Kampuni ya Engineering/Land Surveying

Malikauli

Senior Member
Mar 3, 2012
147
113
Poleni na majukumu wapendwa.Mimi ni mwanafunzi kwa sasa nipo Sweden nafanya kadegree ka Engineering Survey,Ndoto yangu ni kwamba baada ya shule nirudi nyumbani na lengo ni kujiajiri.Natamani sana kuwa na kampuni ya Engineering and Land Survey ila ndo hivyo niliondoka 2008 nchini baada ya kumaliza form six,so sina detail za kutosha kuhusu yafuatayo,kama kuna mwenye ufahamu naomba anijuze pia kama kuna mwenye lengo la kufanya kazi na mimi katika hili tuwasiliane:

1.Demand ya surveying services iko vipi nchini kwa sasa?
2.Is it possible kwa graduate kumiliki kampuni au wanataka experience?Actually nimefanya field attachments za kutosha na kazi naijua sema sina vyeti vya previous employment as they could need, may be!

3.Ni vifaa gani basic kuanza navyo kulingana na nature ya kazi zilizopo ili nije navyo ninavyograduate october this year?...With my poor budget,nilikuwa najaribu kujibana hapa walau nipate total station moja na levelling machine moja.Tell me your ideas.

Naamini sote ni ndugu,maendeleo ya mmoja ni maendeleo ya wote.Tafadhari naomba msaada wa mawazo..Feel free kama unahisi we can work together,as two or three I do hope we can have more solid Company.



​
 
kama ukiventure na mageologist utakuwa umepanua wigo wako.

Watu binafsi wanalipa, ila mining companies na wachimbaji wadogo wadogo ni wateja wazuri.

Usisahau GPS, ni sawa na cha kupimia presha kwa daktari na kazi zake huwa za fasta fasta.
 
kama ukiventure na mageologist utakuwa umepanua wigo wako.

Watu binafsi wanalipa, ila mining companies na wachimbaji wadogo wadogo ni wateja wazuri.

Usisahau GPS, ni sawa na cha kupimia presha kwa daktari na kazi zake huwa za fasta fasta.


Asante kwa ushauri mkuuwazo lako linanipa mwanga zaidi.Hilo la GPS ngoja niangalie upepo unaendaje,I thought about it kabla ya hapo ila nikahisi kwa kianzio changu kidogo hiyo nipotezee kwa muda nitakuwa nakodi hoping kuna watu wanazo TZ,hapa naongelea Real Time GPS,ila kama ni hand held si shida though najua haitanisaidia sana kwenye acurrate jobs.Asante Kongosho
 
unaweza kunielewesha land survey inahusu na nini zaidi?
upimaji wa viwanja?
planning? ya makazi?
je kampuni binafsi bongo unaweza fanya hayo ya viwanja na makazi?
so wizara ya ardhi peke yake?
 
sasa kongosho, uko serious kweli kuhusu hand held gps as professional unaelewa accuracy yake unless if it is for recce only.
Malikauli, inabidi uongeze mtaji kwa hali ya sasa survey tanzania ina changamoto
Sana, vijana wengi wamejiajili na deferential GNSS ndo best sana wengi wana omnistar kwa sababu ni pocket friendly. kama vipi toa contacts au nipm tuone itakuwaje
 
mkuu

you need equipments like total station, GPS, Theodolite na vitu vingine vidogo vidogo, pia uwe na software za transformation ya data and mapping into reports

kazi zipo nyingi, everyday watu wanapima mashamba na viwanja vyao, serikali pia ina-outsource kazi za urban and rural planning kwa private companies, makampuni ya ujenzi wa infrastructures kama barabara, viwanja vya ndege mabwawa n.k yanahitaji surveying companies

cha kufanya; kufungua kampuni hapa taznania haina kikwazo hata kimoja, mimi siyo landa surveyor ila ni quantity surveyor(construction surveyor), unachotakiwa ni ukifika bongo ufanye registration ya land surveyors, i do hope wana professional body yao

if you need more info i can help to follow

all the best
 
unaweza kunielewesha land survey inahusu na nini zaidi?
upimaji wa viwanja?
planning? ya makazi?
je kampuni binafsi bongo unaweza fanya hayo ya viwanja na makazi?
so wizara ya ardhi peke yake?

