• Mpendwa mteja, tunakusihi jitahidi kuosha mikono kwa maji safi na sabuni mara kwa mara na kwa siku chache hizi jaribu kutulia nyumbani kuepusha maambukizi ya #CORONAVIRUS

Elections 2015 Kampeni CCM: Ndugai ampiga mgombea mwenzake, azimia na kukimbizwa hospitali huko Kongwa

M

Mshimba

Member
Joined
Jun 13, 2011
Messages
24
Points
45
M

Mshimba

Member
Joined Jun 13, 2011
24 45

Hatimaye Mheshimiwa Ndugai amechimbia kaburi la kisiasa baada ya kumshambulia Mgombea mwenzake aitwae Dr Joseph Elieza Chilongani kwa gongo katika mkutano wa kuomba kupigiwa kura za maoni CCM

Hayo yametokea leo mnamo saa saa 10 jioni katika kitongoji cha ugogoni mjini Kongwa.

Katika kile kinachoonekana ni kuishiwa sera na kutumia ubabe na ukorofi ili kutetea nafasi yake ya kugombea ubunge wa Jimbo la Kongwa, Mheshimiwa Naibu Spika wa Bunge La Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mbunge wa Jimbo la Kongwa alipiga kwa gongo ambalo amekuwa akitembea nalo huku wasimamizi wa uchaguzi wakifumbua macho kitendo cha mgombea kutembea na silaha hiyo kwenye kampeni.

Inadaiwa na mtu aliyefuatilia kwa karibu tukio hilo mkutanoni kuwa Kuna mgombea mmojawapo (mkazi wa Kongwa aitwaye ngatunga) Alisimama kuuza sera zake na kudai kuwa Kongwa kuna madini jimbo halijafaidika na chochote kutoka kwa wachimbaji wa madini... Mara moja Ndugai alimtishia kuwa anyamaze la sivyo angemuonesha kazi kwa kile anachodai kuwa ni kuongea upuuzi..

Wakati wagombea hao wakiendelea kujibizana suala hilo ndipo ghafla mheshimiwa alipomuona Mmojawapo wa wagombea aitwaye Dr Joseph Chilongani ameshika simu na kutahamaki kuwa alikuwa akimrekodi kwa kuvunja taratibu.

Ndipo Job Ndugai alipoamka na kumwambia "Tena wewe nilikuwa nakutafuta siku nyingi sana, unanirekodi na makamera yako na leo utanitambua mimi ni nani."

Mara Ndugai akakusanya nguvu na kumpiga Dr Chilongani kwa fimbo hiyo. aidha hata baada ya kuanguka chini Ndugai alimfuata na kumrukia kumkanyaga tumboni akiwa na hasira na nia ovu ya kutaka kumdhuru zaidi..

Baadae wananchi walipata hasira na kutaka kumshughukilia kwa kichapo Mbunge huyo na ndipo alipopanda haraka gari lake haraka na kukimbi Eneo la Tukio..Inasadikiwa yule mgombea mwingine alijaribu kumnyanyua Dr. Pale chini, jambo ambalo baadhi ya wananchi walilichukulia ni kama kutaka kumdhuru zaidi hivyo walianza kumpa kichapo huyo mgombea mwengine kiasi hadi watu wengine walipoamulia.. Baada ya tukio hilo ovu mkutano ulivurugika.

Ndugu zake Dr. Chilongani kwa kusaidiana na watu walimbeba akiwa amezimia na kumkimbiz hospital baada y kupata PF 3 toka polisi.

Hadi reporter anaondoka hospitalini Dr alikuwa bado hajazinduka na madaktari walikuwa wanaendelea na harakati za kuokoa maisha ya mgombea huyo.

Shuhuda mmoja wa tukio anasema kuwa tukio hilo lilirekodiwa na pengine ushahidi huo utatumika katika kumuengua Ndugai katika kinyanganyiro cha ugombea ubunge kwa ticket ya CCM hasa baada ya watia wengine kuweka pingamizi mara mbili lakini bado uongozi wa chama ulikuwa unafumbia macho.

