Kamati ya maadili ya bunge inapokiagiza CCM kimchukulie hatua zaidi askofu Gwajima maana yake nini? Mbona CHADEMA ilipuuzwa?!

Jana kamati ya Haki na maadili ya Bunge imeitaka CCM kumchukulia hatua zaidi za kinidhamu askofu Gwajima.

Ninachojiuliza ni je CCM ndio yenye meno zaidi kuliko bunge?

Mbona CHADEMA iliwafukuza akina Halima Mdee lakini bado ni wabunge?

Mbona Cecil Mwambe alijivua uanachama wa CHADEMA lakini akaambiwa aendelee na ubunge kwa sababu waliompigia kura ni Wananchi na siyo CHADEMA.

Je, tunaelekea kwenye mfumo wa chama kushika hatamu?

Maendeleo hayana vyama!
Wanazidi kujianika Kwa matendo Yao maovu dhidi ya wasiowapenda. Bunge chini ya Ndugai ni sawa na Wizara ya Fedha chini ya Mwigulu yaani ni mzigo kwa Taifa.
 
Back
Top Bottom