Kampeni ya "NO ELECTION" ni sasa

Kampeni ya "NO ELECTION" ni sasa

Kalamu

Platinum Member
Joined
Nov 26, 2006
Posts
19,496
Reaction score
26,122
Ni wazi kwamba polisi tayari wamekwisha anza harakati za kuzuia kampeni hiyo; wakidhani kuwadhibiti viongozi wa CHADEMA kila mahali watafanikiwa kuwafanya waTanzania wasisusie uchafuzi huo unaofanyika Oktoba.
Kuwadhibiti viongozi wa CHADEMA hakuzuii tena kuenea kwa kampeni hiyo miongoni mwa wananchi.

Kampeni ya "NO ELECTION", CHADEMA walikwisha maliza wajibu wao siku nyingi, na waTanzania waliwaelewa lengo lililo kusudiwa; la wananchi kutokwenda kuhalalisha kilicho haramu.

Kampeni hiyo sasa ipo mitaani kwa wananchi, kueleweshana ni njia zipi zitatumika kutojihusisha na uchafuzi huo. Haihitaji tena viongozi wa CHADEMA kwenda majukwaani na kueleza wananchi watasusia vipi uchafuzi huo.

Kampeni sasa inatembea mtu kwa mtu, ndani ya vyombo vya usafiri, vilabuni na kila mahali waTanzania wanapokutana wawili au zaidi. Polisi hawawezi kuzuia chochote katika mpangilio huo.

Polisi wakitaka kuizuia kampeni hiyo itawalazimu wakawakamate wananchi huko kwenye mitaa yao.
 
Mpk kufika 29 October kitakuwa kimeeleweka.
Hii ndiyo kazi muhimu ya kila mTanzania; kuhakikisha kwamba taifa letu haligeuzwi kuwa himaya ya GENGE lisilokuwa na uchungu wowote na taifa hili.
Ni fursa nzuri kwa kila mmoja wetu kutoa mchango wake stahiki kwa nchi yetu bila kuwepo na ulazima wa kumwagwa damu ya waTanzania.

Tukisubiri Samia ajitangazie ushindi kwa kutumia nyomi feki; damu ya waTanzania itaendelea kumwagika, huku matokeo yake yakiwa hayaonekani.

Ni fursa ya kipekee sana; tusiache ipite hivi hivi.
 
Ni wazi kwamba polisi tayari wamekwisha anza harakati za kuzuia kampeni hiyo; wakidhani kuwadhibiti viongozi wa CHADEMA kila mahali watafanikiwa kuwafanya waTanzania wasisusie uchafuzi huo unaofanyika Oktoba.
Kuwadhibiti viongozi wa CHADEMA hakuzuii tena kuenea kwa kampeni hiyo miongoni mwa wananchi.

Kampeni ya "NO ELECTION", CHADEMA walikwisha maliza wajibu wao siku nyingi, na waTanzania waliwaelewa lengo lililo kusudiwa; la wananchi kutokwenda kuhalalisha kilicho haramu.

Kampeni hiyo sasa ipo mitaani kwa wananchi, kueleweshana ni njia zipi zitatumika kutojihusisha na uchafuzi huo. Haihitaji tena viongozi wa CHADEMA kwenda majukwaani na kueleza wananchi watasusia vipi uchafuzi huo.

Kampeni sasa inatembea mtu kwa mtu, ndani ya vyombo vya usafiri, vilabuni na kila mahali waTanzania wanapokutana wawili au zaidi. Polisi hawawezi kuzuia chochote katika mpangilio huo.

Polisi wakitaka kuizuia kampeni hiyo itawalazimu wakawakamate wananchi huko kwenye mitaa yao.
Kampeni hiyo sasa ipo mitaani kwa wananchi, kueleweshana ni njia zipi zitatumika kutojihusisha na uchafuzi huo. Haihitaji tena viongozi wa CHADEMA kwenda majukwaani na kueleza wananchi watasusia vipi uchafuzi huo.
 
FB_IMG_1757160741569.jpg
 
Back
Top Bottom