Kamati ya Mzee Ruksa "Msekwa alia na Sitta"

Ngongo

Ngongo

JF-Expert Member
Joined
Sep 20, 2008
Messages
12,432
Likes
4,114
Points
280
Ngongo

Ngongo

JF-Expert Member
Joined Sep 20, 2008
12,432 4,114 280
Makamu mwenyekiti wa CCM Tanzania bara Bwana Pius Msekwa ameelezwa kutaka Spika wa bunge Mheshimiwa Samwel Sitta achukuliwe hatua kali za kinidhamu pamoja na wabunge wote wanaounga mkono vita vya ufisadi.

Ikumbukwe Bwana Pius Msekwa alipoteza nafasi yake ya Uspika baada ya kushindwa na mheshimiwa Sitta.Bwana Msekwa amekuwa akionyesha chuki za waziwazi kwa mheshimiwa Sitta.Hata hivyo Msekwa amekuwa akipata pingamizi kutoka kwa wajumbe wenzake,akiwemo Mzee Ruksa na spika wa kwanza wa jumuiya ya Afrika mashariki Bwana A kinana.

Wakati Bwana kinana ameelezwa kuwa na msimamo mkali zaidi akitaka pande zote husika zichukuliwe hatua kulingana na uzito wa tuhuma kwa watuhumiwa wa ufisadi kushughulikiwa kukisafisha chama na Mheshimiwa Sitta na wenzake kukemewa.

Chanzo raia mwema
 
Regia Mtema

Regia Mtema

R I P
Joined
Nov 21, 2009
Messages
2,974
Likes
31
Points
0
Regia Mtema

Regia Mtema

R I P
Joined Nov 21, 2009
2,974 31 0
Makamu mwenyekiti wa CCM Tanzania bara Bwana Pius Msekwa ameelezwa kutaka Spika wa bunge Mheshimiwa Samwel Sitta achukuliwe hatua kali za kinidhamu pamoja na wabunge wote wanaounga mkono vita vya ufisadi.

Ikumbukwe Bwana Pius Msekwa alipoteza nafasi yake ya Uspika baada ya kushindwa na mheshimiwa Sitta.Bwana Msekwa amekuwa akionyesha chuki za waziwazi kwa mheshimiwa Sitta.Hata hivyo Msekwa amekuwa akipata pingamizi kutoka kwa wajumbe wenzake,akiwemo Mzee Ruksa na spika wa kwanza wa jumuiya ya Afrika mashariki Bwana A kinana.

Wakati Bwana kinana ameelezwa kuwa na msimamo mkali zaidi akitaka pande zote husika zichukuliwe hatua kulingana na uzito wa tuhuma kwa watuhumiwa wa ufisadi kushughulikiwa kukisafisha chama na Mheshimiwa Sitta na wenzake kukemewa.

Chanzo raia mwema
Mmh!
 
Kabuche1977

Kabuche1977

JF-Expert Member
Joined
Feb 10, 2009
Messages
485
Likes
50
Points
45
Kabuche1977

Kabuche1977

JF-Expert Member
Joined Feb 10, 2009
485 50 45
mbona siielewi hii habari, au ya kizushi tu, aliyeweka thread hii atupe source yake
 
Kabuche1977

Kabuche1977

JF-Expert Member
Joined
Feb 10, 2009
Messages
485
Likes
50
Points
45
Kabuche1977

Kabuche1977

JF-Expert Member
Joined Feb 10, 2009
485 50 45
nimesoma raia mwema kwenye mtandao sijaona hayo maneno, is not the real source
 
K

Kabonde

JF-Expert Member
Joined
Aug 12, 2008
Messages
421
Likes
8
Points
0
K

Kabonde

JF-Expert Member
Joined Aug 12, 2008
421 8 0
Makamu mwenyekiti wa CCM Tanzania bara Bwana Pius Msekwa ameelezwa kutaka Spika wa bunge Mheshimiwa Samwel Sitta achukuliwe hatua kali za kinidhamu pamoja na wabunge wote wanaounga mkono vita vya ufisadi.

