Kamishna Nsato Marijani: Tukio la Mauaji ya Polisi Kibiti sio ugaidi, tunaanzisha Operesheni maalumu

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,879
6,356
mm (1).png


Kamishna wa Operesheni na Mafunzo ya Jeshi la Polisi, Nsato Marijani ameongea na waandishi wa habari mchana huu na kutolea ufafanuzi tukio la mauaji ya Askari Polisi 8 lililotokea jana jioni huko Kibiti, Pwani.

CP Marijani ameeleza kuwa tukio hilo sio la kigaidi kama ambavyo imekuwa ikivumishwa, bali ni tukio la kawaida la ujambazi ambalo halililazimu Jeshi la Polisi kuunda Kanda Maalumu ya Kipolisi kwa Mkoa wa Pwani.

Aidha, amesisitiza kuwa, hilo ni tukio la kawaida na wala sio tukio la kutisha na kuzua hofu bali imetokea tu bahati mbaya mapolisi kuuawa na wao kama Jeshi Imara watazidisha mapambano na kudumisha ulinzi.

Mpaka sasa, wameshajibu mashambulizi yaliyowalaza chini majambazi 4 na idadi yao itaongeza kwa kuwa imeundwa operesheni maalumu ambayo haitokuwa na mzaha wala msamaha.

Pia ametangaza kuwa kwa maeneo ya Mkuranga, Kibiti na Rufiji ni marufuku pikipiki kutembea baada ya saa 11 jioni.

Nikimnukuu CP Nsato Marijani

"Ninasema wazi kwamba hiki ni kitendo ambacho hakikubaliki, mpaka sasa nimekwishapoteza askari zaidi ya kumi. Ninaamini wanatosha.

Kuanzia sasa jeshi linakwenda kwenye operesheni maalumu, hatutokuwa na mzaha wala msamaha, tutafanya kile ambacho Jeshi linapaswa kufanya.

Tutawafuata popote walipo, tutawashughulikia kikamilifu na hakuna ambaye atakayebaki. Na mapambano haya hayana mwisho, yaani huu ni mwanzo hayana mwisho. Askari 10 ni wengi sana.

Wananchi mtuwie radhi, mtuunge mkono. Katika hili mtaona sura halisi ya Jeshi la Polisi

Dawa ya moto ni moto, tuna uhakika tutawakamata, sasa hivi ni nane kwa nne lakini magoli yetu yatakuwa mengi kuliko wao.

Wale wote ambao walikuwa wanafikiria kufanya ujambazi wa aina hii wa kutumia silaha wajue kwamba dawa ya moto ni moto."


Mwisho wa kunukuu
 
Mkuu;
Tumesha yazoea majibu yao hawa. Hawawezi kusema kuwa wamewashindwa. Ningetamani kama pamoja na kujibu mapigo, wasije wamaliza watu wema wakiwaacha hao wahuni wakipeta juu ya uso wa nchi. Kama kamanda wa operation, aanzishe pia kitengo cha mafunzo upya ya polisi kuhusu uhusiano wao na raia wengine.

Zamani, ma informer walikuwa watu wa kawaida tu. Leo, hiyo ipo?? Polisi sio kazi ni wito. Wengi wa vijana wake waliomba kazi, hawana wito. Ningelikuwa ni mimi mkuu ningelilifumua jeshi hilo loote nianze from the scratch. Sio kuwapeleka ati kuwa wakuu wa mikoa na zima moto. Waende shamba wala sio Kibiti bali Rukwa.
 
Na hili ndio tatizo la hawa polisi.
Hili sio tukio la kawaida na kuna kila ishara kwamba sio la ujambazi.By definition Jambazi huwa wanaenda kupora mali,ku-ambush polisi na kupora silaha haiwezi kutafsiriwa kama tukio la ujambazi.
Niliona habari kwenye uzi mwengine humu kwamba ati baada ya tukio,walichukuliwa vijana ambao walikwisha kamatwa siku za nyuma ili wakaoneshe wenzao walipojificha.lakii baada ya kufika palitokea mapambano na vijana hao kufariki na wahalifu kutoroka. Hii taarifa ya huyu Marjani na na hiyo ya awali zinajichanganya zenyewe.
Kwa uzoefu wangu wa ufanyaji kazi hovyo wa jeshi letu la polisi ni kwamba baada ya kuuliwa polisi8 walichofanya walienda kuwachukua vijana walikuwa mahabusu kama suspect na kuwauwa kama kulipiza kisasi kisha kutengeneza stori.
Kwa mtindo huu hawataweza kulitatua hili tatizo milele.Hawa waliowauwa polisi ni watu wa agenda na wana believe in something na they are fighting for a course,iwe ni legitimate course or not but they are fighting for a course.
Kuficha ukweli,kuplaydown the problem na kuuwa watu kiholela kwa nia ya kulipiza kisasi hakutatui tatizo bali kutaongeza tatizo.
Hicho kikundi kilichopo hayo maeneo kimejipanga na polisi wanaporeact kimihemko wao kwao ndio inawapa nguvu.
Ni wakati sasa jeshi la polisi kufanya kazi kitaalamu zaidi na sio kwa kukurupuka na kutumia mbinu outdated.
 
