Kamati za Kudumu za Bunge

Tony Almeda

JF-Expert Member
Sep 18, 2011
397
122
Hivi hizi kamati ni lazima ziwe za kudumu?
Je kamati nazo zikiboronga zinawajibika vipi?
Kama ripoti ya kamati ya Uchukuzi ya Peter Serukamba, Mpaka mh John Mnyika anaifanyia mabadiliko kipengele muhimu kwa maslahi ya taifa hili, Kamati nzima inamaana walikuwa wako pale kwa maslahi binafsi na si ya taifa?

Kama JK alivyowatosa maNundu na Mfutakamba, kwa nini mh Anna Makinda na kamati yake ya uongozi asimtoe nduki huyu Serukamba, na kuisambaratisha kamati hii kama waliopo uwezo wao ni mdogo katika kuhoji, kusimamia na kuishauri serikali?
 
Naomba nijibu kipengere cha kwanza kwa jinsi mimi nilivyoelewa:
Rejea Ibara ya 96 ya Katiba ya JMT inasema;
(1)Bunge laweza kuunda Kamati za Bunge za namna mbalimbali kadri litakavyoona inafaa kwa ajili ya utekelezaji bora wa madaraka yake.
(2)Kanuni za Bunge zaweza kufafanua muundo na shughuli za kamati za Bunge zitakazoundwa kwa mujibu wa masharti ya ibara hii.

My take: ktk kipengere hiki basi Kamati za Bunge si lazima ziwe za kudumu huweza pia kuwa za muda kadri Bunge litakavyoona inafaa.
 
Kwa kuzingatia swali lako la Pili; kama Kamati ikiboronga basi yapaswa kuwajibishwa kulingana na Kanuni za Bunge.Rejea Ibara ya 89 ya katiba ya JMT;
(1)Bila ya kuathiri masharti ya Katiba hii Bunge laweza kutunga Kanuni za Kudumu kwa ajili ya kuweka utaratibu wa kutekeleza shughuli zake.
(2) Kanuni za Kudumu zilizotungwa kwa mujibu wa ibara hii zaweza kuweka utaratibu wa kusimamia utekelezaji wa shughuli za Bunge ndani ya Bunge na zile za Kamati na Kamati ndogo za Bunge.
 
Hakuna kamati ilyodhalilisha bunge kama kamati hii. Kamati zote zilionyesha ukomavu mkubwa isipokua hii ya miundombinu hasa iliposhauri(kwa kushinikiza) kampuni ipewe kazi wakati ikijua wazi kua tenda ya kazi hiyo haijatangazwa popote.
 
Sipingani na maelezo yako labda unielewe katika maoni ya kamati au wakati kamati inapendekeza na kuacha kutoa mapendekezo muhimu (Nadhani hili linategemea weledi wa wajumbe wa kamati) kama lilivyoibuliwa bungeni na Mh JJ Mnyika.
Taifa kujua gharama halisi za mradi just simple (Wakati kamati iling'ang'ania kuiambia serikali mradi uanze mara moja) bila kufanya tathmini.
Sijui hapo vipi kaka nadhani hii kamati ilalambishwa au uswahiba wa aliekuwa naibu waziri na mwenyekiti wa kamati ndio uliosukuma kamati kutoa mapendekezo yenye mapungufu?
 
Hakuna kamati ilyodhalilisha bunge kama kamati hii. Kamati zote zilionyesha ukomavu mkubwa isipokua hii ya miundombinu hasa iliposhauri(kwa kushinikiza) kampuni ipewe kazi wakati ikijua wazi kua tenda ya kazi hiyo haijatangazwa popote.
Morinyo: Hata mimi ndio nilipoishangaa hii kamati na hii ilikuwa inapelekwa pelekwa na naibu waziri Athumani Mfutakamba, bahada ya kumshika masikio mwenyekiti wa kamati.
 
Back
Top Bottom