Profesa Kabudi: Nilitumwa kazi Canada nikasumbuliwa sana. Niliandika barua ya kujiuzulu lakini kabla sijaipeleka kwa Rais nikanyan'ganywa

mwanamwana

JF-Expert Member
Aug 1, 2011
1,076
4,113
Katika hafla inayoendelea sasa hivi Ikulu ya Utiaji saini kati ya Tanzania na Barrick Gold, Profesa kutoka Jalalani akiwa anatoa hotuba yake bila tashwishwi amedai kwamba alitumwa kazi na Rais Magufuli lakini kazi ile hakufanikiwa na ikawa fedhaha kubwa kwake kwa kutumwa kazi na Rais na kushindwa kuitekeleza, hivyo alichukua maamuzi ya kumwandikia Rais barua ya kujiuzulu lakini kabla hajaifikisha sehemu husika akawa amepokonywa.

Nanukuu

Katika kujadili mikataba 9 itakayosainiwa leo, hicho kipindi kilikuwa kigumu. Hawakuwa hawa, walikuwa wenzao hawapo hapa. Sipendi kuwataja majina ila hawakutaka mikataba hii isainiwe na tufanikiwe. Kila tulipokutana na kukubaliana kesho yake walibadilika


Ilifika mahali Rais nilitaka kuingiwa na dhambi ya kukata tamaa na vitimbi hivyo vilishia kwa wao wenyewe kufukuzana kazi. Leo nataka kumshukuru Luteni Kanali Mstaafu Richard William

Tulipofika kukata tamaa, Rais nilikuwa nimendika barua ya kujiuzulu kuja kwako. Kwamba kazi uliyonipa imenishinda. Aibu hii na fedheha hii nitaibeba. Barua hiyo sikuileta maana Casmir Simba Kyuke alininyang'anya na kuichana

Nilisema sijawahi kutumwa kazi na Mkuu wangu wa nchi nikashindwa, ila sasa hawa watu hawataki. Rais unaniuliza mnakwendaje, mbona nasikia hamuendelei! Namjibu tunaendelea huku najua hatuendelei.Ndipo nilipowapigia Maaskofu wangu wa Anglikana.
 
Ama kweli nchi hii tumefanywa mambumbumbu mizungu ya reli. Huyu mtoka jalalani angekuwa anaheshimu akili za Watanzania asingethubutu ku-pupu hivi hadharani.

Ina maana aliwaalika hao watu "waliomnyang'anya barua kabla hajaiandika? Au aliwatangazia watu kuwa anaandika barua ya kujiuzulu?

God have mercy on this country
 
Ama kweli nchi hii tumefanywa mambumbumbu mizungu ya reli. Huyu mtoka jalalani angekuwa anaheshimu akili za Watanzania asingethubutu ku-pupu hivi hadharani.
Ina maana aliwaalika hao watu "waliomnyang'anya barua kabla hajaiandika? Au aliwatangazia watu kuwa anaandika barua ya kujiuzulu?
God have mercy on this country

Si ndio hapo sasa, anamaanisha kuwa hivi sasa hapo ikulu wanakaa vibaka ukifika na barua wanaichana!
 
Kwahiyo kule canada kumbe tulipigwa? Siyo kama tulivyoaminishwa kuhusu makinikia

Sent using Jamii Forums mobile app
Hahaha! Mkuu unafikiri kwa haraka sana! Maana Canada tulishindwa ila alizuiwa kujiuzulu! Kwa hiyo Barrick walitufunga dobo kwa hili. Ndio maana walikuwa wanakanusha taarifa zilizotolewa na serikali kwamba hivyo sivyo tulivyokubaliana!
 
Hatari mwananguuuuu
tapatalk_1574972654826.jpeg


dodge
 
Back
Top Bottom