Mkuu Mtanzania,
Tuache ubaguzi jamani, tuache kuhukumu bila ukweli tusichukie wanaanchi wenzetu kwa sababu ni matajiri tu kutoa kwake sio dhambi, kama ana dhambi isemwe hapa lakini tuache hisia kwa sababu ni Mhindi.
Haiwezekani rais akaamuru wahalifu wa EPA, wafikishwe kwenye sheria halafu akarudi kuchukua hela za wahalifu wengine, tusilazimishe tu kwa nguvu uhalifu kwa wananchi kwa sababu hatufanani nao, sio vizuri kwa mshikamano na amani ya taifa letu jamani!
Hili siyo swala la ubaguzi kwamba tunamjadili huyu kwa kuwa ni mhindi, bali tunamjadili huyo kwa kuwa ana tuhuma nzito dhidhi yake katika ufisadi wa ununuzi wa Rada. Huku ni kukumbatia mafisadi na ndiyo maana ufisadi utaendelea kushamiri Tanzania. Usilifananishe hili na ubaguzi hata kidogo. Utajiri wanaoupata kwa kupitia njia za haramu si utajiri unaostahili kupigiwa makofi hata siku moja.
Ndugu yangu FMES,
Naamini tunakubaliana kwenye mambo mengi tu ila moja tu kubwa nalo ni namna ya kupambana na maadui wa taifa letu. Wewe ni mwana CCM na bado una imani kuwa yote yawezekana ndani ya CCM. Mimi kwa upande wangu sijawahi kuwa mwanachama wa chama chochote cha siasa na ni mhitimu tu wa elimu ya sekondari ambacho kwa kiwango cha shule ni kama sijasoma. Nimebahatika tu kwa kujiendeleza na kwa utundu wangu nimeweza kujua kuitumia tovuti na sina utaalamu zaidi ya hapo. Kutofautiana na siasa za kwetu toka umri mdogo kulinifanya niache shule mapema na sasa baada ya miaka hamsini na ushenzi bado msimamo wangu ni ule ule. Sina nia nyingine zaidi ya kuungana na yeyote yule kutetea maslahi ya nchi yangu ninayoipenda Tanzania. Lakini amini usiamini mimi siye unayemfikiria - sina ubia na mtu yeyote humu ndani kwa sababu mbili. Kwanza simfahamu member yeyote wa JF na pili nina hakika hakuna member anayenifahamu hata tukikutana uso kwa uso. Naheshimu sana msimamo wako kwa issues mbali mbali ila hofu yangu ni unavyoonyesha kukerwa na misimamo tofauti na yako. Sisi sote ni binadamu na hakuna aliye perfect - at the end of the day tunajikuta wote ni Watanzania wanaopigania the very best for our country. Asante Mkuu, mag3.
Hapa unajiandikia na kujijibu mwenyewe au umechanganya data za User name katika ku log in?
Hapa unajiandikia na kujijibu mwenyewe au umechanganya data za User name katika ku log in?
Some of us will soon be proved right. Inahitaki moyo wa paka kutetea mambo mengine. Hata hivyo kinachogomba hapa nafikiri ni nani anapokea zaidi kuliko anayetoa huo msaada. Angekuwa anapokea dagaa tu duh JF hapangetosha lakini anayepokea, loh.... funika kombe. JF inapoteza hadhi, koleo haliitwi tena koleo, na nyani anaangaliwa kwanza sura lakini thubutu utamke hivyo. Hivi akina Lowassa, Mkono na hata Mkapa wameshitakiwa ? ..ama kweli, wanavyovaliwa njuga humu JF !!! Kichwa kimenasa, juhudi za kuokoa zapamba moto.... kulikoni ? Sasa ni wakati mwafaka wa kutamka wazi kuwa CCM imeoza, full stop.
Mkuu Mtanzania,
Tuache ubaguzi jamani, tuache kuhukumu bila ukweli tusichukie wanaanchi wenzetu kwa sababu ni matajiri tu kutoa kwake sio dhambi, kama ana dhambi isemwe hapa lakini tuache hisia kwa sababu ni Mhindi.
Haiwezekani rais akaamuru wahalifu wa EPA, wafikishwe kwenye sheria halafu akarudi kuchukua hela za wahalifu wengine, tusilazimishe tu kwa nguvu uhalifu kwa wananchi kwa sababu hatufanani nao, sio vizuri kwa mshikamano na amani ya taifa letu jamani!
Huyu naye ni rafiki wa Somaiya or what?
hii kali!! Na huyu somaiya akiwa kwenye issue ya epa watamkamata kweli?
