Kamati za bunge mnatuchefua

Kamati za bunge mnatuchefua

shauri ya wote ni waogeleaje wa bahari ya siri ya ufisadi .ni mpaka siku tutakapo ipiga nyama chini chama cha mafisadi
 
Dr Slaa,Zito, Mnyika, Tindu lisu, January! najua mnaweza kutengeneza hoja kwanini kila wakati kamati zinapopita katika wizara na taasisi kama zilizotajwa na wahusika wengine humu jamvini na kugundua upotevu mkubwa wa fedha,
1. Hatua hazichuliwi?.
2. watendaji hawawajibishwi?.
3. Tafadhalini tusaidieni kwa kutumia njia sahihi hawa watendaji wafikishwe mahakamani.
Nasikia uchungu sana ninaposikia upotevu wa mabilioni ya shilingi, na kamati ya bunge inaishia kufoka halafu hakuna chochote kinachoendela.
 
Tangu lini mchafu akamsafisha mchafu mwenzie? Tafakakari
 
wakuu ni tatizo la katiba ya Tanzania kamati wajibu wake ni kushauri serikali na sio kuchukua hatua ndo maana hakuna siku utaona mapendekezo ya bunge yanafanyiwa kazi wamebaki kupiga kelele tu.tukibadlli katiba ndo tunaweza kufanya angalau mabadiliko kidogo
 
Kuna upotoshaji mkubwa sana katika hizi kamati za bunge, zinazopitia mahesabu ya taasisi, mashirika, mawizara n.k. Kwanza siyo wabunge wanaoibua hizo hoja au upotevu kama wao wanavyotaka ijulikane. Wanai ibua hizo hoja ni Wakaguzi kutoka ofisi ya Mkaguzi mkuu. Na katika vikao hivyo, kinachofanyika ni kupitia vitabu vya mahesabu na taarifa za mkaguzi mkuu kwa mwaka uliopita. Hivyo wabunge hawaibui wanataka umaarufu tu wa kisiasa. Taarifa ya CAG huwa na taarifa mbalimbali zikiainisha upungufu uliojitokeza katika matumizi au utunzaji wa kumbukumbu. Kwa mfano wataandika masufuru ambayo hayajarejeshwa mil kadhaa, manunu ambayo hayana risiti mil kadhaa, na mambo mengine mengi, ambayo kimsingi siyo wizi au upotevu, bali tu ni baadhi ya nyaraka zinakuwa hazijawekwa sawa.
Baada ya vikao hivyo, taasisi husika hupewa muda wa kujibu na kufanyia kazi hoja mbalimbali na mwisho wa siku, kama mtu hakuwa amerejesha masurufu (imprest retirement), atajaza form na hoja kufutwa. Kama hakukua na risiti risiti itachukuliwa na kuwekwa kwenye jalada, hoja inafutwa na hatimaye hoja zoooote hufutwa na hakuna mtu anayekuwa na hatia.

Ni muhimu kujua kuwa kinachotajwa mara nyingi kama ufisadi au upotevu wa pesa huwa siyo kwamba watumishi wamechukua hizo hela na kuziweka mifukoni mwao, bali huwa ni aidha kitu kimefanyika lakini taratibu sasa hazikufuatwa, au retirement haijafanyika n.k.
Kamati hupaza sauti tu kujustify uwepo wao na posho zao.
 
Tafadhalini tusaidieni kwa kutumia njia sahihi hawa watendaji wafikishwe mahakamani.
song3.jpg
song2.jpg
 
Lifutwe mbona dubai hakuna Bunge na mambo yanaenda vzr?
 
bunge la tanzania na kamati zake halitofautiani hata kidogo na joka la kibisa, kumbuka wabunge wengi pamoja na spika wanajipendekeza kwa serikali ili wapate vyeo na mambo mengine, unategemea watapata wapi ujasiri wa kuiwajibisha serikali. kumbukeni maazimio ya bunge juu ya kampuni hewa ya richmond, jairo, ngeleja, cag na luhanjo. hakuna lililotekelezwa mpaka sasa bado bunge limekaa kimya kama hakuna kilichotokea. bunge na wabunge wanapenda kudhalilishwa na kujidhalilisha. kwa busara ya kawaida ni bora ukakaa kimya kuliko kusema jambo bila kuchukua hatua, huu ni udhaifu mkubwa.
 