Ikumbukwe Bwana Pius Msekwa alipoteza nafasi yake ya Uspika baada ya kushindwa na mheshimiwa Sitta.Bwana Msekwa amekuwa akionyesha chuki za waziwazi kwa mheshimiwa Sitta.Hata hivyo Msekwa amekuwa akipata pingamizi kutoka kwa wajumbe wenzake,akiwemo Mzee Ruksa na spika wa kwanza wa jumuiya ya Afrika mashariki Bwana A kinana.

Wakati Bwana kinana ameelezwa kuwa na msimamo mkali zaidi akitaka pande zote husika zichukuliwe hatua kulingana na uzito wa tuhuma kwa watuhumiwa wa ufisadi kushughulikiwa kukisafisha chama na Mheshimiwa Sitta na wenzake kukemewa.

Chanzo raia mwema

Msekwa bado ana machungu ya kushindwa uspika hana hoja ya msingi dhidi ya six,naamini Nec itafanyakazi yake kwa uadilifu mkubwa.Mafisadi wote wakiongozwa na baba yao Lowassa mwisho wao umefika.
 
K

Kabonde

JF-Expert Member
Joined
Aug 12, 2008
Messages
421
Likes
8
Points
0
K

Kabonde

JF-Expert Member
Joined Aug 12, 2008
421 8 0
nimesoma raia mwema kwenye mtandao sijaona hayo maneno, is not the real source

Soma raiamwema ya 3 feb - 9 feb 2010 hii habari ipo kabisa Ngongo kaifupisha tu
 
Saint Ivuga

Saint Ivuga

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2008
Messages
45,431
Likes
31,659
Points
280
Saint Ivuga

Saint Ivuga

JF-Expert Member
Joined Aug 21, 2008
45,431 31,659 280
Hawa jamaa wanamwabudu Sana Lowassa
 
Luteni

Luteni

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Messages
2,274
Likes
13
Points
0
Luteni

Luteni

JF-Expert Member
Joined Jan 9, 2010
2,274 13 0
nimesoma raia mwema kwenye mtandao sijaona hayo maneno, is not the real source
Ndugu Kabuche1977 jaribu kuwa unajishughulisha umesema umesoma Raia Mwema ipi hebu soma tena vizuri usingoje kila kitu utafuniwe

Raia Mwema 3 February 2010

WAKATI Halmashauri Kuu (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi ikitarajiwa kupokea, Jumatano ijayo, taarifa ya Kamati ya Rais mstaafu, Ali Hassan Mwinyi inayotafuta njia ya kumaliza msuguano ndani ya chama hicho, mmoja wa wajumbe wa kamati hiyo ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa chama hicho, Pius Msekwa, ameelezwa kutaka Spika wa Bunge Samuel Sitta achukuliwe hatua, Raia Mwema limefahamishwa.
Habari za ndani ya CCM zimeeleza kwamba Msekwa, ambaye alipoteza nafasi yake ya Uspika baada ya kushindwa na Sitta, amekuwa akionyesha waziwazi kutaka hatua zichukuliwe dhidi ya Sitta na wabunge wanaomuunga mkono katika vita dhidi ya ufisadi.
Hata hivyo, Msekwa amekuwa akipata pingamizi kutoka kwa wajumbe wenzake, akiwamo Mzee Mwinyi, na Spika wa kwanza wa Baraza la Kutunga Sheria la Jumuiya ya Afrika Mashariki, Abdurahaman Kinana.
Wakati Kinana ameelezwa kuwa na msimamo mkali zaidi akitaka pande zote husika zichukuliwe hatua kulingana na uzito wa tuhuma, kwa watuhumiwa wa ufisadi kushughulikiwa kukisafisha chama na Sitta na wenzake kukemewa, Mzee Mwinyi amekuwa akielezwa kutumia busara zaidi kutoa maoni yake.
"Msekwa alisema wazi kwamba matatizo ya sasa yasingekuwapo kama Sitta angechukuliwa hatua na vikao vya CCM vilivyoandaliwa mahususi kumshughulikia, lakini Mzee Mwinyi akamwambia chama hicho tawala hakiendeshwi kwa jazba," anasema mtoa habari wetu ndani ya CCM.
msekwa_1.jpg

