Kampeni za ccm kibangu na changa la macho

Mzee wa Gumzo

Senior Member
Apr 21, 2008
197
5
Siku zote ninaamini katika ukweli kwa kuwa daima humweka mtu huru hata kama unauma
Wakati Bw.Charles Keenja anaomba kura za wanaubungo wa kibangu na makoka aliweka bayana kuwa yeye na CCM wanaelewa tatizo la barabara inayowaunganisha wakaazi wa Kibangu na Makoka na maeneo mengine ya mkoa wa Dar es Salaam.

Kwa wasiofahamu eneo hili, ili ufike kibangu na makoka leo kwa gari lazima ujilize sana.Barabara inayopitika ni nyembamba, yenye mawe mengi na inakuhitaji kuzunguka kwa muda mrefu.Kwa ujumla kufika huko ni afadhali pikipiki ikupeleke au uende kwa miguu.

Njia iliyokuwa inaunganisha eneo hilo na maeneo mengine ni kama haipo kwa miaka zaidi ya minne sasa.Njia hiyo ilikuwa inaanzia karibu na daraja la ubungo karibu na landmark hotel lakini eneo linalopakana na mto huo likaporomoka na kumega eneo la barabara na nyumba.Hivi sasa watu wanapita kwa miguu tu eneo hilo ili kufika makwao.

CCM iliahidi kuwa ingewapa maisha bora wakazi wa eneo hili tangu mwaka 2005 lakini hakikufanyika chochote.Kinachoshangaza ni jitihada zilizoanza wiki iliyopita za kumwaga kifusi kwenye njia hiyo isiyotoka.Vifusi vimemwagwa kuanzia pale barabara ilipoporomoka na vinaendelea kumwagwa sijui mpaka wapi.Hata baada ya kumwaga vifusi hakuna kinachoendelea.Vimebakia vichuguu njia nzima.

Maswali magumu ni haya kuhusu jitihada hizi
1. Wanaoleta vifusi walikuwa wapi siku zote?
2. Kwanini walete vifusi 2009 kuelekea 2010 na siyo kabla?
3. Hivi kifusi cha udongo wa mfinyanzi (topetope) kitaimarisha barabara au kuleta maafa?
4. Unapoleta kifusi ukamwaga mafungumafungu njia nzima halafu ukaondoka bila
kufanya chochote hivyo kuziba njia hata ya wale wenye mikweche yao au kutumia
pikipiki inaashiria nini?

KIla mwenye macho anaona na kubaki kushangaa.Kuna wanaosema hizi ni kampeni za CCM kwa 2010.Yawezekana sikatai lakini pengine ni changa la macho vilevile.

Kibangu hawahitaji vichuguu njiani.Wanahitaji barabara safi.Kwanza lazima waelezwe ahadi ya kuifungua barabara hiyo kwa kuwalipa wenye nyumba eneo la riverside kusudi nyumba zao zibomolowe na kupisha njia imeishia wapi.Wahisika walishajiandaa kuhamishwa lakini kutokana na longolongo za serikali wakabadili mwelekeo.Leo hii unajaza kifusi njia isiyoelekea kokote?Huu ni uhuni ati
 
Back
Top Bottom