youngsharo
JF-Expert Member
- Jan 8, 2015
- 2,491
- 500
Mwana ukawa yeyote kuanzia leo Tarehe 25/09/2015_25/10/2015 unaombwa kumnadi mgombea wetu Edward Lowassa ili aweze kushinda Uchaguzi Mkuu Mwezi Ujao.
Ni muhimu kuwaelezea kiundani zaidi hasa watu wa vijijini kwani wamedanganywa na mgombea wa ccm kuwa wakiichagua Chadema nchi itakuwa kama Libya, Hivyo kwa uelewa mdogo wa watu wa vijijini wameingiwa na uoga na kurudisha majeshi nyuma [fear of unknown] kwa juhudi zako tunaomba kura 5 kutoka kijijini kwako, tunaamini kama kwa sasa tupo milion 2.3 na kila mtu akaongeza watu watano inamaana tutafika million 11.5 ambayo ni sawa na asilimia 97 ya watu wote waliojiandikisha kupata vitambulisho.
Nawasilisha.
Tayari nimepata kura 5 kutoka familia jirani (yangu zamani sana).
Mimi napiga familia kwa familia, na wananielewewa kwa kutumia ushawishi mdogo tu wa AHADI bila vitendo miaka yote (meli, viwanja vya ndege, vyuo vikuu, uchumi wa kati, maisha bora nk).
Kubwa zaidi kwa vijijini ni kupaa kwa bei ya MAFUTA ya TAA, hata vikongwe vijijini wanafeel effect.
Nilikuwa na jamaa yangu leo nikielekea town. Yeye siku zote ni CCM damu. Mbele yetu kukawa na roli la maji. Nikamwambia miaka hamsini ya uhuru bado tunasambaza maji kwa vidumu, halafu watu bado mnapigia kura CCM? Eti jiji kubwa kama hili zaidi ya asilimia 50 ya watu wanategemea maji ya vidumu?
Kwa safari ya leo tu nimefanikiwa kubadili fikra mmoja, hadi tar 25 nafikiri nitakuwa nao wengi.
Asante mkuu tutafanya hivyo ila rekebisha hizo asilimia 97 za wapinga kura. Wamejiandikisha takriban milioni 23
nimefanikiwa kumbadilisha jirani yangu jana mimi pomoja na familia yake tulijumuika kwa chakula chajioni
ilikua ni furaha ilioje
usiwe na shaka maana hata huko vijijini hawaelewi libya ndo wapi na nini kilitokea.Mwana ukawa yeyote kuanzia leo Tarehe 25/09/2015_25/10/2015 unaombwa kumnadi mgombea wetu Edward Lowassa ili aweze kushinda Uchaguzi Mkuu Mwezi Ujao.
Ni muhimu kuwaelezea kiundani zaidi hasa watu wa vijijini kwani wamedanganywa na mgombea wa ccm kuwa wakiichagua Chadema nchi itakuwa kama Libya, Hivyo kwa uelewa mdogo wa watu wa vijijini wameingiwa na uoga na kurudisha majeshi nyuma [fear of unknown] kwa juhudi zako tunaomba kura 5 kutoka kijijini kwako, tunaamini kama kwa sasa tupo milion 4.1 na kila mtu akaongeza watu watano inamaana tutafika million 20.5 ambayo ni sawa na asilimia 89 ya watu wote million 23 waliojiandikisha kupata vitambulisho.
Nawasilisha.
Nimeshawashawishi ndugu zangu huko kijijini tabora wamenielewa kwanza reli imekufa barabara hakuna Umeme hakuna maji hospital nk. Ilikuwa ngumu lakini nimewasihi ccm tangu wamechaguliwa hawajawahi kufika Kwetu kutoa suluhisho la matatizo mpaka kipindi cha uchaguzi