Wana JF kila siku tuanaskia madudu,ubadhilifua,Uzembe,Rushwa na Ufujaji wa Mali za Uma na kupotea uadilifu kwa Viongozi ambao unai buliwa na KAMATI za Kudumu Za Bunge,
Sasa ni Kipi kinachokataza watu hawa kuchuuliwa Hatua? Kwa Niaba ya Wagosi wenzangu Hapa Tanga sasa tumechoshwa na kuskia UOZO usiochukuliwa hatua kwa kuirekibisha au Kuwachukulia Hatua wahusika(MNATUCHEFUA)
Jamani sasa Basi tumechoka na vikao vyenu visivyo na Hatua za utendaji zaidi ya kutupasha tu Habari,kazi hiyo iacheni Magazeti..
Hata Maamuzi yenu Bungeni sasa hayana Mashiko na ndo Maana Uchaguzi uliopita watu wengi hawakujitokeza kupiga Kura...
Na posho za vikao hivyo ni balaa, pampja na kutochukua hatua yoyote, wanaendelea kufyonza funds za siye walipa kodi, ile ni kama TV series yani, wana maana gani kama siyo kujionyesha tu na hakuna dead end au conclusion zenye mshiko!
 
Kuna upotoshaji mkubwa sana katika hizi kamati za bunge, zinazopitia mahesabu ya taasisi, mashirika, mawizara n.k. Kwanza siyo wabunge wanaoibua hizo hoja au upotevu kama wao wanavyotaka ijulikane. Wanai ibua hizo hoja ni Wakaguzi kutoka ofisi ya Mkaguzi mkuu. Na katika vikao hivyo, kinachofanyika ni kupitia vitabu vya mahesabu na taarifa za mkaguzi mkuu kwa mwaka uliopita. Hivyo wabunge hawaibui wanataka umaarufu tu wa kisiasa. Taarifa ya CAG huwa na taarifa mbalimbali zikiainisha upungufu uliojitokeza katika matumizi au utunzaji wa kumbukumbu. Kwa mfano wataandika masufuru ambayo hayajarejeshwa mil kadhaa, manunu ambayo hayana risiti mil kadhaa, na mambo mengine mengi, ambayo kimsingi siyo wizi au upotevu, bali tu ni baadhi ya nyaraka zinakuwa hazijawekwa sawa.
Baada ya vikao hivyo, taasisi husika hupewa muda wa kujibu na kufanyia kazi hoja mbalimbali na mwisho wa siku, kama mtu hakuwa amerejesha masurufu (imprest retirement), atajaza form na hoja kufutwa. Kama hakukua na risiti risiti itachukuliwa na kuwekwa kwenye jalada, hoja inafutwa na hatimaye hoja zoooote hufutwa na hakuna mtu anayekuwa na hatia.

Ni muhimu kujua kuwa kinachotajwa mara nyingi kama ufisadi au upotevu wa pesa huwa siyo kwamba watumishi wamechukua hizo hela na kuziweka mifukoni mwao, bali huwa ni aidha kitu kimefanyika lakini taratibu sasa hazikufuatwa, au retirement haijafanyika n.k.
Kamati hupaza sauti tu kujustify uwepo wao na posho zao.

Yote hayo uliyoyaorodhesha yanatokana na kuwa na wahasibu incompetent(VIHIYO). Kwa kuwa majibu hayo hutolewa kwa lugha ya kiingereza basi ripoti kutoka kwa baadhi ya wahasibu wetu hawa ni kituko!

Nadhani waruhusiwe kujibu hoja hizi kwa kiswahili!
 
Hii ndio tofauti yetu kubwa na matatifa yaliyoendelea. Wao kila kosa ni au madai au jinai na sisi kila kosa linakabiliwa kisiasa!! Inaitwa "impunity". Kuanzia Rais, CAG, Takururu na Kamati za Bunge wote wanazugumzia upotevu wa fedha tena wakisema kabisa "kutumiwa vibaya au bila taratibu kufuatwa" lakini utasikia.

a) Rais - "Nawaomba muache mara moja tabia hiyo"
b) CAG - "kazi yangu ni kutoa ushauri kwa serikali"
c) Takururu - "tukipata ushahidi wa kutosha tutawafikisha mahakamani"
d) Kamati za Bunge "taifa linapoteza mapato kwa taratibu kutofuatwa, tutaishauri serikali iwe angalifu"

Katika yote hayo hatuoni adhabu kwa wakosaji. Tsu Nzu, mwandishi wa zamani sana wa Uchina ambaye kitabu chake cha "The art of war" ni text book katika vyuo vya kijeshi vya kimagharibi alisema "Kila tendo litakuwa na au pongezi au adhabu"!! Sisi tuna mambo mengi yenye kuhitaji adhabu lakini tutayapongeza kwa maneno matamu ya "acha", "usirudie"!!
 