Baadhi ya wanachama wa CCM walidai kuwa kama haki itatendeka Ndugai atakuwa amejichimbia kaburi la kisiasa na kushuhudia KIAMA CHAKE RASMI KATIKA SIASA ZA JIMBO LA KONGWA..

Updates;

Alie shambuliwa Kongwa, yuko admitted Hospitali ya Wilaya Kongwa. Hali yake ina recover na hakuna hata dalili ya kumhamishia Hosptali ya Mkoa Dodoma.

CHanzo: CID wa Kongwa.
 
Attachments:

  • File size
    38 KB
    Views
    7,536
Last edited by a moderator:
KING COBRA

KING COBRA

JF-Expert Member
Joined
Nov 10, 2011
Messages
2,783
Points
1,225
KING COBRA

KING COBRA

JF-Expert Member
Joined Nov 10, 2011
2,783 1,225
Aliyekuwa Naibu Speaker Job Ndugai amempiga Fimbo ya Kichwani Mtia nia Dkt Joseph Chilongani eneo la Kata ya Ugogoni na amekimbizwa Hospitali ya Kongwa.

Mkuu wa Wilaya na Katibu wa CCM Kongwa wamekimbilia huko kumuona !!!!!!!

Hatimaye Mheshimiwa Ndugai amechimbia kaburi la kisiasa baada ya kumshambulia Mgombea mwenzake aitwae Dr Joseph Elieza Chilongani kwa gongo katika mkutano wa kuomba kupigiwa kura za maoni CCM

Hayo yametokea leo mnamo saa saa 10 jioni katika kitongoji cha ugogoni mjini Kongwa.

Katika kile kinachoonekana ni kuishiwa sera na kutumia ubabe na ukorofi ili kutetea nafasi yake ya kugombea ubunge wa Jimbo la Kongwa, Mheshimiwa Naibu Spika wa Bunge La Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mbunge wa Jimbo la Kongwa alipiga kwa gongo ambalo amekuwa akitembea nalo huku wasimamizi wa uchaguzi wakifumbua macho kitendo cha mgombea kutembea na silaha hiyo kwenye kampeni.

Inadaiwa na mtu aliyefuatilia kwa karibu tukio hilo mkutanoni kuwa Kuna mgombea mmojawapo (mkazi wa Kongwa aitwaye ngatunga) Alisimama kuuza sera zake na kudai kuwa Kongwa kuna madini jimbo halijafaidika na chochote kutoka kwa wachimbaji wa madini... Mara moja Ndugai alimtishia kuwa anyamaze la sivyo angemuonesha kazi kwa kile anachodai kuwa ni kuongea upuuzi..

Wakati wagombea hao wakiendelea kujibizana suala hilo ndipo ghafla mheshimiwa alipomuona Mmojawapo wa wagombea aitwaye Dr Joseph Chilongani ameshika simu na kutahamaki kuwa alikuwa akimrekodi kwa kuvunja taratibu.

Ndipo Job Ndugai alipoamka na kumwambia "Tena wewe nilikuwa nakutafuta siku nyingi sana, unanirekodi na makamera yako na leo utanitambua mimi ni nani."

Mara Ndugai akakusanya nguvu na kumpiga Dr Chilongani kwa fimbo hiyo. aidha hata baada ya kuanguka chini Ndugai alimfuata na kumrukia kumkanyaga tumboni akiwa na hasira na nia ovu ya kutaka kumdhuru zaidi..

Baadae wananchi walipata hasira na kutaka kumshughukilia kwa kichapo Mbunge huyo na ndipo alipopanda haraka gari lake haraka na kukimbi Eneo la Tukio..Inasadikiwa yule mgombea mwingine alijaribu kumnyanyua Dr. Pale chini, jambo ambalo baadhi ya wananchi walilichukulia ni kama kutaka kumdhuru zaidi hivyo walianza kumpa kichapo huyo mgombea mwengine kiasi hadi watu wengine walipoamulia.. Baada ya tukio hilo ovu mkutano ulivurugika.

Ndugu zake Dr. Chilongani kwa kusaidiana na watu walimbeba akiwa amezimia na kumkimbiz hospital baada y kupata PF 3 toka polisi.