Mkuu ni kweli kabisa kua enzi za mwalimu huyu asingesogea kabisa kwa sababu ya kuhisiwa tu, maana kulikuwa hakuna sheria enzi hizo, sheria ilikuwa ni yeye Mwalimu,
lakini je unajua enzi za mwalimu CCM walikuwa wanatoa wapi hela za kuendesha chama? angalau siku hizi tunajua kuwa wana ruzuku!
Mtamsingizia vingi Mwalimu (Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi) Ha ha ha ha eti wakati wa Mwalimu kulikuwa hakuna sheria ndiyo maana hawa mafisadi na mabulungutu yao waliogopa kuisogelea CCM ili kutoa misaada ya mabulungutu yao!!! Kama sheria ilikuwa ni yeye Mwalimu tu basi majaji, Mahakimu na wanasheria wangeshalalamika kwamba Mwalimu anawaingilia kwenye kazi zao!!! Na kuwataka kila kesi waamue alivyotaka yeye Mwalimu!!!! lakini hatukusika hata mara moja malalamiko yao!!! Mwalimu hakuwa perfect lakini msimsingimzie vya kumsingizia!!!!
Na siku hizi kwa kuwa tuna sheria nzuri sana Tanzania mafisadi hawaogopi tena kuisogelea CCM na kutoa mabulungutu yao!!!
Hivi umesahau kama TANU na CCM ya Mwalimu ilikuwa inaendeshwa kwa ada toka kwa wanachama!? Wakati ule Watanzania wengi tuliona fahari kutoa ada zetu za kila mwezi maana tuliona chama kimeweka mbele maslahi ya Watanzania na siyo wageni ama mafisadi kama ilivyo hii leo. Au huna 'data' za kukumbuka hayo!?
Maneno umesema mengi sana lakini hayana uhusiano wowote na CCM kupokea msaada wa mwananchi, semeni labda tatizo ni kwa sababu ni Mhindi, dataz nilizonazo ni kwamba CCM enzi hizo ilikuwa haina bajeti wala responsibility, ilikuwa inachota tu serikalini bila idhini yetu wananchi, Mwalimu alikuwa na mazuri na mapungufu pia, lakini no way ninataka kurudi kwenye maisha yake tena yale ya foleni za unga wa njano no thank you!
Mhindi ni mwananchi ametoa mchango wake kwa chama cha siasa, kama kuna sheria inakataza isemwe, kama mhindi ni mwizi isemwe wizi wake, tule naye sahani moja, hisia haziwezi kuwa sheria ni just hisia tu!!
Tunaelewa kwamba CCM ina ubovu, so is vyama vyote vya siasa, lakini tuwe na sababu ya kumshambulia mwananchi anayetoa msaada kwa taifa.
Lakini Tajiri Soros mbona amewahi kutumia dola millioni 20 kusaidia Democrats huko USA, hasa kwenye uchaguzi dhidi ya Bush kwenye term ya pili?
Hapa sidhani kama tatizo ni kutolewa kwa hela, au kwa CCM kupokea hizo hela, labda tatizo ni mtoaji anataka nini au amewahi kutaka nini au amewahi kupewa nini na watawala wetu, kama yanafahamika yawekwe wazi hapa otherwise tusiwakatishe tamaa wananchi wenye nia ya kutoa misaada kusaidia vyama vyetu vya siasa.
Kutoa misaada kwa vyama vyetu vya siasa sio kuvunja sheria ya jamhuri yetu, au?
Date::11/10/2008
Mfanyabiashara atoa Sh400milioni kugharimia mkutano UVCCM
Na Daniel Mjema, Dodoma
MFANYABIASHARA mashuhuri nchini, Tanil Somaiya anayemiliki Kampuni ya Shivacom ametoa Sh400 milioni kugharamia Mkutano wa Uchaguzi wa Jumuiya ya Vijana (UVCCM) unaotarajiwa kufanyika mwezi ujao.
Mfanyabiashara huyo alikabidhi msaada huo unaohusisha vifaa vyenye thamani ya Sh250 milioni na fedha taslimu Sh150 milioni za posho za wajumbe wanaokadiriwa kuwa 1,000, kwa Mwanyekiti wa CCM Rais Jakaya Kikwete katika tafrija fupi iliyofanyika Makao Makuu ya chama hicho mjini Dodoma.
Kabla ya kukabidhiwa kwa msaada huo, Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM, Francis Issack alisema katika kufanikisha mkutano huo wa uchaguzi, Baraza Kuu la UVCCM liliamua kuteua kamati maalumu ya watu wanne ikiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma William Lukuvi, kutafuta fedha.
