakae nyumbani kwa kigezo cha kusubiria malindo.Na wakienda nyumbani ndio imetoka hiyo.Zile ni sare tu ila kiukweli sio wafanyakazi sahihi wa sgroup.huu ni wizi.

Kwa kweli hapa lazima hatua kali zichukuliwe dhidi ya hawa many'angau wanaonyonya wafanyakazi wa Tanzania na kukwepa kodi za serikali.
 
anacho sema mkuu ni sawa kabisa,wao wanatafuta tenda kisha kazi wanawapa kampuni ya iron sides ipo mikocheni,na uniform wanazotumia ni za security group,ila mishahara ndio yao inakuwa midogo ukilinganisha na wale walio ajiriwa moja kwa moja na security group.Na hata usaili wanafanyia makao makuu yao pale msasani ila mkataba ndio utakuonyesha kuwa haupo chini yao ila upo kwa bosi mwingine ambaye ni iron side.na hata mafunzo yao ni ya kama wiki mbili tu na mabosi wote ni wakenya.
'

Serikali inashindwa nini kuchukua hatua hapa, au vigogo serikalini wanakula rushwa kwenye hili dili?
 
Kwa kweli hapa lazima hatua kali zichukuliwe dhidi ya hawa many'angau wanaonyonya wafanyakazi wa Tanzania na kukwepa kodi za serikali.
mkuu mimi nimefanya kazi ya ulinzi zaidi ya miaka sita kabla sijaacha hiyo kazi.na kwa taarifa kuna watu serikalini wanakula fungu la kumi.kwa hakika hatuna kimbilio mkuu
 
haya makampuni ya ulinzi yaani ni moja ya majanga ya taifa ukiachilia mbali mishahara midogo isiyo kizi mahitaji bado kuna unyanyasaji mkubwa kwa wafanyakazi wake
 
Shughuli za makampuni ya ulinzi zinatakiwa kuchunguzwa kwa umakini mkubwa na serikali, kwani hawa ni sawa na jeshi binafsi la polisi lenye silaha zake. Sasa kama wanaachiwa wafanye madudu waziwazi tu hivi ujue kuna mambo makubwa zaidi yanaendelea. Usalama wa nchi uko hatarini!
 


Kampuni ya kigeni ya Security Group inavyokwepa kodi Tanzania

Kampuni ya ulinzi ya kimataifa ya Security Group, ambayo inatoa huduma ya ulinzi kwa Umoja wa Mataifa (U.N.), mabalozi, mabenki na ofisi nyingine kubwa nchini Tanzania, inahusika na kashfa kubwa ya kukwepa kodi, utapeli, kuwakosesha ajira Watanzania na kuvunja sheria za nchi.

Kampuni hiyo inafanya utapeli mkubwa kwa kuajiri wafanyakazi wachache wake wenyewe na badala yake kuwavalisha sare (uniform za Security Group) wafanyakazi wa kampuni za ulinzi za Kitanzania ili kukwepa kodi na gharama za uendeshaji.

Security Group Tanzania ina wafanyakazi wa kwake wenyewe takriban 300 tu, lakini inatumia zaidi ya wafanyakazi 1,000 wa kampuni za ulinzi za Kitanzania kwa kuwavalisha sare zake na kuwaweka walinde ofisi za Umoja wa Mataifa na nyinginezo.

Kampuni hiyo ya Security Group inalipwa mabilioni ya shilingi kwa kutoa huduma kwa kuwachaji wateja wake kama kampuni ya kimataifa kumbe inatumia walinzi wa kampuni za Kitanzania wanaolipwa mishahara midogo wafanye kazi hizo.

Kuna mtandao wa raia wa Kenya ambao unatumika kufanikisha wizi huu mkubwa na unyonyaji wa wafanyakazi wa Tanzania.

