Kampeni kabla ya uchaguzi tunakusanyika kusikiliza uongo na uzushi wa wanasiasa.

Jumakidogo

R I P
Jul 16, 2009
1,851
417
Hii ndiyo desturi popote pale duniani kuwa, ifikapo wakati wa uchaguzi mkuu wanasiasa hufanya kampeni kwa mbwembwe nyingi ili wapewe nafasi ya kushika hatamu za uongozi. Wakati wa kampeni kuna kila aina ya maneno kutoka kwa wanasiasa wale wanaogombea ama wapambe walio nyuma yao. Huu ndiyo wakati wa wanasiasa kusema uongo kwa kuwadanganya wananchi. Huo ndio wakati wa wanasiasa kusikika wakitoa kashfa, vipasho na hata matusi ya hapa na pale kwa wapinzani wao. Kampeni ni adui wa wananchi kwa sababu, ahadi nyingi hutolewa hadharani lakini kwa sehemu kubwa huwa hazitekelezwi. Wananchi hupumbazwa na ahadi moto moto za watu hawa. Jambo la kushangaza mpaka mwisho wa kampeni unakuta mtu kaahidi mamia ya ahadi ambayo ni muujiza kuyatekeleza yote wakati wa kipindi chake cha uongozi. Hivi hakuna njia na mbinu nyingine mbadala ya kuwapata viongozi kidemokrasia bila ya kutumia mtindo huu wa kampeni? Naona kama tunapoteza muda kukusanyika kwenye mikutano ya kampeni kusikiliza ahadi zisizotekelezeka kutoka kwa wanasiasa, tunakusanyika kusikiliza vijembe na mipasho, tunakusanyika kusikiliza uzushi na maneno ya ushawishi yenye sehemu kubwa ya uongo kuliko ukweli wakati majumbani mwetu tunalala njaa. Uongouongo huu wa wanasiasa tutauvumilia mpaka lini?
 
Back
Top Bottom