four eyes
JF-Expert Member
- Jan 11, 2017
- 905
- 1,406
Kuna hii vita iliyoanzishwa kwa kasi sana na ndugu yetu mkuu wa mkoa na ambayo ilizua taharuki na taflani kubwa sana nchini huku ikifanikiwa kusambaa sehemu kubwa ya nchi.
Pamoja na lawama kadha wa kadha angalau vuguvugu lile liliwezesha kutajwa Kwa watumiaji na wauzaji wa madawa hayo ambao wengi wao wamekuwa wakitajwatajwa chinichini kwa muda mrefu sana.
Katikati ya vita hyo iliyokuwa katika mtindo wa series na wakati tukiwa bado tunafaidi season za awali kabisa labda kutokana na kelele mbalimbali kuhusu uhalali au namna ya uendeshaji vita hiyo ghafla rais akakumbuka kumteua kamishna wa madawa ya kulevya bwana Siang'a na ambae akakabidhiwa jukumu la vita hiyo pamoja na majina ya watoto wa wakubwa na vigogo wa madawa hayo.
Kinachonisononesha ni ukimya uliofuatia baada ya vita hii kukabidhiwa huyu bwana, hakuna tena cha majina wala kesi mahakaman na suala hili limeanza kufifia kama awali huku vigogo walioanza kuwa na hofu wakipata tena amani ya moyo.
Swali langu ni je huyu bwana aliteuliwa ili kuizima vita hii au? Aliahidi kuendeleza "tempo" iliyokuwepo lakini ukimya wake unadhihirisha kitu tofauti,
Karibun wadau ambao mmeshaliona hili ili tuchangie.