Kambi ya jeshi yatekwa Nigeria

Kambi ya jeshi yatekwa Nigeria

KAMJUS

Member
Joined
Mar 16, 2012
Posts
83
Reaction score
16
Waziri wa Ulinzi wa Nigeria amethibitisha kuwa kambi yake moja ya kijeshi mpakani mwa Nigeria na Chad, imetwaliwa na wapiganaji wa kiislaamu.

Mkuu wa jeshi la angani Alex Badeh, amesema kuwa wanajeshi wa Nigeria ndio waliokuwa katika kambi hiyo ya kijeshi, inayotumika na wanajeshi wa mataifa mbalimbali.

Kambi hiyo iliyoko kando ya ziwa Chad ilishambuliwa siku ya Jumamosi na wapiganaji wa boko haram.

BBCswahili.com
 
Ajabu kambi ya jeshi kutekwa na paramilitary?
 
Yaani kama kambi ya jeshi inatekwa hebu piga goti uwahurumie wananchi wa hali ya chini ambao silaha yao kubwa ni panga butu.

Hii ni aibu ni fedheha!

Ee Mungu wape moyo wa ubibadamu ha BokoHaramu!
 
Hao boko haram silaha wanazomiliki ndio napopata tabu kutoamini kama hamna mkono wa Mmarekani hapo
 
Hili suala nakuwa na wacwac na hiz nchi za afrika na majeran zake.

Vita nigeria c dini, ni utajiri wa mafuta.
 
Hivi huyo Waziri wa ulinzi anapata wapi ujasiri wa kutangaza kuwa kambi ya kijeshi imetekwa?
This story is not real!
 
oil is a curse instead of blessing,marekani ni wabaya sana..
 
Marekani Nuksi,tayari Hivi Sasa Wamempakata Nyalandu Ili Wamtumie Kutuuza.
 
Akili zingine bhana zimejaa kamasi tu, bokoharamu wanaua watu mijitu mingne inakuja na longolongo eti ni mmarekani,
 
Akili zingine bhana zimejaa kamasi tu, bokoharamu wanaua watu mijitu mingne inakuja na longolongo eti ni mmarekani,

we kalia hivyohivyo kuwatetea mabwana zako wamarekani wabaya sana hawa watu wanafitina mbaya sana we waone hivyo tu
 
Kuteka kambi ya jeshi sio kitu kidogo,

Ujue vita inapotokea ni opportunity kubwa sana kwa baadhi ya watu, wananufaika na vita inayoendelea kwenye nchi zenye utajiri wa vitu flani
 
Jamani huko kaskazini si ndiyo kwenye majimbo yaliyopiga kura yajitawale kwa sharia? Na boko haramu wanapigania utawala wa sharia hukohuko ktk majimbo ya kaskazini. Sasa sielewi kwa nini majeshi yawapige boko wakati wakazi wa huko walikuwa radhi kabisa wawe chini ya mfumo wa sharia. Wakati mwingine huwa napata jibu kuwa inawezekana ndiyo maana walioko majimbo ya kusini wanakuwa kama hawajali vile kile kinachoendelea kaskazini. Jamani kupanga ni kuchagua. Kaskazn walichagua majimbo yao yajiendeshe kwa sharia na ndiyo huo unaosistizwa na boko. Waache shule na mambo mengine ya kimagharibi. Nadhani boko h wanatekeleza kwa nguvu zote lile azimio la Abuja la mwaka 1987. Mwenye macho haambiwi tazama na kupanga ni kuchagua
 
Back
Top Bottom