FRANCIS DA DON
JF-Expert Member
- Sep 4, 2013
- 36,066
- 40,725
Katika juhudi ya kukuza viwanda vya ndani vya magari, serikali ya nchini Ghana imeipa likizo ya kodi ya miaka 10 kampuni ya kutengeneza magari ya mtume Osafo Kantanka ijulikanayo kama KANTANKA MOTORS.
Hatua hii inalengo la kuiwezesha Ghana iweze kushindana na kampuni za magari toka Ulaya, Asia na Marekani, pia inafikiria kupiga tozo kubwa zaidi kwa magari toka nje ili kuvutia wanunuzi wa ndani.
Pia serikali imeweka mkakati wa kuacha kuagiza magari toka nje ya nchi na badala yake wameanza kunua magari yanayozalishwa ndani kwani imebainika ni imara, yana muonekano nadhifu na yanadumu kuliko yale ya Japana na Marekani, poa hatua hii inalengo la kupunguza tatizo la ajira nchini Ghana.
Mambo kama haya ni ya kuigwa na kupigiwa mfano, najiuliza tu, kama kweli serikali yetu inania ya kukuza viwanda vya ndani, inawezaje kuagiza mabuti na sare za jeshi toka China huku maelfu ya vijana waliosomea ushonaji wakiwa hawana ajira, hivi kweli huwa tunatumia kiungo gani cha mwili kufikiri? Msaada tafadhali; video inamaelezo ya ziada.
_________________________________