Makamu Mwenyekiti wa CCM, Pius Msekwa
Kutokana na msimamo mkali wa Msekwa, imeelezwa kwamba katika kikao kijacho cha NEC kamati hiyo itawasilisha taarifa yake lakini wajumbe wake watakua na nafasi ya kuongeza mambo kwa kuchangia, huku baadhi ya maoni yao yakielezwa kuwa mazito zaidi na yatakayozingatiwa na kuongoza mjadala.
Imeelezwa kwamba kikao kilichoandaliwa mahususi kumng'oa Sitta kiliongozwa na mashambulizi dhidi ya Spika huyo aliyejijengea heshima kubwa kwa jamii kutokana na msimamo wake, lakini yalizimwa na Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, ambaye aliwazuia baadhi ya wajumbe kutoa michango iliyoshambulia bila kuwa na hoja za msingi.
Imeelezwa kwamba hata uanzishwaji wa Chama cha Jamii (CCJ) ulitokana na matokeo ya kikao hicho kilichoonyesha kusudio la wazi la kushusha hadhi ya Spika na wabunge waliojitokeza kupambana na ufisadi, kabla ya uongozi wa juu wa CCM na serikali kutuliza hasira za kundi hilo kwa kuonyesha wazi kuliunga mkono.
"Si uliona hata Katibu Mkuu wa CCM, Yussuf Makamba, katika hali ya mshangao alikwenda Urambo nyumbani kwa kina Sitta na kuonyesha kumuunga mkono. Ile ilikuwa ni moja ya hatua za makusudi za kupooza hasira za Sitta na wanaomuunga mkono," anasema mtoa habari wetu ndani ya CCM..
Habari zinaeleza kwamba tayari kumekuwapo na wasiwasi mkubwa ndani ya kundi la watuhumiwa wa ufisadi, baada ya kubaini kuwapo kwa mabadiliko katika nyendo za baadhi ya viongozi na watendaji wa serikali dhidi yao, tofauti na ilivyokuwa awali.
"Kwa sasa mafisadi wamechanganyikiwa na wamekuwa wakihaha kutafuta mbinu za kujihami na kuvuruga mambo. Kuna wakati wanaelekea kama wanafanikiwa lakini hali si shwari kabisa kwa upande wao. Wanalishwa chambo, wakinasa wamekwisha," anasema Ofisa mmoja mwandamizi wa serikali aliye karibu na mifumo ya kisiasa.
Hayo yakijiri, CCM bado imekuwa na kiwewe cha kuanzishwa kwa CCJ huku matokeo ya kikao kijacho cha NEC yanaelezwa kuwa msingi mkuu wa kuimarika ama kufa kwa chama hicho kipya kinachohusishwa na vigogo ndani ya CCM.
sitta_2.jpg

Samuel Sitta, Spika wa Bunge
Pamoja na kuwapo makundi mengi ndani ya CCM, makundi mawili ndiyo yanayotajwa kuwa chachu ya misuguano ndani ya chama hicho, yakiongozwa na wanasiasa wawili wazito, Sitta na Waziri Mkuu aliyejiuzulu kwa kashfa Edward Lowassa, wanasiasa ambao kwa sasa ndio wanaokiyumbisha chama hicho tawala.
Tayari kulikuwa na maelekezo kutoka kwa Mwenyekiti wa CCM, Rais Kikwete, alishauri kuwapo maridhiano kati ya kundi la Lowassa na Sitta, pendekezo ambalo limekwama kutokana na kila upande kuuamini liko sahihi.
Habari za karibu na Kamati ya Mwinyi zinasema kwamba baada ya kukutana na wahusika wa pande zote mbili, kundi la Lowassa lilielezwa kukubali maridhiano lakini kwa sharti la kuombwa radhi hadharani ikiwamo ndani ya Bunge, pendekezo ambalo lilipingwa vikali na Sitta akibainisha kwamba hakuna "ugomvi binafsi" kati yao bali masuala yanayowagusa Watanzania wote ambao hawajahojiwa na kamati hiyo.
Kiongozi mmoja wa CCM ameliambia Raia Mwema kwamba hoja ya kukisafisha chama imekuwa ikisubiriwa kwa hamu na wajumbe wengi wa NEC ambao wamepokea maoni ya wananchi katika maeneo yao ambao wameelezwa kuchoshwa na matusi kutoka kwa wapinzani kwamba chama chao ni cha mafisadi.
"Nashangaa watu wanashangilia eti mafisadi kutochukuliwa hatua. Hakuna mtu aliyetaja fisadi ni nani na kwamba kama kuna mtu anashangilia wahalifu kutochukuliwa hatua basi huyo hana akili timamu ama amepumbazwa na ufisadi. Ndio maana Dk. Harrison Mwakyembe (Mbunge wa Kyela) alisema kuna ujasiri wa kisiasa," anasema mjumbe mmoja wa NEC kutoka kanda ya ziwa.
 
