Kampuni ya mabasi ya Dar Express inawalaghai abiria wanaotoka Rombo na Arusha kuelekea Dar kwamba basi litapitia barabara ya Chalinze lakini wakifika Msata wanawapitisha Bagamoyo hata kama huyo abiria anashukia Mlandizi na ana mizigo mingi. Malalamiko ya abiria tumeyasikia sana ila leo tumeshuhudia abiria waliopanda basi lenye namba za usajili T 155 DBU kupitia Bagamoyo ilhali wanashukia Kibaha, Mbezi, Kimara, Kibo n.k. Tulihakikishiwa kuwa gari Litapitia route ya Chalinze. Sasa tunajiuliza, ushindani mkubwa mnaokabiliwa nao kutoka kwa makampuni shindani umewafanya 'mtapeli' abiria? Kinachosikitisha ni kwamba mmiliki wa kampuni alishuhudia tukirubuniwa kwamba Gari itapitia Chalinze ingawaje yeye alishukia Same. Je kwa mtindo huu mnaitakia mema kampuni yenu? Naomba kama kuna waliopitia madhila kama haya kwenye hii kampuni wanishauri kuhusu huu usumbufu na gharama za ziada ambazo nimesababishiwa na utapeli wa hii kampuni. Abiria 15 wamekumbwa na huu utapeli wa basi namba T155 DBU leo tarehe 22/04/2018.