Kamati za Bunge | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kamati za Bunge

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mbopo, Feb 25, 2011.

 1. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #1
  Feb 25, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Mimi nimeshangazwa na Wenyeviti wa baadhi ya Kamati za bunge letu la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na hasa hawa waliochaguliwa majuzi kuongoza kamati za nishati, miundombinu na kamati ya mambo ya nje, ulinzi na usalama.

  Muda mfupi baada ya wakubwa hawa kuteuliwa wamekuwa wanatoa matamko mbalimbali ambayo yanaleta picha kana kwamba wao ni wasemaji wa wizara zilizo chini ya kamati hizo. Wakati mwingine wao wamekuwa kama watendaji wa serikali. Mifano miwili ya haraka ni mwenyekiti wa kamait ya nishati na madini ambaye ame-take advantage ya mgao wa umeme kuwa kama vile yeye ndiye waziri na wakati mwingine MD wa Tanesco. Mfano wa pili ni mwenyekiti wa kamati ya mambo ya nje , ulinzi na usalama ambaye naye ametoa tamko zito kuhusu harakati na hatimaye mapinduzi ya umma yaliyohitimisha utawala wa Mubarak. Mkubwa huyu alitoa tamko ambalo kwa kweli liliibua hisia kwamba huo ndiyo msimamo wa Tanzania bila kujali athari za kidiplomasia na hasa kwa kuzingatia mahusiano yetu na Misri na ukweli kwamba mpaka sasa hivi bado mabaki ya utawala wa Mubarak (kupitia jeshi) yapo madarakani. Ukiachilia mbali unafiki uliojaa katika tamko lake hilo (maana yeye hana tofauti na Mubaraka kwa uchu wa madaraka na kujilimbikizia mali), mimi nafikiri kamati hizi ni vizuri zikaelewa kwamba zenyewe ni watchdog institutions zikitekeleza majukumu ya bunge ambayo ni kuishauri na kuikosoa serikali pale inapobidi. Vinginevyo tutajikuta tukishuhudia watu wakijinyakulia madaraka ya uwaziri wakati hawamo kwenye baraza la mawaziri. Hili ni baya, hasa linapofanywa na kusumkumwa na ajenda ya 2015.
   
 2. D

  Dotori JF-Expert Member

  #2
  Feb 25, 2011
  Joined: Nov 3, 2007
  Messages: 547
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Good observation....Inaonekana kama kamati zinaendesha shughuli za kila siku za wizara, jambo ambalo sio sahihi. Katika hili la Tanesco ni
  vyema Bunge ikawa ni chombo cha kuhoji badala ya kuwa sehemu ya maamuzi. Maana ikiwa Bunge itakuwa sehemu ya maamuzi nani atahoji Wizara na taasisi husika?
   
 3. AMARIDONG

  AMARIDONG JF-Expert Member

  #3
  Feb 25, 2011
  Joined: Jun 24, 2010
  Messages: 2,506
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 0
  fisadi anatetea ufisadi wake na wa mwenzake hamna kupingana hawa ni kama luba
   
 4. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #4
  Feb 25, 2011
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 145
  Naona katika bunge hili la 10 viongozi wa hizi kamati wanakuja juu sana. Nimemsikia pia Serukamba-kamati ya miundo mbinu akizungumza kimamlaka kama waziri husika
   
 5. k

  kukubata Member

  #5
  Feb 25, 2011
  Joined: Oct 9, 2010
  Messages: 69
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kuanzia raisi hadi baraza lake la mawazilri ni mambumbumbu
   
 6. F

  Froida JF-Expert Member

  #6
  Feb 25, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Kila kitu ni shaghala bagala nchi hii watu hata hawajui kikomo cha uongozi wao
   
 7. sijuikitu

  sijuikitu JF-Expert Member

  #7
  Feb 25, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 286
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mi kila nikimuona January najiuliza hivi Ngeleja ndio nani tenaaa?...nimeshaanza kumsahau.

  Nahisi kama kungekuwa na kamati ya kumsimamia rais tungemsahau JK within 24 hours.
   
 8. S

  Salimia JF-Expert Member

  #8
  Feb 25, 2011
  Joined: Feb 14, 2011
  Messages: 665
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Very true! Tumekuwa na mabunge mengi tangu uhuru na sikuwahi kusikia wenyeviti wa kamati za Bunge wana nguvu kuliko hawa wa sasa. Aidha wakati mwingine ilikuwa ni nadra sana kwa watu wa kawaida kujua wenyeviti wa kamati hizi labda mtu awe mfuatiliaji sana wa masuala ya Bunge. Lakini tutazame leo hii, nani asiyejua kwamba January ni mwenyekiti wa kamati ya nishati na madini tena akiwa ameshika wadhifa huo katika kipindi kifupi sana? Same thing kwa Lowassa, ameona njia ya kutokea sasa.
  Labda wengi hawajui tu kwamba kamti hii ya madini na nishati imeundwa yote na Lowassa kuanzia mwenyekiti hadi wajumbe. Unapomweka January mwenyekiti halafu makamu Diana Chilolo (darasa la saba), na wajumbe akina Vick Kamata, nani atamchallenge January? Labda kidooooogo Ole Sendeka. Vinginevyo ni mpango mkakati wa Lowassa kama ilivyo kwa kamati yake ya ulinzi,nje na usalama.
  Hawa watu wajihoji nafsi, wapunguze kasi, wawe wa kuhoji na si kushiriki maamuzi kama baadhi ya waungwana walivyotangulia kunong'ona hapo juu.
  Nawasilisha.
   
 9. e

  ebwana eh Member

  #9
  Mar 2, 2011
  Joined: Feb 24, 2011
  Messages: 18
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  walichaguliwa na kina nani?
   
Loading...