Hadi reporter anaondoka hospitalini Dr alikuwa bado hajazinduka na madaktari walikuwa wanaendelea na harakati za kuokoa maisha ya mgombea huyo.

Shuhuda mmoja wa tukio anasema kuwa tukio hilo lilirekodiwa na pengine ushahidi huo utatumika katika kumuengua Ndugai katika kinyanganyiro cha ugombea ubunge kwa ticket ya CCM hasa baada ya watia wengine kuweka pingamizi mara mbili lakini bado uongozi wa chama ulikuwa unafumbia macho.

Baadhi ya wanachama wa CCM walidai kuwa kama haki itatendeka Ndugai atakuwa amejichimbia kaburi la kisiasa na kushuhudia KIAMA CHAKE RASMI KATIKA SIASA ZA JIMBO LA KONGWA..

B

babylata

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2015
Messages
3,317
Points
2,000
B

babylata

JF-Expert Member
Joined Jul 28, 2015
3,317 2,000
imekuwaje tena ccm zaidi ya hongo sasa wanataka kuuana kaanza wasira kaja kangi sasa ndugai kazi ipo
 
L

lubajaro

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2015
Messages
1,198
Points
1,195
L

lubajaro

JF-Expert Member
Joined Mar 29, 2015
1,198 1,195
Bora wapigwe tu, kwani hamna namna tena
 
mimitungi

mimitungi

JF-Expert Member
Joined
May 14, 2013
Messages
631
Points
195
mimitungi

mimitungi

JF-Expert Member
Joined May 14, 2013
631 195
Ndugai anatumia cheo chake vibaya. Mwaka huu CCM wana kazi.
 
gnassingbe

gnassingbe

JF-Expert Member
Joined
Jun 14, 2015
Messages
4,721
Points
2,000
gnassingbe

gnassingbe

JF-Expert Member
Joined Jun 14, 2015
4,721 2,000
imekuwaje tena ccm zaidi ya hongo sasa wanataka kuuana kaanza wasira kaja kangi sasa ndugai kazi ipo
Ngumi nje nje nitaanza kufuatilia hiyo mikutano ya watia nia nijionee sinema ya bure.
 
NGANU

NGANU

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2012
Messages
1,914
Points
1,225
NGANU

NGANU

JF-Expert Member
Joined Oct 18, 2012
1,914 1,225
Bungeni kuna ulaji ndugu ndo maana anafanya kila linalowezekana ili arudi na isitoshe atakuwa kahidiwa uspika si unajua tena mwaka huu spika lazima awe mwanaume kama ilivyotokea kwa Makinda .
POLE YAKE NDUGAI.
 
SHIMBA YA BUYENZE

SHIMBA YA BUYENZE

JF-Expert Member
Joined
Dec 22, 2014
Messages
120,015
Points
2,000
SHIMBA YA BUYENZE

SHIMBA YA BUYENZE

JF-Expert Member
Joined Dec 22, 2014
120,015 2,000
Habari kama hii bila picha ni uzushi!
 
balibabambonahi

balibabambonahi

JF-Expert Member
Joined
Apr 5, 2015
Messages
8,344
Points
2,000
balibabambonahi

balibabambonahi

JF-Expert Member
Joined Apr 5, 2015
8,344 2,000
unajifanya we we ndo mjanja sana,mjuaji kweli,utapigwa tu
 
Chimunguru

Chimunguru

JF-Expert Member
Joined
May 3, 2009
Messages
10,583
Points
2,000
Chimunguru

Chimunguru

JF-Expert Member
Joined May 3, 2009
10,583 2,000
Ccm kwishnei naona wanachapana tu na kutoa rushwa
 
charty

charty

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2013
Messages
7,354
Points
2,000
charty

charty

JF-Expert Member
Joined Oct 28, 2013
7,354 2,000
naona wameanza kupanic live..hahaa alianza wasira naona ndugai naye amefuata...
 
Forum statistics

Threads 1,403,301
Members 531,177
Posts 34,419,952
Top