Kampuni 8 za China zapigwa marufuku nchini Marekani

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
3,377
2,000
Rais wa Marekani Donald Trump amesaini amri ya Rais ya kupiga marufuku kampuni nane za China zenye program ya kutoa huduma ya ulipiaji wa bidhaa kwa njia ya mtandao.

Programu hizo ni pamoja na ile maarufu ya mtandao wa Alipay inayomilikuwa na mfanyabiashara tajiri China Jack Ma, QQ Wallet na WeChat pay.

Amri hiyo inaanza kutekelezwa ndani ya siku 45 baada yar ais kusema kuwa programu hizo zinapigwa marufuku kwasababu ni tishio kwa usalama wa taifa la Marekani.

Inasemekana kuwa kuna uwezekano program hizo zinatumika kufuatilia na kupata data za raia wa Marekani.

Programu zingine zilizopigwa marufuku ni pamoja na Tencent QQ, CamScanner, SHAREit, VMate na WPS Office.

"Marekani lazima ichukue hatua madhubuti dhidi ya waliotengeneza na kudhibiti programu za China kulinda usalama wa taifa letu," Amri hiyo ya rais imesema.

Aidha, amri hiyo ya Rais Trump inasema "kwa kufikia bidhaa za elektroniki za simu aina ya smartphones, tablets, na kompyuta, programu za China zinaweza kufikia taarifa muhimu za watumiaji ikiwemo taarifa nyeti za utambulisho na taarifa za kibinafsi."

Utawala wa Trump umeongeza shinikizo kwa makampuni ya China mwezi wake wa mwisho madarakani ikiwemo kampuni anazozichukulia kuwa zenye kuhatarisha usalama wa taifa hilo.

Rais Trump amesaini amri kadhaa za rais dhidi ya kampuni za China kwa madai kwamba huenda zikashirikisha data za raia wa Marekani kwa serikali ya China.

Media captionAmbar, an influencer, say she has seen inappropriate content on TikTok

Chinese social media app TikTok and telecoms giant Huawei have been among the casualties of Washington's crackdown.

Mwezi uliopita, Wizara ya biashara iliongeza kampuni kadhaa za China ikiwemo ya kutengeneza chipu ya SMIC na ndege zisizo na rubani ya DJI Technology kwenye orodha ya zilizopigwa marufuku kufanya biashara.

Utawala wa Trump pia uliweka masharti kwa makapuni ya China na Urusi kwa madai ya kushirikiana kijeshi na kununua bidhaa nyeti pamoja na teknolojia za Marekani.

China imekanusha mara kadhaa madai kuwa kampuni za nchi yake zinaishirikisha data walizonazo za raia wa Marekani na imejibu madai hayo kwa kuweka masharti makali kwa kampuni za China zinazofanya manunuzi nje ya nchi hiyo kwa kupiga marufuku ununuaji wa teknolojia ya kijeshi.

Agosti mwaka jana, Marekani iliagiza kampuni ya ByteDance, inayomiliki mtandao wa kijamii wa programu ya TikTok, ama ifunge mtandao huo au iuze mali zake zilizopo Marekani.

Licha ya kushindwa kutekeleza mauzo yake kwa siku ya mwisho iliyokuwa imewekwa, Marekani bado haijafunga programu hiyo na inaendeleza mazungumzo ya utendani kazi wa kumpuni hiyo siku za baadaye.
 

SirChief

JF-Expert Member
Jun 23, 2014
3,013
2,000
Huyu jamaa ni binaadamu ambae anaongoza duniani kwa rohombaya ya kishetani, watu kama hawa ni hatari sana
Subiri sasa mashetani halisi yanaingia ikulu 20th January, Na mbaya zaidi yamekatama chambers zote za uwakilishi na executive. Hapo indio akili zitawakaa sawa.
 

STRUGGLE MAN

JF-Expert Member
May 31, 2018
5,319
2,000
Subiri sasa mashetani halisi yanaingia ikulu 20th January, Na mbaya zaidi yamekatama chambers zote za uwakilishi na executive. Hapo indio akili zitawakaa sawa.
Hatukatai kila raisi wa Marekani ana mabaya yake ila huyu ni miongoni mwa Raisi mwenye chuki za waziwazi sio tu kwa nje ya Marekani bali pia hata wamarekani wenyewe kawgawa, ni Raisi ambae ubaguzi wa miaka 60 70 nk waliokua wakifanyiwa wamarekani weusi aliuleta nyakati hizi za kidigitali, ana mambo ya ajabu sana kama mgonjwa wa akili
 

BUSH BIN LADEN

JF-Expert Member
Mar 16, 2019
3,527
2,000
Huwezi kuendelea kuwa wa kwanza kwa kumfanyia fitna anaeshika namba mbili.. China ni unstopable kwa sasa
 

Dalmine

JF-Expert Member
Sep 8, 2016
4,849
2,000
Huyu jamaa ni binadamu ambae anaongoza duniani kwa rohombaya ya kishetani, watu kama hawa ni hatari sana.

Bado sijaona wa kumfikia bill clinton,,jamaa alikua hapendi vita.

Bushi ❌
Obama ❌
Trump ❌
Huyu mwingine hatujui.

Ndio maana cnaga time kuwafatilia wendawazimu kama hawa wanaowachukia waarabu/waislamu. Damu za waislamu zinamwagika skwa ajili yao mashetani wakubwa.
 

tochi 28

JF-Expert Member
Oct 5, 2019
266
500
bora trump baiden hafai kabisa...kwa sababu anasiasa za Africa kuja kueneza ushoga kama obama .na pia biden atakuja na mikataba ya ajabu soon Tanzania ,bora Trump alikuwa anapinga ugaidi kwa waharabu.
 

Mpinzire

JF-Expert Member
Jan 18, 2013
2,419
2,000
Wazungu wameshtukia hawawapendi kinoma,wapumbavu wengine wadosi wakikaa sehemu wakiwa wengi wanaanza ubaguzi
Wameshtuka kuwa huyu jamaa akiachwa anawapita pakubwa tu..!! USA akiona taifa linakuwa imara hapendi
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom