Kamati yakataa ripoti ya Jiji la Mwanza

Kamati yakataa ripoti ya Jiji la Mwanza

Peter Dafi

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2012
Posts
394
Reaction score
272
Mwanza. Ripoti ya mapato na miradi ya maendeleo ya Jiji la Mwanza, imekataliwa tena na Kamati ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, baada ya ripoti hiyo kushindwa kufafanua jinsi mabilioni ya fedha yaliyotengwa kwa miradi ya maendeleo, yalivyotumuka.

Kukataliwa kwa ripoti hiyo kumempa wakati mgumu Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza, Halifa Hida, ambaye amehamishiwa jijini hapa hivi karibuni.

Chini ya uenyekiti wa Dk Hamis Kigwangalla, kamati hiyo ya bunge licha ya kubaini matumizi mabaya ya fedha za miradi iliyokusudiwa, pia ilibaini kutokuwepo kwa umakini katika utendaji wa kazi wa maofisa wa Jiji la Mwanza, ambalo ni la pili kwa ukubwa nchini.

Kutokana na mkanganyiko huo, Mwenyekiti wa kamati hiyo, Dk Kigwangalla alidai kuwa ripoti iliyotayarishwa kwa mara ya pili kama ilivyokuwa ya awali, haieleweki.

Akizungumza katika ukumbi wa halmashauri hiyo jana, Dk Kigwangalla alisema majibu yaliyotolewa baada ya taarifa ya awali kuhusu miradi mbalimmbali ya maendeleo, si ya kweli na kwamba yanaipotosha kamati.
Aliwataka watendaji kuandaa nyaraka zote za miradi ukiwemo ule wa ujenzi wa Kituo cha Biashara cha Kimataifa cha Mwanza.

"Kamati imesikitishwa sana na namna ya uandaaji wa taarifa ya halmashauri ya jiji hili, hii ni pesa ya umma inakuwaje mtu unakosea kujumlisha hesabu na kutoa takwimu ambazo si sahihi kabisa," alihoji Dk Kigwangalla.
 
Wizi wa fedha za umma katika Nchi hii si mgeni masikioni mwetu,kigeni masikioni mwetu na ambacho tungependa kukisikia ni hao wezi kukamatwa na kufungwa.
 
Na hapo wamekutana na taarifa mbovu watendaji walioiandaa wako wapi na wanafanya nini au wamefanyiwa nini
Je hao ambao wanasekana kuidhinisha matumizi ya hayo mamilioni wamefanyiwa nini au wameambiwa wakaandae taarifa nyingine wafiche namna pesa zilivyotumika
 
Hapa wanataka kutuonesha wanafuatilia ufujaji wa Mali ya umma, tunataka kujua watachukua hatua gani ili kukomesha hivi vitendo, na hiyo ripoti hata iandikwe mara 20 haitokuwa sawa, wameshagundua matumizi mabaya na kubaini utendaji Usilolijua makini sasa wanategemea ripoti itakaa sawa kweli.?
 
Na Annastazia Fredy, Mwananchi

Posted Jumapili,Februari2 2014 saa 6:0 AM

KWA UFUPI
Kukataliwa kwa ripoti hiyo kumempa wakati mgumu Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza, Halifa Hida, ambaye amehamishiwa jijini hapa hivi karibuni.

Mwanza. Ripoti ya mapato na miradi ya maendeleo ya Jiji la Mwanza, imekataliwa tena na Kamati ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, baada ya ripoti hiyo kushindwa kufafanua jinsi mabilioni ya fedha yaliyotengwa kwa miradi ya maendeleo, yalivyotumuka.

Kukataliwa kwa ripoti hiyo kumempa wakati mgumu Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza, Halifa Hida, ambaye amehamishiwa jijini hapa hivi karibuni.

Chini ya uenyekiti wa Dk Hamis Kigwangalla, kamati hiyo ya bunge licha ya kubaini matumizi mabaya ya fedha za miradi iliyokusudiwa, pia ilibaini kutokuwepo kwa umakini katika utendaji wa kazi wa maofisa wa Jiji la Mwanza, ambalo ni la pili kwa ukubwa nchini.

Kutokana na mkanganyiko huo, Mwenyekiti wa kamati hiyo, Dk Kigwangalla alidai kuwa ripoti iliyotayarishwa kwa mara ya pili kama ilivyokuwa ya awali, haieleweki.

Akizungumza katika ukumbi wa halmashauri hiyo jana, Dk Kigwangalla alisema majibu yaliyotolewa baada ya taarifa ya awali kuhusu miradi mbalimmbali ya maendeleo, si ya kweli na kwamba yanaipotosha kamati.

Aliwataka watendaji kuandaa nyaraka zote za miradi ukiwemo ule wa ujenzi wa Kituo cha Biashara cha Kimataifa cha Mwanza.

“Kamati imesikitishwa sana na namna ya uandaaji wa taarifa ya halmashauri ya jiji hili, hii ni pesa ya umma inakuwaje mtu unakosea kujumlisha hesabu na kutoa takwimu ambazo si sahihi kabisa,” alihoji Dk Kigwangalla
 
Hili ni suala la kawaida sana ktk serikali iliyo chini ya Chama Sikivu.
 
Kama baba ni mwizi unategemea watoto watakua wema!?. Baba alipiga EPA, RICHMOND, DEEPGREEN, MEREMETA etc watoto wanakwapua kwenye halmashauri, wizarani, kwenye tenda na rushwa za barabarani. Na hakuna wa kumwadhibu mwenzake!
 
Umbea unalipa mkurugenzi kahamishiwa wapi tena?
 
Wanacheza na Dr kigwangalla safari hii atawavuta mabongolo masalia yoooote ya magamba humo mwanza.na vilevile wanatakiwa wamueleze hela zooote za kuwalipa wenye tenda za kuzoa taka zinaendaje? maana uchafu una nuka kama mavi mfano buzuruga dampo Igoma nyegezi ngokozi tishio ni Kirumba kwa Lakairo ni kituko .mwakani utawaona wanasimamakwenye majukwaa tuwape kura watatujengea barabara za juu Mwanza-Dar .Kweri wanajamvi hii inaingia akilini? hatudanganyiki.
 
Back
Top Bottom