Vikao vya kamati za bunge ni vya kuwania posho tu na kuuza sura katika vyombo vya habari. Wakati serikali ikikabiliwa na UKATA mkubwa na hivyo kushindwa kutoa fedha za matumizi ya kawaida katika idara zake wabunge wanaendelea na vikao vyao visivyo na tija.

By the way kwa nini vikao vya bunge visipunguzwe ili kuokoa fedha zinazohitajika sana na walala hoi wa nchi hii kwa ajili ya matibabu?
 
imind pole kwa kuwa huna unalolijua, unataka kupotosha umma, watafute wahasibu wakueleweshe, imprest isyofutwa ni sawa na fedha iliyoibiwa, malipo yasiyo na nyaraka ni sawa na malipo hewa. hivyo kutenganisha wizi na hicho kinachoandikwa ni kupotosha watu kwa kutokujua kwako.
 
Yote hayo uliyoyaorodhesha yanatokana na kuwa na wahasibu incompetent(VIHIYO). Kwa kuwa majibu hayo hutolewa kwa lugha ya kiingereza basi ripoti kutoka kwa baadhi ya wahasibu wetu hawa ni kituko!

Nadhani waruhusiwe kujibu hoja hizi kwa kiswahili!
Nilifanya kazi serikalini, ni kaamua kuacha baada ya kuona ubabaishaji ni mwingi. Kuna matatizo kadhaa. Kwanza mfumo wa utendaji serikalini is tooo manual, kiasi hata utunzaji wa kumbukumbu ni shida. Kwa hiyo wakati mwingine siyo kweli kuwa huwa hizi nyaraka hazipo, bali huwa ni vigumu kupatikana pale zinapohitajika kutokana na utunzaji kumbukumbu wa kizamani.
Pili sheria za ajabu ajabu ambazo hazina tija. Kwa mfano hiyo ya kurejesha masurufu ni usanii tupu. Sheria ya manunuzi ni usanii mtupu n.k. Ambao hawajahi kufanya kazi serikalini, inakua vigumu kuelewa kwa jinsi mifumo ya serikali ilivyo duni, na isiyo na ufanisi. Mbaya zaidi hakuna mtu anachukua hatua.
 
Kuna upotoshaji mkubwa sana katika hizi kamati za bunge, zinazopitia mahesabu ya taasisi, mashirika, mawizara n.k. Kwanza siyo wabunge wanaoibua hizo hoja au upotevu kama wao wanavyotaka ijulikane. Wanai ibua hizo hoja ni Wakaguzi kutoka ofisi ya Mkaguzi mkuu. Na katika vikao hivyo, kinachofanyika ni kupitia vitabu vya mahesabu na taarifa za mkaguzi mkuu kwa mwaka uliopita. Hivyo wabunge hawaibui wanataka umaarufu tu wa kisiasa. Taarifa ya CAG huwa na taarifa mbalimbali zikiainisha upungufu uliojitokeza katika matumizi au utunzaji wa kumbukumbu. Kwa mfano wataandika masufuru ambayo hayajarejeshwa mil kadhaa, manunu ambayo hayana risiti mil kadhaa, na mambo mengine mengi, ambayo kimsingi siyo wizi au upotevu, bali tu ni baadhi ya nyaraka zinakuwa hazijawekwa sawa.
Baada ya vikao hivyo, taasisi husika hupewa muda wa kujibu na kufanyia kazi hoja mbalimbali na mwisho wa siku, kama mtu hakuwa amerejesha masurufu (imprest retirement), atajaza form na hoja kufutwa. Kama hakukua na risiti risiti itachukuliwa na kuwekwa kwenye jalada, hoja inafutwa na hatimaye hoja zoooote hufutwa na hakuna mtu anayekuwa na hatia.

Ni muhimu kujua kuwa kinachotajwa mara nyingi kama ufisadi au upotevu wa pesa huwa siyo kwamba watumishi wamechukua hizo hela na kuziweka mifukoni mwao, bali huwa ni aidha kitu kimefanyika lakini taratibu sasa hazikufuatwa, au retirement haijafanyika n.k.
Kamati hupaza sauti tu kujustify uwepo wao na posho zao.

Umenena ya ukweli halisia
 
Back
Top Bottom