Kambi ya jeshi yavamiwa Kinshasa DRC

Kambi ya jeshi yavamiwa Kinshasa DRC

MK254

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2013
Posts
33,574
Reaction score
53,605
Nilidhani JWTZ wamemaliza mgogoro wote huko Congo, bado shughuli ipo.


22 Julai, 2014 - Saa 19:22 GMT



140722191853_majeshi_yazima_shambulizi_kinshasa_drc_512x288_bbc_nocredit.jpg
Majeshi yazima shambulizi Kinshasa DRC


Kumetokea ufyatulianaji mkali wa risasi katika kambi ya kijeshi katika mji mkuu wa Kinshasa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Taarifa zinasema kuwa raia wameondolewa katika eneo hilo na haijafahamika makabiliano hayo yaliyotokea katika kambi ya wanajeshi wa kumlinda rais yametokana na nini.
Wadadisi wa mambo wanahisi kwamba kisa hiki huenda kikazusha utata tena kati ya Congo Kinshasa na Congo Brazzaville kwa vile shambulio lilitokea karibu na mpaka kati ya nchi hizo mbili.
Taarifa kutoka kwa serikali zinasema kuwa wavamizi walijaribu kupenyeza katika kambi ya kijeshi ya Camp Tshatshi na makabiliano yalizuka kwa zaidi ya dakika 30 hivi.
Jamhuri hiyo ya Kidemokrasia ya Congo imesakamwa na vita kwa kipindi kirefu sasa na hata rais aliyepo madarakani kwa sasa Joseph Kabila alichukua mamlaka baada ya kuuawa kwa babake Laurent Kabila mwaka wa , 2001.
140722191802_majeshi_yazima_shambulizi_kinshasa_drc_512x288_bbc_nocredit.jpg
Majeshi yazima shambulizi Kinshasa DRC


Duru zinasema kuwa wavamizi takriban 20 walijaribu kuingia ndani ya kambi hiyo lakini shambulizi likazimwa .
Raiya walihamishwa kutoka maeneo yaliyoko karibu na uwanja wa ndege ulifungwa wakati wa shambulizi hilo.
Serikali bado haijamtaja nani aliyeishambulia .
Hii sio mara ya kwanza kwa Camp Tshatshi kushambuliwa mwaka uliyopita kami hiyo ilishambuliwa tena na wakati huo wafuasi wa dini ya ya kikristo ya dhehebu linaloongozwa na Paul Joseph Mukungubila walilaumiwa.


 
Congo nini tena bila shaka watakua waasi wa serikali ya Rais Joseph Kabila Jr.
 
Back
Top Bottom