Kampeni ya kumng’oa Trump yashika kasi

Kampeni ya kumng’oa Trump yashika kasi

comrade igwe

JF-Expert Member
Joined
Jan 12, 2015
Posts
7,295
Reaction score
3,952

Ndoto za Donald Trump aliyechaguliwa hivi karibuni kuwa Rais wa 45 wa Marekani huenda zikayeyuka baada ya wajumbe sita wa Democratic watakaopiga kura za majimbo kuanzisha kampeni maalumu ya kuwashawishi wajumbe wengine kutomwidhinisha Rais huyo mteule.

Wajumbe hao ambao majina yao yalitangazwa jana wanaamini kuwa iwapo watafanikiwa kuwashawishi wenzao wengine 37 kutoka Chama cha Republican basi watakuwa wamefanikiwa kumzuia bilionea huyo kuingia ikulu.

Desemba 19 wajumbe 538 kutoka majimboni watakutana kupiga kura ya kisheria kumthibitisha Rais mteule anayetarajiwa kuapishwa Januari 20. Kura hizo zitahesabiwa mbele ya Bunge la Congress Januari 6.

Hatua ya wajumbe hao wa Democratic kuanzisha kampeni hiyo imekuja siku chache baada ya makundi ya kiharakati kuanza kukusanya saini nchi nzima ili kuwashinikiza wajumbe hao kutompitisha rais huyo ambaye tayari ameanza kutangaza vipaumbe vyake.

Mmoja wa wajumbe hao aliyetambulika kwa jina la Michael Baca anayewakilisha Colorado amekuwa akizunguka huku na kule kuwashawishi wajumbe wenzake kuepuka kumuunga mkono Trump wakati wa upigaji wa kura.

Mjumbe mwingine ambaye hakupenda jina lake kutajwa alisema kutokana na mvutano unaoendelea kujitokeza sasa kunaweza kuzusha hoja zitakazolazimisha kuangaliwa upya kwa mfumo unaotumika sasa kupitia kura za majimbo kumchagua rais.

Ingawa bado haijajulikana ni wajumbe wangapi wanaendelea kuwa waaminifu kwa kambi ya Trump lakini mchambuzi wa masuala ya siasa, Profesa George Edwards III amesema kama kutatokea wajumbe nane au 10 wakaamua kutomuunga mkono rais huyo mtarajiwa basi kunaweza kubadilisha ndoto za kiongozi huyo kuingia ikulu Januari 20 mwakani.

Tayari wafuasi hao wameitisha kampeni ya kuomba Wamarekani kuwaunga mkono mtandaoni kupitia tovuti ya www.change.org wa kuwashawishi wachaguaji hao kumchagua Clinton badala ya kumthibitisha Trump kwa kuwa hafai kuwa rais wa taifa hilo.

Ujumbe huo unaeleza kuwa iwapo watachagua kama ambavyo majimbo yamepiga kura katika uchaguzi huu, Trump atashinda.

“Hata hivyo, wanaweza kumpigia Hillary Clinton wakiamua,” inasomeka sehemu ya kampeni hiyo yenye kichwa cha habari; “Kura ya uamuzi: Mfanye Hillary Clinton kuwa rais Desemba 19”.

“Hata katika majimbo ambayo wajumbe hawatakiwi kufanya hivyo, wakiamua kura zao zitahesabika, wanaweza wakafanya uamuzi kidogo ambao tutaamini wafuasi wa Clinton watavutiwa nao.”

Mtandao huo unaeleza kuwa Clinton alishinda kura ya wengi hivyo anafaa kuwa rais kwa kuwa Trump alishinda majimbo yenye kura nyingi za majimbo basi mwenendo ukaonyesha bayana kuwa atashinda kura za uamuzi.

Katika uchaguzi uliofanyika Novemba 8 mwaka huu, Wamarekani waliwachagua wagombea wa urais kwa kura ya wengi na kuchagua wapigakura watakaomchagua rais mteule mwezi mmoja ujao.

Clinton aliongoza kura za wengi kwa zaidi ya kura 200,000 lakini Trump aliibuka mshindi kutokana na kushinda majimbo yenye kura nyingi za majimbo.

Ili Rais ashinde kinyang’anyiro hicho, anatakiwa kushinda kura 270 kati ya kura 538 zilizopo kutoka majimboni.

