Kampeni ya kura 50 kila mfanyakazi tz | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kampeni ya kura 50 kila mfanyakazi tz

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Sir R, May 29, 2010.

 1. Sir R

  Sir R JF-Expert Member

  #1
  May 29, 2010
  Joined: Oct 23, 2009
  Messages: 2,177
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  Rais JK alipokuwa anawahutubia wazee wa Dar es salaam (CCM) alisema wazi kuwa hajali kura za wafanyakazi yaani yuko tayari kukosa kura 350000 za wafanyakazi. Ni kauli iliyojaa kiburi, ubabe na kejeli

  Nilishangazwa sana na ujasiri wa JK kwani najua atakuwa mgombea wa urais october mwaka huu, nilifikiri angechagua maneno ya kusema wakati huu tunapoelekea october.

  Nimeamua kuwahamasisha wafanyakazi wenzangu kumnyima JK na CCM kura mwaka huu. Vile vile nimeona hiyo haitoshi, kila mfanyakazi ajitahidi kutafuta si chini ya watu 50 watakaomnyima JK na CCM kura kwa kumpa mgombea wa upinzani, tujifunze kwa waingereza, Godon Brown alimkejeli Bi kizee mmoja na watu wakamfundisha nidhamu.

  Kila atakayesoma ujumbe huu amtumie mwenzake hasa mfanyakazi,

  Ewe mfanyakazi popote ulipo hamasisha watu kushiriki uchaguzi mwaka huu na wasiwape wagombea wa CCM na JK wao kwani kauli yake ni matusi kwa wafanyakazi na watanzania kwa ujumla.

  Wafanyakazi tushiriki katika KAMPENI YA KURA 50+ tutabadilisha historia ya nchi.

  Nakaribisha michango itakayoleta mabadiliko.

  NAKUPENDA EWE TANZANIA
   
 2. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #2
  May 29, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,196
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Hawahitaji kura hawa, ona wanavyoshinda!


  GADO
  [​IMG]
   
 3. S

  Subira Senior Member

  #3
  May 30, 2010
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 162
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  mfano halisi ni huko arusha 2005 yule mrema alianguka vibaya, maana hatakiwi hata, lakini yule mwanasheria wa manispaa akawapigia hao wakuu wao kuwaambia jimbo limeondoka ndugu, yangu ,akaamriwa kutangaza mrema mshindi, wacha bwana hawaitaji kura za mtu wadhuluma tu hawa
   
 4. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #4
  May 30, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Kura 50 mbona nyingi sana nne au tano tu zinatosha kwa kila mfanyakazi na ni rahisi kupatikana mimi tayari nimeshapata nne bado natafuta ya tano.
   
 5. P

  Paul S.S Verified User

  #5
  May 30, 2010
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 5,933
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Angalau zinaweza kusaidia tuka pata wabunge wengi wa upinzani bungeni, ila kumngoa mkwere wala haitaji kura vyombo vyote vinavyoratibu amevikumbatia yeye.dhulma tu
   
 6. Sir R

  Sir R JF-Expert Member

  #6
  May 30, 2010
  Joined: Oct 23, 2009
  Messages: 2,177
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  Najua watawala wana mbinu nyingi za kupata kushinda uchaguzi , kumtangaza mgombea wa chama tawala ni mojawapo. Pamoja na hayo yote siyo muda wa kukata tamaa zaidi tuelimishane namna ya kuziba njia zao mbaya ya kuvuruga uchaguzi.

  Wasiwasi wangu ni kwamba watu wengi waichagua CCM kwa kura halali kwa kutokujua kuwa ni chama haramu, kimejenga propaganda chafu katika vichwa vya watanzania.

  Tuwanyime kura wagombea wa chama tawala.

  Tusiamini kuwa kila uchaguzi na kkila mahali CCM huiba kura, kuna maeneo mengi wanapigiwa kura na wananchi kwa imani kuwa kitabadilika kitu ambacho ni kigumu kwa CCM.
   
 7. Sir R

  Sir R JF-Expert Member

  #7
  May 30, 2010
  Joined: Oct 23, 2009
  Messages: 2,177
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  Hongera mkuu kwa hatua uliyochukua, naomba uendelee na kazi njema uliyoanza ya kuhamasisha jamii kuharakisha mabadiliko yanayohitajika katika taifa la Tanzania.

  Tutafika
   
 8. Johnsecond

  Johnsecond JF-Expert Member

  #8
  May 30, 2010
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 1,077
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Cha msingi aibe tu lakini akijua kuwa amedondoka hakuna anayempenda. Unajua hilo pekee litakuwa pigo tuendelee mimi nilishatangaza toka muda sana kuwa nina kura 7 nyumbani kwangu na za majirani jumla ni zaidi ya kumi tayari. Mimi nataka tuone nyie msiwe na hofu maana watakaohesabu kura hizo ni wafanyakazi. atakula kiburi chake.
   
 9. Sir R

  Sir R JF-Expert Member

  #9
  May 30, 2010
  Joined: Oct 23, 2009
  Messages: 2,177
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  Bravo mkuu, mimi nyumbani nina kura 4, mtaani nishafikisha zaidi ya watu 15 ambao wamebadilisha msimamo wa kuhusu JK na CCM yaani hawatampa kura, najitahidi ndani ya mwezi june nipate watu at least 20 jumla itakuwa 39.

  Tuharakishe mabadilikko yanayohitaji
   
 10. Mgeninani

  Mgeninani Senior Member

  #10
  May 30, 2010
  Joined: Jan 3, 2010
  Messages: 190
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Suluhu ni tume huru ya uchaguzi, msajiri huru wa vyama vya siasa, lengo kuu la CCM ni kushika dola kama ilivyo kwa chama chochote cha siasa, kama vitu hivi visipodaiwa basi ni mlolongo wa michezo ya kuigiza utaendelea.
   
 11. Mahesabu

  Mahesabu JF-Expert Member

  #11
  May 30, 2010
  Joined: Jan 27, 2008
  Messages: 5,043
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  JAMANI TUELEKEAPO NI KUBAY......TUKAE TUJADILI TUFIKIE MUAFAKA..........pieces of papers can not remove anybody from power.....TUMEAMBIWA UKWELI....NA UKWELI UNAUMA....TUMUOMBE BASI ANGALAU ATUONGEZEEE ZIKARIBIE ZILE TULIZOKUWA TWAHITAJI NA SI MAWAZO TULIYONAYO SASA......!
   
Loading...