Huyo kamishina aseme ukweli, na wale wanaogoma kuhudhuria mahakaman kule Arusha wanakabiliwa na mashtaka yapi?????
Waseme tu ukweli kuwa nchi hii ina magaidi bhas tujue namna ya kujilinda
 
Hiyo sentence ya mwisho ina ukakasi!!! Katika operations kama hizi ndipo polisi huharibu uhusiano wao na jamii!! Maana hapa watu watateswa ili wawataje wahusika hata kama hawajui.....mateso nayo pia uporaji hutokea kwa maana polisi wakikuta Mali kata kama ni TV au computer hudai risiti kama huna hondoka na Mali hizo!!!!!! Operation inatakiwa itende haki
 
Tukio la kawaida? hivi hizi kauli viongozi wanapata jeuri wapi tukio lakawaida mtu mmoja kuua watu nane he's not serious au kwa vile ye anastarehe na kuzunguka kwenye kiti haendi lindo eti kawaida ***** ungekufa wewe au ndugu yako afu tuone kama kawaida ngese we
 
Tukio la polisi wanane kuuwawa ni tukio la kawaida tu. Watanzania msiwe na hofu msherehekee pasaka vizuri tu na mchape kazi hapa kazi tu! ( kwa sauti ya Sizonje)

Eh! Mungu inusuru nchi yetu!

Kamishna wa Operesheni na Mafunzo ya Jeshi la Polisi, Nsato Marijani ameongea na waandishi wa habari mchana huu na kutolea ufafanuzi tukio la mauaji ya Askari Polisi 8 lililotokea jana jioni huko Kibiti, Pwani.

CP Marijani ameeleza kuwa tukio hilo sio la kigaidi kama ambavyo imekuwa ikivumishwa, bali ni tukio la kawaida la ujambazi ambalo halililazimu Jeshi la Polisi kuunda Kanda Maalumu ya Kipolisi kwa Mkoa wa Pwani.

Aidha, amesisitiza kuwa, hilo ni tukio la kawaida na wala sio tukio la kutisha na kuzua hofu bali imetokea tu bahati mbaya mapolisi kuuawa na wao kama Jeshi Imara watazidisha mapambano na kudumisha ulinzi.

Mpaka sasa, wameshajibu mashambulizi yaliyowalaza chini majambazi 4 na idadi yao itaongeza kwa kuwa imeundwa operesheni maalumu ambayo haitokuwa na mzaha wala msamaha.

Msikilizeni zaidi kwenye video hiyo hapo chini..
 
Omg tukio hili la kawaida jamani akati familia zimepoteza ndugu Zao!! Kweli msiba sikia kwa wenzio usiombe ukupate ndo utajua ni kawaida au ni wakuumiza..ee Mungu tunusuru waja wako.
 
Hivi uchunguzi umeshafanyika?Kama bado jibu kama hawa ni majambazi sio magaidi limepatikanaje?This is funny.Dah,naihurumia nchi yangu Tanzania.Fumbo mfumbe mjinga,mwerevu atatambua!
 
Weledi wa viongozi wa Polisi siku hizi unatia kichefuchefu. Hao majambazi wa kusubiri polisi watoke lindo wawavizie na kuwaua kisha wachukue silaha 9, ni ujambazi wa aina yake. Naomba tafsiri ya ujambazi labda.
 
IGP Mangu kweli CP Marijani wanauwawa Polisi wanane kazini then anasema Tukio la KAWAIDA tu tusiwe na wasiwasi???

Kweli IGP kweli kabisa ....No No this is unacceptable IGP Mangu kwa huyu CP Marijani

Ni lini tena Polisi wetu wamewahi kuuwawa kwa Idadi kubwa kama huyo kwa Mara moja?? Halafu CP Marijani anasema ni tukio la KAWAIDA tu.
 
Back
Top Bottom