Jayfour_King

Jayfour_King

JF-Expert Member
Joined
Nov 15, 2009
Messages
1,141
Likes
12
Points
0
Jayfour_King

Jayfour_King

JF-Expert Member
Joined Nov 15, 2009
1,141 12 0
Wagombanapo tembo ziumiazo ni nyasi, yetu sisi macho na masikio.
 
Field Marshall ES

Field Marshall ES

JF-Expert Member
Joined
Apr 27, 2006
Messages
12,659
Likes
92
Points
0
Field Marshall ES

Field Marshall ES

JF-Expert Member
Joined Apr 27, 2006
12,659 92 0
Ndugu Kabuche1977 jaribu kuwa unajishughulisha umesema umesoma Raia Mwema ipi hebu soma tena vizuri usingoje kila kitu utafuniwe

Raia Mwema 3 February 2010

WAKATI Halmashauri Kuu (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi ikitarajiwa kupokea, Jumatano ijayo, taarifa ya Kamati ya Rais mstaafu, Ali Hassan Mwinyi inayotafuta njia ya kumaliza msuguano ndani ya chama hicho, mmoja wa wajumbe wa kamati hiyo ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa chama hicho, Pius Msekwa, ameelezwa kutaka Spika wa Bunge Samuel Sitta achukuliwe hatua, Raia Mwema limefahamishwa.
Habari za ndani ya CCM zimeeleza kwamba Msekwa, ambaye alipoteza nafasi yake ya Uspika baada ya kushindwa na Sitta, amekuwa akionyesha waziwazi kutaka hatua zichukuliwe dhidi ya Sitta na wabunge wanaomuunga mkono katika vita dhidi ya ufisadi.
Hata hivyo, Msekwa amekuwa akipata pingamizi kutoka kwa wajumbe wenzake, akiwamo Mzee Mwinyi, na Spika wa kwanza wa Baraza la Kutunga Sheria la Jumuiya ya Afrika Mashariki, Abdurahaman Kinana.
Wakati Kinana ameelezwa kuwa na msimamo mkali zaidi akitaka pande zote husika zichukuliwe hatua kulingana na uzito wa tuhuma, kwa watuhumiwa wa ufisadi kushughulikiwa kukisafisha chama na Sitta na wenzake kukemewa, Mzee Mwinyi amekuwa akielezwa kutumia busara zaidi kutoa maoni yake.
“Msekwa alisema wazi kwamba matatizo ya sasa yasingekuwapo kama Sitta angechukuliwa hatua na vikao vya CCM vilivyoandaliwa mahususi kumshughulikia, lakini Mzee Mwinyi akamwambia chama hicho tawala hakiendeshwi kwa jazba,” anasema mtoa habari wetu ndani ya CCM.
msekwa_1.jpg