Mkuu naomba nikujuze kuwa hata kampuni binafsi inafanya hii kazi,serikali imeanzisha mpango uitwao PRIVATE PUBLIC PARTNERSHIP(PPP). hivyo unaweza enda katika halmshauri ukaingia nao mktaba wa upimaji maeneo kwani serikali haina pesa kutosheleza mahitaji.
 
Kiongozi kumiliki kampuni sio tatizo hata kama ni Graduate cha msingi ni namna ya kuifanya kampuni iwe running na namna ya kupata kazi. Kama walivyosema baadhi ya wachangiaji, kwa sasa kazi za Surveying zipo ila ni namna tu ya kuzipata. Kuna baadhi ya makampuni makubwa 'yamehodhi' hizi kazi ila kwenye nia pana njia, ukipambana vya kutosha unazipata tu japo si lazima uanze na kazi kubwa - kubwa!

Kwenye suala la vifaa nakushauri usiumize sana kichwa kama huwezi kupata RTK GPS, nunua unachoweza njoo nacho (Though sidhani kwa sasa kama Theodolite zina ishu kwa kweli), kwa ulivyofikiria Total station na Level ni sawa tu kwa kuanzia. Kama unapata kazi kubwa unaweza kukodi tu baadhi ya vifaa.

LAT kwa TZ ni ngumu sana kwa Land Surveyors kujisajili kwenye hiyo bodi yao, kuna ukiritimba mkubwa sana na baadhi ya masharti ya kupata usajili hayatekelezeki kabisa, masavea wa zamani wameharibu kabisa utaratibu na matokeo yake vijana wengi wanaendesha maisha yao ya usavea bila kuwa members ila wanapitishia kazi zao kwa registered members kwa kuzisaini na mihuri tu, ni bahati mbaya sana hii bodi haitaki kwenda na wakati.

Muheshimiwa Boss, Land surveying ni zaidi ya upimaji viwanja. Ina kazi nyingine nyingi sana kwa jinsi nijuavyo mimi, upimaji wa chochote juu ya ardhi (Volumes za materials excavated, kuweka designs za barabara kwenye ardhi, kuonesha minerals zilipo exactly kwenye ardhi, kutengeneza ramani mbali mbali, kuset majengo na structures juu ya ardhi, kuset mifereji iweze kutiririsha maji vizuri, kuset njia za umeme na madaraja nk nk nk ni baaadhi ya kazi za Surveyors).

Kwahiyo ndugu yangu Malikauli, ishu hapa ni nia tu wala usikate tamaa
 
mie sio profession yangu per se but i did some courses on GIS and data base mgt which is not so different to this, kuwa mbunifu na jaribu kujishusha na kuchukua kazi kwa bei ndogo hadi upate jina. Mfano kina Mugerezi wanafanya hizi GIS work na wanalipwa na kucharge hela kubwa sana (InfoBridge)
Ukisajili kampuni yako waweza hata kutafuta kuajiriwa in case unahitaji hela au experience na jina kisha after two years ukaacha na kufanya kazi zako tu. GPS zipo mlimani city kuna kipindi pia mtu alikuwa anauza hapa Jf nunua software na vitu vingine ambavyo huku ni too expensive. Kila la heri usiache kumwomba Mungu pia
 
Poleni na majukumu wapendwa.Mimi ni mwanafunzi kwa sasa nipo Sweden nafanya kadegree ka Engineering Survey,Ndoto yangu ni kwamba baada ya shule nirudi nyumbani na lengo ni kujiajiri....​
Uendeshaji wa kampuni sio jambo rahisi. Kujiajiri ni wazo zuri na hasa kama una skills za kutosha za kijasiriamali. Hata hivyo mimi ningekushauri kama itakuwa rahisi uajiriwe kwanza (kwa angalau mwaka mmoja) ili usome mazingira ya fani yako hapa kwetu na kutengeneza network ambayo itakuja kukusaidia ukishaanzisha kampuni yako. Inawezekana unazo ndoto nyingi sana kuhusu fani yako lakini itakuwa vema kama ndoto hizo ukizipima kwanza katika mazingira halisi ya kitanzania.
 
