Kamati ya nidhamu ya CCM imemfanya nini Lusinde?

mwandiga

JF-Expert Member
Dec 5, 2011
1,506
661
Kwa maneno yake machafu, ambayo hayapaswi kutamkwa na binadamu na kama mtoto wake angekuwepo eneo hilo angemkana kuwa lusinde sio baba yake, sijajua ni uamuzi gani au nini kamati ya ccm imemfanyia huyu bwana. Nape nauye aje hapa atuambie maana amezoea kuongea sana na kwahili la lusinde aje aseme kama sheria za uchaguzi ziliruhusu ccm kutumia matusi kutukana CHADEMA na ni kifungu gani cha hiyo sheria, na polisi waliokuwepo hapo uwanjani walifanya au walichukua hatua gani baada ya kuona matapishi yaliyooza yanatoka mdomoni mwa lusinde.
ccm tuelezeni ni nini mmefanya kwani ni aibu kuanzia kwa kikwete hadi wa mwisho kwenye chama
 
Kwa ccm tuijuayo hayo ni matusi kama tu yakitolewa na mpinzani wa ccm. Hapo hata msajili wa vyama ungeshamsikia akilaani na polisi wasingesubiri amri. Ila kwa hili utasikia yale yalikuwa mambo ya kampeni na sasa yamepita. Wenyewe tumpandishe Lusinde kizimbani ndo tuuone utetezi wa ccm huko!
 
Back
Top Bottom