Security Group Tanzania inaongozwa na Mkenya ambaye anashirikiana na kampuni ya ulinzi iliyosajiliwa Tanzania, Iron Side, lakini inayoongozwa na Mkenya ili kuhakikisha ukwepaji kodi huu.

Kampuni ya Iron Side ina wafanyakazi zaidi ya 700 ambao wanalipwa mshahara mdogo kama wafanyakazi wa kampuni ya kiTanzania. Hata hivyo, Security Group inawavalisha sare zake wafanyakazi hawa na kuwafanyikisha kazi kama wafanyakazi wa kampuni ya kimataifa ya ulinzi lakini inawapunja mshahara.

Kampuni hii ya Security Group pia inaitumia kampuni nyingine ya ulinzi ya Kitanzania, Insight Security, kufanya ukwepaji huu mkubwa wa kodi.

Kwa mujibu wa sheria za nchi, makampuni ya ulinzi ya kimataifa yanatakiwa yawalipe wafanyakazi wao mshahara wa juu kuliko makampuni ya ulinzi ya Kitanzania.

Wadau wa sekta ya ulinzi wanasema kuwa makampuni ya kimataifa ya ulinzi yanatakiwa yawalipe wafanyakazi wake kima cha chini cha mshara (net salary) cha shilingi 154,000.

Makampuni ya Kitanzania yanatakiwa kuwalipa wafanyakazi wake mshahara usiopungua 117,440.

Kampuni hii ya Security Group inawatapeli wateja wake wakubwa Tanzania, ikiwemo ofisi za Umoja wa Mataifa na mabenki, kuwa inawawekea walinzi waliopata mafunzo ya kimataifa kumbe inatumia wafanyakazi wa kampuni ndogo ambao hawajapata mafunzo ya kutosha na kuwavalisha sare zake ili kukwepa kodi.

Pia kampuni hii inawanyima haki ya ajira na mishahara Watanzania na kukwepa kodi za serikali.

Taarifa hizi zimetolewa na wafanyakazi wa kampuni hiyo ya Ulinzi (anonymous) ambao wamechoshwa na kunyonywa na kampuni hii ya kigeni ya Security Group inayowatumia kwa kuwavalisha sare za kampuni hiyo ili ipate tenda kubwa za ulinzi, lakini inawapunja mishahara na kukwepa kodi za serikali.

Haueleweki kbs
 
Mtoa mada naona umeingia kwa jazba sana.
Labda utusaidiw kuliko kubaki kulalamika kwamba wanakwepa kodi hapo ungefafanua tuelewe, pia ungefafanua kipengele cha sheria ambacho wamekivunja.

Kuna taarifa kwamba kampuni ya Security Group imekuwa tishio kwa makampuni makubwa, sasa hii mada yako isiwe sehemu ya kuanza majungu.

Tunaamini kampuni yoyote iliyosajiliwa kihalali lazima ilipe kodi.

Mtoa mada ungekuja na facts kwamba wanakwepaje kodi, utoe facts pia kuhusu basic pay and gross pay ya makampuni makubwa, then take home maana uliyotaja obviously ni ndogo kwa makampuni ya kimataifa.

Halafu uje na facts ya basic pay ya kampuni ndogo, gross pay then take home, ambayo pia hapo umedanganya

Mbona mtoa mada kaeleza vizuri tu jombaa? Unaposema tunaamini ka puni iliyosajiliwa kihalali lazima ilipe kodi ina maana huna habari kuhusu ukwepaji kodi uliokithiri wa makampuni ya kigeni nchini? Are you serious kwamba nchi hii makampuni yote ya kigen yanalipa kodi? Jamaa anakwepa kulipa kodi kwa kukodi wali zi wa makampuni mengine halafu anatoa taarifa kwamba ni wa kimataifa kumbe ndo wa pale Packers Kawe kwa training ya siku tatu. Labda haiko fresh kwa leo ila mtoa mada kakupa mishahara iliyopo huku kwenye field, siyo ya kwenye vitabu wizarani.
 
Back
Top Bottom