kifupi kirefu
JF-Expert Member
- Oct 29, 2018
- 539
- 3,507
Kuna Vita kubwa ndani ya chama cha Mapinduzi kuhusu uchaguzi wa 2025, Vita hii imekuwa kali ikamfanya Mhe. Rais kutangaza nia mapema. Baada ya kutangaza nia mapambano yamekuwa makali kwenye majimbo na kata kundi la utawala uliopo likitaka kuwaondoa waliowekwa na utawala uliopita.
Huko Mbeya/ Songwe tumesikia mapambano ya Mbunge na Kiongozi wa chama, huko Arusha hali ni mbaya, ukienda Kanda ya ziwa napo panafukuta macho. Kundi lililopewa madaraka nje ya uchaguzi halali lipo hatarini kupukutika kwa mbinu mbalimbali ili wale wanaoamini wanakubalika na wapiga kura wapewe nafasi.
Najiuliza, tulisema hakuna siasa baada ya uchaguzi tukasema upinzani unachelewesha maendeleo. Leo hii upinzani ndio wanaopiga kampeni au sisi wenye madaraka ndio tunaoangaika na madaraka ya miaka mitano mbele? Kama tunawaza 2025, leo ni 2021 tunaamini tutawatumikia wananchi au tutawatumikia wenye dhamana yakututeua tugombee 2025?