Hii ya Mbagala iwe funzo kwa Taifa kwa ujumla, na kuna kambi nyingi sana zimezungukwa na makazi ya watu, Ukonga asilimia kubwa ni Jeshi kuna Kikosi cha anga, Magereza na FFU ukija kawe kuna JKT, Lugalo JWTZ, Mgulani JKT, kigamboni ni kikosi cha wanamaji, na vyote hivyo vimezungukwa na raia sasa tuliulize je ikitokea bahati mbaya kama ya mbagala itakuwaje. Na sehemu nyingi za makambi hayo ujenzi wake ni holela na watu ni mwengi nikimaanisha makazi ya watu wengi sana kutofautisha na sehemu nyinginezo.
Ukija Wazo kiwanda cha saruji na chenyewe ni bomu kubwa tu, hapo turudi nyuma kidogo miaka ya mwanzoni mwa 90's kulikuwa pori kubwa hasa tena la kutisha hata njia yenyewe ilukuwa ni mbinde kupita kipindi cha mvua lakini sasa ni kama uzunguni kuna nyumba za kufa mtu barabara zimechongwa vilivyo zinapitika kipindi chote, na sio kuwa waliojenga huko ni kina mbavu mbili lahasha ni watu wenye vijisenti vyao vya uhakika na wanaelewa madhara ya kile kiwanda kiafya na mazingira.
Ukija Tanesco pale Ubungo ile mitambo nayewe siku ya siku ikijibu sijui tutamlaumu nani, mitambo imezungukwa na makazi ya watu wengi mno.
Nina swali moja tu : Je! watu wote waliojenga maeneo hayo hatarishi wapelekwe wapi?
Ushauri wangu kwa Serikali yetu itowe mafunzo au Elimu kwa wananchi.