Kampala International University kuna mgomo

Kampala International University kuna mgomo

Joined
Oct 10, 2014
Posts
14
Reaction score
4
Mi ni mwanafunzi wa kinachoitwa 'chuo kikuu cha kimataifa kampala' chuo hiki kwa kushirikiana na TCU kwa pamoja wamewalaghai watanzania...., kwanza T.C.U Wamewezaje kusajili wanafunzi zaidi ya 650 kujiunga na kozi za afya (b.pharmacy,b.medicine na b.medical lab) kana kwamba taasisi zote za nchi zinazohusika na usajili wa wataalamu wa afya kama (baraza la wafamasia,madaktari na wataalamu wa maabara) hazikitambui chuo hiki pamoja na kozi hizi kwa ngazi zote kuanzia ngazi ya cheti,stashahada na shahada

hiyo ni kwa upande wa usajili.na cha kushangaza zaidi jambo hili linajulikana hadi na waziri wa elimu na viongozi wote wa husika wa ngazi za juu.

La pili,mwongozo wa masomo ya chuo hiki yaani(cariculum/prospectus) haupo ,chuo hakina mtaala mfano wanafunzi wa diploma mwaka wa tatu wamerudishwa mwaka wa pili kwa kigezo kwamba mpaka chuo kifuate mtaala wa afya wa kufundishia kama ilivyoagizwa na NACTE.Kwa sasa chuo kinatumia mtaala wa uganda ambao ni kinyume na vyuo vyetu vya tanzania.

Na mengine ni mengi sana ikiwa ni pamoja na utofauti wa ada,mfumo wa supplimentary umekuwa ni wa kibiashara zaidi kwa gharama yake ni kubwa sana ukilinganisha na vyuo vingine(40,000tshs kwa somo na kuappeal ni 100,000tshs),uongozi wa chuo umejaa waganda na wanigeria pia wao kwa wao hawaelewani.


HIVI SASA TUKO KWENYE MGOMO LEO NI SIKU YA 3 LAKINI HATUJUI HATIMA YETU KWA SABABU MKURUGENZI WA T.C.U ALIFIKA SIKU YA IJUMAA NA KUONDOKA BILA KUSEMA CHOCHOTE NA ESCOT YA ZAIDI YA MAASKARI 20 CHI YA UONGOZI WA O.C.D.


TUNAOMBAA MSAADA TUFANYEJE WATANZANIA IKIWA SERIKALI IMETUSUSA!

YANAYOENDELEA:-


========================
========================


[TABLE="align: center"]
[TR]
[/TR]
[TR]
[TD] KIU_Strike3.jpg

Kamanda wa Polisi wa wilaya ya kipolisi Gongo la Mboto jijini Dar es Salaam, JCN Simba, akizungumza na baadhi ya wanafunzi wa shule ya afya na sayansi shirikishi ya chuo kikuu cha kimataifa cha Kampala (KIU), kampasi ya Dar es Salaam, huko Gongo la Mboto nje kidoho ya jiji leo Jumanne Aprili 15, 2015.

Wanafunzi wote kuanzia mwaka wa kwanza hadi wa tano wanaochukua shahada, stashahada na vyeti, kwenye taaluma za madawa, pahamasi, na maabara, wamegoma jana, wakipinga chuo hicho kuendesha kozi hizo bila ya kuwa na cheti kutoka baraza la wafamasia la wizara ya afya na ustawi wa jamii, kama sheria inavyotaka.

Ingawa chuo hicho kimesajiliwa na tume ya vyuo vikuu (TCU), lakini sheria inataka chuo hicho kipate cheti cha kutambuliwa kozi inazotoa hususan katika masuala ya tiba kutoka kwenye baraza hilo.

Akizungumzia mgomo huo, Mkurugenzi wa mawasiliano wa chuo hicho, Uki Keneth, alikiri shule hiyo kutokuwa na cheti hicho, lakini akaelezea juhudi za chuo toka mwaka 2012za kuhakikisha cheti hicho kinapatikana, zinafanikiwa.

