Lizaboni
JF-Expert Member
- Feb 21, 2013
- 33,894
- 20,375
Wadau, amani iwe kwenu.
Nikiwa katika safari zangu Jijini Dar es Salaam nilikofika kwa shughuli za kibiashara, nimepita maeneo ya Leaders Club na kukuta makontena ya kampuni ya DSTV pamoja na wafanyakazi wa kampuni hiyo wakiwa wametapakaa kila kona. Nimebahatika kuongea na mmoja wa wafanyakazi wa kampuni hiyo na kunithibitishia kuwa kampuni hiyo imefukuzwa kwenye jengo walilopanga Barabara ya Ali Hassan Mwinyi, jirani na Kanisa la St Peters baada ya kushindwa kulipa pango.
Nimejiuliza sana. Inakuwaje kampuni kubwa kama DSTV ishindwe kumiliki mjengo wake wenyewe? Au wapo mguu ndani mguu nje? Nashindwa pia kuelewa sababu za wao kushindwa kulipa pango la nyumba ilhali ina wateja kila kona ya nchi hii.