Profesa Kabudi: Nilitumwa kazi Canada nikasumbuliwa sana. Niliandika barua ya kujiuzulu lakini kabla sijaipeleka kwa Rais nikanyan'ganywa

Alikuwa akiipeleka huku kila mtu njiani akiiona?
Hiyondiyo siasa.
Prof. mzima anadanganya ili ionekane wanamheshimu mkubwa wao. Sasa hapo anataka kumwambia boss wake kuwa hata yeye anania ya kujiuzulu au, lakini wakati ni mwalimu mzuri. Tusubiri tu.
 
When Kabudi addresses an audience you’d be forgiven to assume he was giving a church sermon to a Christian audience rather than speaking as a national minister.

Who recommends these bozzos to senior posts.

Hakuna mtu mwenye akili zake timamu atamtuma Kabudi kufanya contract negotiation ni serikari ya Tanzania tu.
Wewe hizo contract negotiations tangu uzaliwe mpaka leo hii imeshazifanya ngapi?.
 
mwanamwana,
Jama muongo ni muongo sana kama kiungo kashata anaetishia kupita huku na mpira ghafla anasita na kupita kwingine.
Kama ni kweli Kabudi ni aina ya watu wa kujiuziru basi angejiuzuru kwenye lile sakata la korosho pale alipowabeba machokoraa na wakora na kuwapeleka Ikulu akimuaminisha rais kuwa ni wafanyabiashara wakubwa.
Kabudi umeshakuwa mtu mzima sasa, na si busara taifa likakutambua kama mtu mzima muongo ambaye kula na kuishi kwake kunategemea sana tabia za uongo uongo alio nao.

Nakukumbusha tu kwamba mwenzako Lugola alitumbuliwa dakika chache tu baada ya kumaliza kukata mauno na huku akiwa anajifuta jasho lililotokana na mauno hayo huku kelele za kumshangilia kwa mauno yake zikiwa hazijaisha. Wewe ni kati ya wapotoshaji wakubwa wa taifa hili.
 
Wewe hizo contract negotiations tangu uzaliwe mpaka leo hii imeshazifanya ngapi?.
Kabudi alikuwa amefanya mingapi kabla ya kupewa kazi? Vinginevyo kwa Tanzania kila mtu anaweza kama yeye kaweza.

Walau mimi naelewa negotiation elements za contract ya mikataba kwenye natural resources unlike him ukimsikiliza tu unaona hana anachokijua.

Kwa kilichoongelewa leo ndio kile kile people like me have always thought what was behind the scene.

Ni Barrick tu walitaka kulimaliza baada ya kuona washavuna sana bila ya kupitia njia za mahakama and guess what nina uhakika mkataba wa awali ukija hadharani financial wise walichowekeza na walichovuna mpaka sasa still its a bad deal tulichopewa ndani ya Twiga.

The whole thing concluded out of pity, I could have told you that 3 years ago after listening to Prof Thornton; and not because of the skills possessed by Kabudi.
 
Huku ni kujitafutia kiki tu.
Kama alinyang'anywa hiyo barua, kwa nini akuandika nyingine? Kwani alinyang'anywa mawazo aliyokuwa nayo?
Ni mbwembwe tu za kiototo za viongozi wa awamu hii. Si unakumbuka mkubwa wao alisema alikuwa anabeep tu simu ikapiga kabisa na sasa yupo ofisi kuu. Mara akasema mimi sikutaka ila watu fulani wakanisukumiza kwenye ofisi ya cheo alicho nacho.
 
Katika hotuba ya Prof Kabudi ikulu amemtaja kijana mdogo Kasmir Simba Kyuke kuwa alimnyanganya barua na kuichana, naombeni wanaomjua watupe wasifu wake kijana hodari na mchapa kazi na mwenye msimamo kuntu. Huyu pia katajwa kama msiri mkuu wa serikali kweli ni msiri yaani mazungumzo yote hayajavuja hata chembe, ni kijana mwenye roho ngumu sana.

Halafu kuna kijana mdogo kabisa katajwa kwenye tume ya majadiliano huyu unaweza mkuta njiani ukamzaba hata kibao kumbe kichwani ni mzima balaa, napendekeza hii team ya kabudi ipewe heshima ya kipekee.
 
Back
Top Bottom