Mapping(surveying), location -based data, GIS are future determinants of business and ecenomic dynamics.. ubunifu ndio muhimu... chagua tawi mojawapo ujikite..Surveying ni pana sana... registation ni ubababishaji tu... muhimu ni kuwa wateja na uzoefu wa kupiga kazi.... fani hivi sasa inalipa..
 
Kwa mtu anayeanza na mtaji wake mdogo sidhani kama anaweza nyimwa kazi sababu ana hand held GPS
Anyway, mie bado naona zinatumika na accuracy ni + or - few meters

Na acuracy yake ni nzuri asubuhi zaidi kuliko muda wa jua kali zaidi.


Ila kama anatakiwa kufanya survey kwenye sehemu ambayo ni more detailed kuna possibility ya errors, at the same time kazi za aina hii hupewa kampuni zilizojizatiti kidogo, for a new comer?! sidhani kama wanapata.

Na nikiangalia katoka mtizamo wa kibiashara, lazima uanze mdogo mdogo kuendana na soko lako, kadiri unavyokua kibiashara utakuwa una-invest more katika technology.

Ila kama anaweza kuwa na GPS ya kisasa zaidi ni bora zaidi, but with budget constrain, ni bora nikanunua hand held GPS, Vifaa vingine vya muhimu kwenye land survery, laptop, supporting softwares.

sasa kongosho, uko serious kweli kuhusu hand held gps as professional unaelewa accuracy yake unless if it is for recce only.
Malikauli, inabidi uongeze mtaji kwa hali ya sasa survey tanzania ina changamoto
Sana, vijana wengi wamejiajili na deferential GNSS ndo best sana wengi wana omnistar kwa sababu ni pocket friendly. kama vipi toa contacts au nipm tuone itakuwaje
 
Vipi hali mkuu Malikauli?
Vipi mpango wako ulifanikiwa?
Hapana mkuu, nilirudi nchini nikawa kwenye harakati za kulianzisha nikapata mchongo mwingine kwenda nje ya nchi tena na sioni kama bado nina ndoto hiyo maana sijajua nchini narudi lini. Nilikuwa nimekuja na baadhi ya vifaa basic vimekaa tu home kwa sasa naviuza, siku nikirudi nitaangalia utaratibu mwingine. Check attachment ukiweza kunilink kwa wateja....bei ya KiCovid covid kabisa 😀. Kuna namba hapo juu kwenye document I can be contacted on Whatsapp.
 

Attachments

  • SURVEY EQUIPMENT FOR SALE.pdf
    173.8 KB · Views: 23
Hapana mkuu, nilirudi nchini nikawa kwenye harakati za kulianzisha nikapata mchongo mwingine kwenda nje ya nchi tena na sioni kama bado nina ndoto hiyo maana sijajua nchini narudi lini. Nilikuwa nimekuja na baadhi ya vifaa basic vimekaa tu home kwa sasa naviuza, siku nikirudi nitaangalia utaratibu mwingine. Check attachment ukiweza kunilink kwa wateja....bei ya KiCovid covid kabisa . Kuna namba hapo juu kwenye document I can be contacted on Whatsapp.
Poapoa mkuu Malikauli ngoja tuangalie kama tunaweza pata mtu wa kununua hizi.

Na huu uzi ulifanya tupate mengi kutoka kwa wachangiaji hasa kwa mazingira yetu ya kitanzania.

SUKAH
 
Back
Top Bottom