Makamu Mwenyekiti wa CCM, Pius Msekwa
Kutokana na msimamo mkali wa Msekwa, imeelezwa kwamba katika kikao kijacho cha NEC kamati hiyo itawasilisha taarifa yake lakini wajumbe wake watakua na nafasi ya kuongeza mambo kwa kuchangia, huku baadhi ya maoni yao yakielezwa kuwa mazito zaidi na yatakayozingatiwa na kuongoza mjadala.
Imeelezwa kwamba kikao kilichoandaliwa mahususi kumng’oa Sitta kiliongozwa na mashambulizi dhidi ya Spika huyo aliyejijengea heshima kubwa kwa jamii kutokana na msimamo wake, lakini yalizimwa na Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, ambaye aliwazuia baadhi ya wajumbe kutoa michango iliyoshambulia bila kuwa na hoja za msingi.
Imeelezwa kwamba hata uanzishwaji wa Chama cha Jamii (CCJ) ulitokana na matokeo ya kikao hicho kilichoonyesha kusudio la wazi la kushusha hadhi ya Spika na wabunge waliojitokeza kupambana na ufisadi, kabla ya uongozi wa juu wa CCM na serikali kutuliza hasira za kundi hilo kwa kuonyesha wazi kuliunga mkono.
“Si uliona hata Katibu Mkuu wa CCM, Yussuf Makamba, katika hali ya mshangao alikwenda Urambo nyumbani kwa kina Sitta na kuonyesha kumuunga mkono. Ile ilikuwa ni moja ya hatua za makusudi za kupooza hasira za Sitta na wanaomuunga mkono,” anasema mtoa habari wetu ndani ya CCM..
Habari zinaeleza kwamba tayari kumekuwapo na wasiwasi mkubwa ndani ya kundi la watuhumiwa wa ufisadi, baada ya kubaini kuwapo kwa mabadiliko katika nyendo za baadhi ya viongozi na watendaji wa serikali dhidi yao, tofauti na ilivyokuwa awali.
“Kwa sasa mafisadi wamechanganyikiwa na wamekuwa wakihaha kutafuta mbinu za kujihami na kuvuruga mambo. Kuna wakati wanaelekea kama wanafanikiwa lakini hali si shwari kabisa kwa upande wao. Wanalishwa chambo, wakinasa wamekwisha,” anasema Ofisa mmoja mwandamizi wa serikali aliye karibu na mifumo ya kisiasa.
Hayo yakijiri, CCM bado imekuwa na kiwewe cha kuanzishwa kwa CCJ huku matokeo ya kikao kijacho cha NEC yanaelezwa kuwa msingi mkuu wa kuimarika ama kufa kwa chama hicho kipya kinachohusishwa na vigogo ndani ya CCM.
sitta_2.jpg

Samuel Sitta, Spika wa Bunge
Pamoja na kuwapo makundi mengi ndani ya CCM, makundi mawili ndiyo yanayotajwa kuwa chachu ya misuguano ndani ya chama hicho, yakiongozwa na wanasiasa wawili wazito, Sitta na Waziri Mkuu aliyejiuzulu kwa kashfa Edward Lowassa, wanasiasa ambao kwa sasa ndio wanaokiyumbisha chama hicho tawala.
Tayari kulikuwa na maelekezo kutoka kwa Mwenyekiti wa CCM, Rais Kikwete, alishauri kuwapo maridhiano kati ya kundi la Lowassa na Sitta, pendekezo ambalo limekwama kutokana na kila upande kuuamini liko sahihi.
Habari za karibu na Kamati ya Mwinyi zinasema kwamba baada ya kukutana na wahusika wa pande zote mbili, kundi la Lowassa lilielezwa kukubali maridhiano lakini kwa sharti la kuombwa radhi hadharani ikiwamo ndani ya Bunge, pendekezo ambalo lilipingwa vikali na Sitta akibainisha kwamba hakuna “ugomvi binafsi” kati yao bali masuala yanayowagusa Watanzania wote ambao hawajahojiwa na kamati hiyo.
Kiongozi mmoja wa CCM ameliambia Raia Mwema kwamba hoja ya kukisafisha chama imekuwa ikisubiriwa kwa hamu na wajumbe wengi wa NEC ambao wamepokea maoni ya wananchi katika maeneo yao ambao wameelezwa kuchoshwa na matusi kutoka kwa wapinzani kwamba chama chao ni cha mafisadi.
“Nashangaa watu wanashangilia eti mafisadi kutochukuliwa hatua. Hakuna mtu aliyetaja fisadi ni nani na kwamba kama kuna mtu anashangilia wahalifu kutochukuliwa hatua basi huyo hana akili timamu ama amepumbazwa na ufisadi. Ndio maana Dk. Harrison Mwakyembe (Mbunge wa Kyela) alisema kuna ujasiri wa kisiasa,” anasema mjumbe mmoja wa NEC kutoka kanda ya ziwa.
- Uzuri wa hii ishu ni kwamba wafadhili wapo pembeni wakiifuatilia kwa makini sana, mchawi wa Msekwa alikuwa ni yeye mwenyewe Mtandao walimtumia mjumbe Marehemu Amina, kwamba hawamuhitaji, yeye akakimbilia kwa Rais kulia eti nasikia hunihitaji, Muungwana akamponza zaidi akaishia kulizwa, aliyemliza ni marehemu Akukweti, kutokana na uamuzi wa Rostam, aliyekua pia muajiri wa Msekwa kule Vodacom na ndiye aliyemrudisha tena,