Wajumbe wengine wanaounda kamati hiyo ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Lawrence Masha, Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja na Somaiya.
Issack alisema Baraza Kuu la UVCCM liliwaagiza kutafuta vifaa 1,000 kila kimoja ambavyo ni pamoja na fulana, kofia, mabegi, kalamu na madaftari ambavyo vilitengenezwa kwa gharama ya Sh250,000 katika kiwanda kinachomilikiwa na Somaiya mwenyewe.
Kwa mujibu wa kaimu katibu huyo, ingawa wajumbe wa Mkutano Mkuu wa UVCCM Taifa ni 750 lakini wapo waalikwa ambao ni pamoja na Rais Kikwete na wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM ambao pamoja na wajumbe wengine watalipwa posho ya Sh50,000 kwa siku.
Akikabidhi msaada huo, Somaiya alisema ameamua kukisaidia chama hicho kwa kuwa yeye ni mkereketwa na mpenzi wa CCM, kauli ambayo ilipongezwa na Rais Kikwete ambaye alisema kwa kutoa msaada huo, mfanyabiashara huyo atakuwa amejitangaza kibiashara.
Tafrija hiyo fupi ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa chama hicho wakiwemo wajumbe wa NEC waliomaliza kikao chao jana mchana na kupitisha majina ya wanachama wanaogombea nafasi mbalimbali za uongozi UVCCM, Jumuiya ya Wanawake (UWT) na Jumuiya ya Wazazi.
Katika hatua nyingine, wazee wa CCM wa wilaya ya Dodoma mjini wamemuomba Rais Kikwete kuharakisha mpango wake wa kupitisha utaratibu unaotenganisha suala la uongozi na biashara ndani ya Serikali na ndani ya chama cha Mapinduzi.
Akisoma risala kwa niaba ya wazee hao Ikulu ndogo mjini Dodoma jana, Mohamed Makbel alisema bila maadili hakuna nidhamu na kutaka linalowezekana leo lisingoje kesho.
Pamoja na hayo ili kulinda umoja wetu tunaomba viongozi wetu wa chama na serikali wanapotofautiana watumie vikao husika vya chama, ilisema sehemu ya risala hiyo.
Pia waliomba kupitiwa kwa sheria ya mwaka 1979 iliyoagiza Dodoma kuwa eneo maalumu la uwekezaji ili sheria hiyo ihuishwe kuwawezesha wawekezaji wengi kuwekeza Dodoma na kuufanya mkoa huo kuwa kitovu cha usambazaji wa bidhaa mbalimbali katika nchi za Afrika Mashariki na Kati.
Walimpongeza Rais Kikwete kwa uamuzi wake wa ujasiri wa kuamua kujenga chuo kikuu cha Dodoma na ujenzi wa uwanja wa kisasa wa ndege wakisema uamuzi huo umeongeza shauku kubwa ya maendeleo ya kiuchumi ya mkoa huo wa Dodoma.
Akiwahutubia wazee hao, Rais Kikwete alisema azima ya serikali ya makao makuu kuhamia Dodoma iko palepale na kwamba amefarijika na hotuba ya wazee hao kwani imeonyesha namna ambavyo bado wako pamoja na serikali yao katika kupigania maendeleo ya wananchi.
Kuhusu suala la kuufanya mkoa wa Dodoma kuwa eneo huru la kibiashara, Rais alisema utekelezaji wa suala hilo ulikwishaanza japo kasi yake haiendi kama ilivyotarajiwa lakini aliahidi kuwa serikali italitazama suala hilo ili shabaha iliyokusudiwa na Serikali iweze kufanikishwa.
Maneno umesema mengi sana lakini hayana uhusiano wowote na CCM kupokea msaada wa mwananchi, semeni labda tatizo ni kwa sababu ni Mhindi, dataz nilizonazo ni kwamba CCM enzi hizo ilikuwa haina bajeti wala responsibility, ilikuwa inachota tu serikalini bila idhini yetu wananchi, Mwalimu alikuwa na mazuri na mapungufu pia, lakini no way ninataka kurudi kwenye maisha yake tena yale ya foleni za unga wa njano no thank you!
Mhindi ni mwananchi ametoa mchango wake kwa chama cha siasa, kama kuna sheria inakataza isemwe, kama mhindi ni mwizi isemwe wizi wake, tule naye sahani moja, hisia haziwezi kuwa sheria ni just hisia tu!
Tunaelewa kwamba CCM ina ubovu, so is vyama vyote vya siasa, lakini tuwe na sababu ya kumshambulia mwananchi anayetoa msaada kwa taifa.