Kwa kutumia mfumo wa mshindi wa jimbo anashinda pia kura za uamuzi. Hadi sasa Trump ana kura 306 wakati mpinzani wake, Clinton akiondoka na kura 232. Ni mara chache kwa Marekani mshindi wa urais kuzidiwa katika kura za wengi.

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Fordham, Christina Greer alisema kati ya wajumbe 538 watakaopiga kura mwaka huu, 100 ni maseneta ambao ni wawili kila jimbo, wajumbe watatu kutoka makao makuu ya nchi, Washington D.C, na wabunge 435.

“Majimbo yote kasoro mawili ya Maine na Nebraska mgombea mwenye kura nyingi kwenye jimbo basi ndiye mshindi pia wa kura za wajumbe.

“Hii ina maana matokeo yakitoka tu mwenye kura nyingi huwa ni mshindi licha ya kura kusubiri kura za uamuzi Desemba 19,” Dk Dreer.

Hata hivyo, matumaini ya wafuasi hao wa Clinton huenda yasizae matunda kwa kuwa sheria za majimbo mengi likiwamo la Minnesota Marekani zinakataza uwepo wa “wajumbe wasiowaaminifu” na baadhi yanatoza faini kati ya Dola 500 (Sh1 milioni) za Marekani hadi 1,000 (zaidi ya Sh2 milioni).

Faini hiyo ni matokeo ya uamuzi wa Mahakama juu ya nchi hiyo iliamua mwaka 1952 wapigakura hao wawe wanakula viapo mapema wakati wa mkutano mkuu wa chama juu ya nani watamchagua, mtandao wa Factcheck.org unaochapisha habari za siasa, umeeleza.
 
ukuiona watu wengi walikuwa wanamwuunga mkono bi clinton basi ujue Kulikuwa na Ajenda ya siri nyuma yake.

Haiwezekani mtu hajaanza kutimiza majukumu yake na kupimwa kwa utendaji wake kwa kipindi cha muhula wake wa kwanza.

Alafu watu wanaanza kuandamana kama hakuna msukumo kutoka upande fulani.

Hapa ndipo marekani inapothibitisha kwamba hata wao hawana Demokrasia wanayo jidai kuipigania mchana na usiku kwenye mataifa mengine.

Kama wangekua ni watu wanao ihishi demokrasia basi hii michezo ya tega ni kutege wasingekuwa wanaifanya.

Maana wange siamamia demokrasia kwamba uchaguzi umekwisha na tumeshindwa na tujipange uchaguzi ujao.
 
media are blowing things out of proportion and idiots are just singing along...........
 
Hii inaitwa kujifariji

Trump hakutakiwa kushinda

Ni Kosa la Democrats kuweka mtu dhaifu

Sanders angemuweza sana Trump

Mama clinton ana habari nyingi sana


Watu wa ajabu sana hawa, walifahamishwa mapema kwamba Hillary na kudi lake walifanya vote rigging ili Sanders asiteuliwe kuwa mgombea wa Chama cha Democratic - sasa mtu ungetegemea baada ya kupata taarifa hizo zenye uhakika wangemchukulia hatua kali Hillary na kumuondoa kwenye kinyanganyiro cha kupendekezwa kuwa mgombea wa chama chake.

Sasa nini kilicho tokea? badala ya kumchukulia hatua kali Hillary - wao wakamuacha bila ya kumchukulia hatua yoyote wakakimbilia kumuandama msimamizi wa upigaji kura wa Chama chake akaondolewa kwenye wadhifa wake.

Wanafanya mambo kizezeta zezeta tu - sasa kilipo kuja kinyanganyiro cha upigaji kura wa Rais wa Merikani ndio Trump akahibuka mshindi - katika kiwewe cha kushidwa Hillary kundi lake linakimbilia kumtafuta mchawi na kuleta maigizo eti wanataka kurudia kuhesabu kura!!! Hiyo itawasaidia nini? Wanaendelea kujidhalilisha tu.
 
Nimeamini kuna wazungu vilaza sana...hiv huo utaratibu wa kupiga kura si waliuweka wenyewe...kwa nn hawakubadilusha kabla ya mambo ya uchaguz kuanza..Yaan Kisa kashinda wasiomtaka bac et mashinikizo yaanze...Kwa hiyo wakimuweka huyo mama mfano...na watu wa Trump nao waanze kuandamana......dah.....
 
Back
Top Bottom