- Sasa kama Msekwa ana hasira na Six basi sio taabu hapa kujua anamuwakilisha nani! Ndio maana ninasema uzuri ni kwamba wafadhili wapo karibu sana na hii ishu! CCM haijawahi kucheza na wafadhili hata siku moja, kwa hiyo hapa mafisadi wamepiga chini, puuh! Kinana amesema mara nyingi sana in private kwamba anataka mafisadi wote wafungwe jela na wafukuzwe CCM!

Respect.

FMEs!
 
Ngongo

Ngongo

JF-Expert Member
Joined
Sep 20, 2008
Messages
12,432
Likes
4,114
Points
280
Ngongo

Ngongo

JF-Expert Member
Joined Sep 20, 2008
12,432 4,114 280
- Uzuri wa hii ishu ni kwamba wafadhili wapo pembeni wakiifuatilia kwa makini sana, mchawi wa Msekwa alikuwa ni yeye mwenyewe Mtandao walimtumia mjumbe Marehemu Amina, kwamba hawamuhitaji, yeye akakimbilia kwa Rais kulia eti nasikia hunihitaji, Muungwana akamponza zaidi akaishia kulizwa, aliyemliza ni marehemu Akukweti, kutokana na uamuzi wa Rostam, aliyekua pia muajiri wa Msekwa kule Vodacom na ndiye aliyemrudisha tena,

- Sasa kama Msekwa ana hasira na Six basi sio taabu hapa kujua anamuwakilisha nani! Ndio maana ninasema uzuri ni kwamba wafadhili wapo karibu sana na hii ishu! CCM haijawahi kucheza na wafadhili hata siku moja, kwa hiyo hapa mafisadi wamepiga chini, puuh! Kinana amesema mara nyingi sana in private kwamba anataka mafisadi wote wafungwe jela na wafukuzwe CCM!

Respect.FMEs!

[FONT=&quot]Heshima kwako FMES,

Maneno yako mazito sana tunaomba Mungu hawa mafisadi mwaka huu uwe mwisho wao.Kuna kila sababu waTanzania wote bila kujali itikadi kuhakikisha makuwadi wote wanaowabeba mafisadi hawakatizi wala hawapati heshima mbele ya jamii.[/FONT]
 
K

kisikichampingo

Senior Member
Joined
Oct 28, 2009
Messages
129
Likes
3
Points
35
K

kisikichampingo

Senior Member
Joined Oct 28, 2009
129 3 35
Jayfour_king mbona hueleweki? Wagombanapo tembo ziumiazo nyasi. Yetu sisi macho na masikio. Nyasi ni nani? Kama nyasi ni sisi, kwa nini tukae kimya?
 
B

Boramaisha

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2009
Messages
820
Likes
6
Points
0
B

Boramaisha

JF-Expert Member
Joined Apr 29, 2009
820 6 0
Msekwa ni gwiji wa fitina!
 
K

Kabonde

JF-Expert Member
Joined
Aug 12, 2008
Messages
421
Likes
8
Points
0
K

Kabonde

JF-Expert Member
Joined Aug 12, 2008
421 8 0
Mzee Msekwa yuko kwenye nafasi za uongozi tangu nchi yetu ipate uhuru nashangaa sana mpaka leo bado hataki kupumzika bado anaendeleza fitina zake.Alitaka kina Lowassa wasiguswe katika kashfa ya Richadmonduli
 
Forum statistics

Threads 1,237,961
Members 475,776
Posts 29,307,965