NnyaMbwate
JF-Expert Member
- Nov 3, 2010
- 1,678
- 1,204
Nani, Bulembo? Elimu, Elimu, Elimu!
Ni meneja wa kampeni Abdallah Bulembo amemsihi rais aingilie kati.
Tupatupa! Umeambiwa ushauri huo kapewa na Wastara ambaye naye alikuwa mpiga kampeni na no muhanga wa bomoabomoa. Hivi mzee Tupatupa ukiona nyumba ya mchepuko unaowaka kama kama kandili utaacha kuweka itikadi pembeni? Mwache mzee Bulembo aitumie falsafa ya nzi kufia kwenye kidonda sio kosa.Jana, umekaririwa ukipinga zoezi la bomoabomoa linaloendelea jijini Dar es Salaam. Umeshauri na kumuomba Rais Magufuli aingilie kati na kulisitisha zoezi hilo. Ndugu Abdallah Bulembo, ukiwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM Taifa na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, unajua haya?
Unajua kuwa bomoabomoa ndiyo 'inayoibeba' Serikali ya Rais Magufuli na kuonekana inatenda kazi usiku na mchana? Unajua kuwa fukuzafukuza,simamishasimamisha na bomoabomoa ndizo nguzo za 'Hapa Kazi Tu'? Unajua kuwa ili uonekane mtendaji katika Serikali hii lazima utajwetajwe kama uliyefanya maamuzi makubwa kama hayo?
Ndugu yangu Bulembo, nenda taratibu. Wewe ulikuwa Meneja wa Kampeni wa Rais Magufuli kama alivyokuwa Kanali Mstaafu Kinana kwa Rais Mstaafu Kikwete. Ulipokuwa Meneja wa Kampeni uliunga mkono mipango na mikakati ya mgombea na chama kwa ujumla. Mipango yenyewe ndiyo hiyo ya bomoabomoa. Mbona unarudi nyuma?
Kunya anye kuku, akinya bata kaharisha. Tukipinga sisi inakuwa nongwa. Waache watanzania waliomchagua Rais Magufuli waisome namba!
Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
Kwa akili yako kamsihi aingilie kati kwa kuongeza magreda ya kuvunja?Kumsihi "Rais aingilie kati" haimaanishi kupinga.
Hivi hizo shule mlienda kusomea ujinga?
We kijana hapo Houston unaishi maeneo gani?Bulembo ni mswahili swahili
Kwa akili yako kamsihi aingilie kati kwa kuongeza magreda ya kuvunja?
Jana, umekaririwa ukipinga zoezi la bomoabomoa linaloendelea jijini Dar es Salaam. Umeshauri na kumuomba Rais Magufuli aingilie kati na kulisitisha zoezi hilo. Ndugu Abdallah Bulembo, ukiwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM Taifa na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, unajua haya?