Kampeni meneja wa Magufuli Abdallah Bulembo, apinga bomoabomoa

The Phylosopher

JF-Expert Member
Mar 11, 2015
1,503
2,046
Ni meneja wa kampeni Abdallah Bulembo amemsihi rais aingilie kati.
 
Last edited by a moderator:
Kuna dalili kuwa Bulembo na Wastara walijenga mahusiano wakati wa kampeni na haya maneno ni ushauri wa Wastara (muigizaji) anayebomolewa nyumba zake
 
Safi bulembo , NEMC wanafanya sifa sasa , hata watu ambao hawapatwi na mafuriko wanabomolewa kwa lipi hasa
 
Safi bulembo , NEMC wanafanya sifa sasa , hata watu ambao hawapatwi na mafuriko wanabomolewa kwa lipi hasa
kuna umbali uliowekwa kutoka mto. ukiwa ndani yake nyumba inabomolewa. baada ya bomoabomoa huenda mto msimbazi na mingine iliyokua inakatiza jiji itafufuka. vilio vya mafuriko hata manyunyu ya mvua vitakua historia.
 
kuna umbali uliowekwa kutoka mto. ukiwa ndani yake nyumba inabomolewa. baada ya bomoabomoa huenda mto msimbazi na mingine iliyokua inakatiza jiji itafufuka. vilio vya mafuriko hata manyunyu ya mvua vitakua historia.
Mkuu Nemc wamepitiliza hata ule umbali wa mita60 kutoka kwenye kingo za mto ndio maana malalamiko yamekuwa mengi maana hao wengine miaka yote nyumba zao hazijawai kuwekwa X
 
wameshazalisha wakimbizi ndani ya nchi sasa wanatapatapa ... kwanini wasinge wajengea nyumba za milioni 10 kila mmoja ... mbona SA wameweza?
 
Ni meneja wa kampeni Abdallah Bulembo amemsihi rais aingilie kati.
kwa mtu yeyote mstarabu lazima afanye utafiti wa kutosha kabla ya kubomoa hizo nyumba kwani kama ni makosa hata serikali inamakosa kuachia mpaka nyumba zimejengwa hapo ni sawa na mwamke kufanya kosa la kupata mimba alafu unakuja kumuua mtoto kwa kudai kwamba mimba haikuwa ya halali. hapo lazima uingie gharama ya kumlea mtoto na ndivyo ilitakiwa serikali iingie gharama ya kuakikisha wanaobomolewa wanakuwa na mahali pa kuishi
 
Hizi habari za kampeni,mbio za mwenge nk zinazalisha mambo mengi.Niliwahi kusikia eti mbio za Mwenge hueneza maradhi na kuongeza idadi ya watoto wasio na baba zao.Hii ya leo Kampeni imejenga uhusiano kati ya Meneja na Msanii.Hebu tuache haya mambo ya kijingajinga tutafute maendeleo kwa kuwaiga watu wa kanda ya kaskazini ...wachagga nk.
 
Jana, umekaririwa ukipinga zoezi la bomoabomoa linaloendelea jijini Dar es Salaam. Umeshauri na kumuomba Rais Magufuli aingilie kati na kulisitisha zoezi hilo. Ndugu Abdallah Bulembo, ukiwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM Taifa na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, unajua haya?

Unajua kuwa bomoabomoa ndiyo 'inayoibeba' Serikali ya Rais Magufuli na kuonekana inatenda kazi usiku na mchana? Unajua kuwa fukuzafukuza,simamishasimamisha na bomoabomoa ndizo nguzo za 'Hapa Kazi Tu'? Unajua kuwa ili uonekane mtendaji katika Serikali hii lazima utajwetajwe kama uliyefanya maamuzi makubwa kama hayo?

Ndugu yangu Bulembo, nenda taratibu. Wewe ulikuwa Meneja wa Kampeni wa Rais Magufuli kama alivyokuwa Kanali Mstaafu Kinana kwa Rais Mstaafu Kikwete. Ulipokuwa Meneja wa Kampeni uliunga mkono mipango na mikakati ya mgombea na chama kwa ujumla. Mipango yenyewe ndiyo hiyo ya bomoabomoa. Mbona unarudi nyuma?

Kunya anye kuku, akinya bata kaharisha. Tukipinga sisi inakuwa nongwa. Waache watanzania waliomchagua Rais Magufuli waisome namba!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
 
Back
Top Bottom