Hata hivyo alisema, chuo kina barua ya kuruhusiwa kuendesha kozi hizo kutoka baraza ingawa kisheria barua hiyo haina uzito wowote wa wanafunzi wanaohitimu masomo ya sayansi ya afya chuoni hapo kitambuliwa katika soko la ajira.


Chanzo:
KhalfanSaid Blog
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
 
sisi ndio tulioanza na hiko chuo hapo gongo la mboto mwaka 2010 ,chuo cha kijinga sana
 
Hata NBAA hakikitambui chuo hichi.
 
Jamani hakuna kinacho ni umiza kama upangaji wa matokeo,kama uki below course work una repeat semester????? shereia za wapi jamani halafu kwanini msitutalifu mapema miongozo yenu....
TCU please mtusaidieeee tunaomba
 
Hapo endelezen mgomo na msilegeze kamba hata kidogo...otherwise itakula kwenu..
Ila msifanye fujo,,,,endeleen kutafuta solution kweny ngaz za juu za uongoz serikalin...
 
Hali si shwari kampala,OCD azuia daradara zilizokuwa zimetubeba kuelekea wizarani,wanafunzi wazuia barabara,zaidi ya FFU 40 watawanya wanafunzi.hakuna aliyeumia,uongozi was juu wakimbia ofisi na kufunga ofisi za utawala.
mpaka sasa wanafunzi wamezagaa maeneo ya chuo....wakisubiri uongozi wa mkoa (mkuu wa mkoa) na uongozi toka wizara ya afya ambao umeahidi kufika chuoni muda wowote kuanzia sasa
 
Daaa kumbukaaa kozii za afya zinaitajii userious sanaaa sasa kwamtindoo huoo mtatoa watuu competitive kweliii!!?? Hapoo hakuna chuo biashara tuu
 
komaeni ndugu zangu hao waganda wasiwachezee akili, mimi wananiudhi sn! Hayo ni maisha yenu mkilegeza kamba imekula kwenu! TCU hawajielewi wawashieni moto coz wanawapotezea muda kwa kugeuza taaluma za watu km biashara!
 
Du siyakucheka hicho chuo magumashi kabisa tatizo nilikuja ktk graduate ya mdogo wangu hapo kina mikono ya watu wa juu ktk serilikali na rushwa wanazitoa zinakurejesheni nyuma kweli. TCU Maboya waliwapeleka watu vipi kuja kusoma hapo kupitia Tcu wakati chuo hakijapitishwa na bodi husika ya mambo ya afya ama kweli elimu biashara komaeni tu mtafanikiwa
 
Mimi najiuliza mpaka ninachoka,ili kuwaje TCU ikaruhusu huu upuuzi,
Mwaka wa kwanza ,Bachelor of medicine anda surgery (BMS) wapo wanafunzi 300
Mwaka II wapo 25
Mwaka III wapo 6
Mwaka IV wapo 5
Swali miaka hiyo yote TCU,walikuwa hawalitambui hilo,kwa sababu hao walioko mwaka IV,waliingia mwaka 2011,ambapo mfumo wa kudahili wa wanafunzi kupitia TCU na NACTE ulianza 2011, kwa maana hiyo wanafunzi wa kwanza kabisa wali dahiliwa na TCU,..swali miaka hiyo yote TCU walikiwa hawalitambuiii kweli????Tanzania na watanzania Tuweni serious
 
Kitu kingine wali wanafunzi wa mwaka wa nne kwa BMS ...kwa yeyote ambaye anawajua hasa wanafunzi wa pale chuoni,wale kweli ni watanzania?? nina mashaka hilo
 
Jamani naombeni mwenye taarifa yoyote kuhusu mgomo wa wanafunzi wa chuo cha Kampala KIU. Pale Gongo la Mboto
 
Serikali imelala. Badala ya kufungia chuo cha hovyo kama hiki
 
Back
Top Bottom